Je katiba mpya ni hisani ya rais Magufuli au uamuzi wa wananchi?

Je katiba mpya ni hisani ya rais Magufuli au uamuzi wa wananchi?

Alosema sio ajenda yake sababu haikuwa kipaumbele kwenye kampeni zake. Raisi hawezi kuzuia mchakato wa Katiba mpya sababu mchakato wake upo kwa mujibu wa sheria


Hivi unaelewa unachokiongea? huo mchakato ulikuwa umefikia wapi na ni nani anatakiwa auendeleze?
 
Hivi unaelewa unachokiongea? huo mchakato ulikuwa umefikia wapi na ni nani anatakiwa auendeleze?
Kasome sheria namba 8 ya mwaka 2011 (sura ya 83 ya sheria za tanzania toleo la mwaka 2012), pamoja na na sheria namba 2 ya mwaka 2012, na G.N. namba 394 ya mwaka 2011. Usipende kubisha kama hujui kitu
 
Kwa mujibu wa katiba iliyopo rais hahojiwi wala kuwajibika kwa mtu au chama chochote, anatenda anachotaka.

Vv
 
Raisi hashikilii mchakato. Mchakato umewekwa kwa mujibu wa sheria. Kubalini tu viongozi wenu wanapuyanga tu hawajitambui, msimsingizie Raisi.
Unamtengaje rais na mkwamo wa katiba na kuwalaumu viongozi?

Vv
 
Hao ndio wenye madaraka ya kutuletea katiba mpya? Kama hawana uwezo wananchi wakae kimya tu?

Vv
katiba ni ya mwananchi na inatengenezwa na mwananchi. Wananchi wanaongozwa na/au kupewa elimu na viongozi wao/wawakilishi. Viongozi wa upinzani kazi yao kususa na kuka nje ya bunge la katiba. unategemea nani angetengeneza katiba? Wabunge wa CCM waliikalia wakaisuka kadri watakavyo wao, na sana wacha waendelee kuiatamia kadri watakavyo wao. Narudia tena... Aliyekwamisha mchakato wa katiba mpya ni UKAWA.
 
Back
Top Bottom