Je, kansa ya koo inatibika? Nipo njia panda

Je, kansa ya koo inatibika? Nipo njia panda

khamis kilo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
1,137
Reaction score
1,380
Habari wanaJamiiForums,

Nimepata changamoto kwa mzazi wangu kwa kusumbuliwa na uvimbe katika koo na tulivyoenda hospitali ya taifa Muhimbili alifanyiwa kipimo kinachoitwa (OGD) ni kipimo hatara sana kama una moyo mdogo unaweza ukakimbia maana unasokomezwa limpira mdomoni hadi kwenye koo, baada ya kupata kipimo hicho cha OGD tulirudi nyumbani hadi majuzi tulipoenda tena hospitali kupata majibu ya vipimo na ndipo tulipoambiwa kuwa kuna tatizo la kansa kwenye koo.

Sasa basi, kitu nisichoelewa: je, kansa ya kwenye koo inatibika kwa njia ya upasuaji au kwa kupewa dawa au kwa mionzi? maana huku katika familia watu tuna hofu juu ya kutibika kwa kansa ya koo huku wengine wakisema kupona kansa ya koo ni mtihani.

Ushauri wenu jamani kuhusu ili tatizo la kansa ya koo kutibika au lah.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
khamis kilo, Inatibika kama haijafikia stage ya 3..najua wengi wamepona kabisa. ila wapo waliolazimika kufanyiwa oparesheni ambayo iliondoa uwezo wa kuongea tena..unakuwa kama bubu sauti haitoki.

Najua juice za staferi sijui topetope..juice ya karoti isiyo tiwa maji..matunda jamii ya fenesi..yanasaidia sana sana kupambana na seli za kansa.

Kuna watu wanashuhuda humu watakuja. Usiache matibabu ya hosp huku ukitumia sana sana hivyo nilivyokwambia.

Jitahidi sana ingia Google uliza home remedies for cancer na hasa YouTube..utapata maelekezo mengi sana sana.

Msikate tamaa wengi wamepona no matter what my friend.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
khamis kilo, Inatibika kama haijafikia stage ya 3..najua wengi wamepona kabisa.ila wapo waliolazimika kufanyiwa oparesheni ambayo iliondoa uwezo wa kuongea tena..unakuwa kama bubu sauti haitoki.

Asante sanaaaaa [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pole sana bro kwa kuuguliwa na mzazi wako,

Kuanzia sasa anapaswa aanzwe kupewa mlo kamili, epuka Nyama ya aina yoyote, Mboga mboga na matunda ndio iwe mlo wake, Aepuke SUKARI kabisa, Chumvi iwe kidogo sana, Tangawizi na Thom viwekwe katika kila mlo wake,

Tengenezeni juice ya mstafeli lita moja kila siku, Tengenezeni juice ya Komamanga lita moja kila siku,
Anywe mafuta ya habati sauda kila siku, Aondoshwe stress, awe mwenye furaha na mwenye kusikia mazuri.

Anywe maji safi kila siku.
 
Pole sana bro kwa kuuguliwa na mzazi wako,

Kuanzia sasa anapaswa aanzwe kupewa mlo kamili, epuka Nyama ya aina yoyote,
Mboga mboga na matunda ndio iwe mlo wake,...

Asante kaka kwa ushauri
 
Wakati mnatafakari cha kufanya tumieni dawa za kiswahili wengine wanasema matunda ya stafeli wengine wanssema majani sina uhakika kwa hilo
 
h ndo iliondoa uhai wa mume wa mwanamuzik celine dione.mungu ampe wepes mgonjwa apone
 
Back
Top Bottom