Chulumeshy
Member
- Jul 27, 2022
- 17
- 11
Lawama na kelele zinazoendelea kuhusiana na uanzishwaji wa tozo za miamala na za kifedha sasa zimekuwa kama kelele za chura akiwa kwenye maji kwani hayamzuii tembo kuyanywa maji apatapo kiu.
Lawama na malalamiko mengi yameanza mwaka 2021 baada ya serikali kuanzishwa kwa tozo mbalimbali kwa lengo la kuinua uchumi wa Taifa kwa kasi jambo lililopelekea kupandishwa kwa tozo katika makampuni ya simu na hata taasisi za kifedha kama vile benki.
Lakini mwanzoni watumiaji wakubwa wa huduma hizi walilalamika kwa kuwa makato ni makubwa sana na kudai makato hayo yaweze kupunguzwa jambo ambalo limekuwa kama kelele zisizokuwa na faida kwani japokuwa kuna madai na malalamiko mengi kuhusiana na kupandishwa kwa kodi na tozo lakini bado watumiaji wengi wamezidi kutumia huduma hizo huku takwimu zikioneshwa kwamba matumizi hayo yanazidi kupanda kama BoT
Na hat idadi ya mawakala imeongezeka jambo linaloonesha kuwa watumiaji wanazidi kutumia kwa kasi na wamekubaliana na tozo hizo.
Hata hivyo, hivi karibuni tozo za miamala ya kibenki nayo imeanzishwa huku watu wengi wakilalamikia madai hayo na wakati huo huo takwimu zilizotolewa na BoT zinaonesha kuwa watumiaji wa miamala ya kibenki ni wachache kuliko watumiaji wa miamala ya Makampuni ya simu.
Swali linabaki Je, kelele hizi zitakuwa ni za bure kama za tozo za miamala ya simu au zitafanyiwa kazi na watumiaji kwa ujumla na wakati bado watu wanatumia kwa kasi huku takwimu zinaonesha kuwa kila siku inazidi tu kupanda?