Hii case ya huyu binti Lulu ina mambo mengi sana ya kujiuliza.....hope we had forensic expertise in the country..lakini hamna na kuna hatari sana ukweli halisi wa kilichotokea usijulikane.....kama ambavyo inakuwaga kwenye case nyiiingi tu TZ.....Ukosefu wa taaluma ya forensic medicine lazima utaathiri kesi hii.....mfano: kwenye post mortem investigations kumeonesha kuwa marehemu Kanumba alipata brain concussion(mshtuko wa ubongo)uliopelekea kuzimika kwa mfumo wake wa hewa na hata kupoteza maisha.....Ijulikane tu kuwa mshtuko wa ubongo hutokea kwa kugonga/kugongwa/au mtikisiko mkubwa wa kichwa....ambao unaweza kusababishwa na either kuanguka na kujigonga chini/ukutani au kugongwa na mtu mwingine......hapa ili kupata jibu la hakika la kilichotokea lazima kuwe na mambo ya forensic medicine expertise...mfano kupima DNA traces kwa vitu vilivyokuwepo around chumbani n.k...n.k.....kifupi kunahitajika uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane...jambo ambalo sidhani kama kwa TZ yetu litafanyika.....nionavyo watachukua tu short cuts.....kwa vigezo vya kimazingira......na kumtia/kutomtia hatiani huyo binti.
Tukija upande mwingine.......nimesoma gazeti la daily news hapa....soma...
http://www.dailynews.co.tz/index.ph...ice-work-on-clues-to-cause-of-kanumba-s-death> Ukisoma hii story ya mkuu wa polisi Kinondoni Charles Kenyela inasema.....kwa maelezo na makovu ya kutoka kwa huyo binti ...inaonyesha marehemu katika ugomzii wao alimpiga kwa panga(michete)Lulu katika sehemu zake za siri.....jambo ambalo anasema kwa sasa Lulu anauguzia majeraha madogo madogo kwenye sehemu zake za siri......Sasa kwa kuangalia hizi info naweza kusema tu hii case ni kubwa sana na inahitaji investigations beyond the just condected postmortem......ili ku rule out homicide au manslaughter au suicide......