Je kampuni zinakopa benki kwa dhamana gani?

Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
218
Reaction score
318
Habari za leo wanabodi.
Naomba kujua Jambo hili. Katika ukopaji wa kawaida huwa tunalazimika kuwa na Shaman ya Mali isiyo hamishika na pengine iwe na thamani sawa au zaidi ya kiwango cha mkopo kinacho ombwa. Sasa napenda Kujua juu wa makampuni, Yanapo kopa hulazimika kuwa na dhamana kama hizo?. Na je, kuna mazingira yoyote ya kampuni kukopa bila kuwa na dhamana ya mali isiyo hamishishika?
Nina thamini michango yenu nyote.
Naomba kuwasilisha.
 
Kampuni ina majengo. Ina mitambo. Ina viwanja. Stock. Madeni (debtors) n.k so ili iweze kukopa ni lazima iwe ña statements za fedha zinazoonesha mkopo utarudi na kama cyo ivo basi hutumia Mali nlizozitaja kama dhamana endapo ni secured loan. Na ndio maana ikifirisika huwa inauza mali zake kufidia madeni kwa wadai wake.
 
Asante kwa majibu, Umenipa mwanga kwa kiasi flani. Labda sasa niingie Google kutafuta zaidi. Pia na wengine naamini watajazia nyama zaidi.
 
Kwanza tujiulize "Kampuni" ni nani?

Kampuni ni legal person kisheria, yaani Kampuni anaweza kumiliki property, kuingia mkataba, kukopa, nk kama mtu wa kawaida anavyoweza.

Linapokuja suala la kumkopesha kampuni, mabenki huwa wanamfanyia kampuni assessment juu ya kiwango cha mkopo na pia kama anao uwezo wa kulipa huo mkopo kwa kuangalia financial statements za huyo kampuni.

Kwenye financial statements za kampuni tutaona mali anazomiliki, madeni alokua nayo mpaka sasa na pia mtaji aliokua nao. Vilevile tutaweza kuona faida anayotengeneza kila mwezi, na gharama zake za uzalishaji au uendeshaji.

tukijiridhisha kuwa kampuni ana hali nzuri ya kifedha (ataweza kulipa mkopo), basi tutampatia huo mkopo. akishindwa kulipa baadae tutampeleka mahakamani, mahakama itam-declare bankruptcy kisha mali za kampuni zitauzwa ili kuwalipa watu wanaomdai.
 
Nmekuelewa zaidi ya sana boss ubarikiwe
 
Back
Top Bottom