waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 197
- 468
Je, kesi ya kuchukua Mlungula inayomkabili Mutalemwa Kishenyi Haki itatendeka au yale yale?
Mnamo tarehe 23/4/2021 majira ya saa mbili usiku mwnasheria Mwandamizi katika ofisi ya mashtaka ya wilayani Babati mkoani Manyara alikamatwa akipokea rushwa ya shilingi milioni tano (5,000,000) inaeleweka kwamba alikamatwa na watumishi waadilifu wa TAKUKURU kwa kukataa mazungumzo na huyo mkware kwani angeendeleza tabia ya kuwaibia wananchi wakati amevaa makoti na skafu nyeupe za heshima.
Toka wakati alipokamatwa hadi leo kesi hiyo imekuwa kimya ni kama kawaida yetu,inasemekana yuko anahangaika kujinasua kwenye kadhia hiyo,hapo ndipo linapojidhihirisha tatizo letu mojawapo tulilonalo sisi wenyeji wa nchi yetu “Mama Tanzania “🇹🇿 .
Tatizo hili ni kufanya mambo yasiyostahili bila kujali kwa lugha ya kigeni “impunity “Hii inatokana na tabia ya watu waliopewa madaraka mbalimbali ya umma kuyatumia vibaya na wanapokamatwa kuibuka wengine wanaokuwa watetezi na watetezi hawa huwa ama ndugu wenye maumivu kutokana na mahusiano ya kifamilia ama wafanyakazi wenza wao wenye tabia hizo zinazolalamikiwa.
Katika hali hii watu wenye madaraka ya umma wamekuwa rahisi kurubuniwa na kuihujumu nchi kwa mategemeo kwamba ikitokea ajali basi watapangua kesi zinazofuata, Sasa turudi kwenye kesi ya Mwanasheria Kishenyi je tunahoji imefikia wapi? Wanaoishughulikia ni watu makini na waadilifu au ni hao hao wa aina yake wanaorubuniwa kwa pesa?Haki itatendeka?
Katika duru za wanasheria kuna usemi wanaoupendelea kwamba “Haki sio itendeke tu bali ionekane imetendeka “(justice must not only be done but it must be seen done). Tunategemea kwamba haya yatatendeka hakika kila mtu ana haki ya kujitetea na itakuwa jambo jema kujua utetezi wake huyu Mwanasheria na hatuachi kujiuliza je alikuwa anakopa hizo milioni tano?au alikuwa yeye kakopesha sasa alikuwa anarudishiwa?
Katika siku za hivi karibuni imejitokeza dhama ya majadiliano na wanaokabiliwa na mashtaka (pre bargain)tunaelewa kwamba mtu akikwepa kodi au akikwapua pesa basi inawezekana yakitokea majadiliano ya kuzirejesha fedha husika je hiyo plea bargain inaruhusiwa kwenye kesi za wahudumu wa umma wanaoshtakiwa kuchukua mlungula?Hapo ni kwamba mwanasheria Kishenyi ataruhusiwa kuzirejesha hizo milioni tano?
Hatudhani hivyo ndivyo kwa kuwa hizo pesa zipo mikononi mwa Takukuru je kwenye plea bargain hiyo atakuwa anahaidi kuwa hatachukua tena mlungula?au atahaidi kuwa hatakuwa tena mtu wa kati katika kusambaza mlungula?
Wako watumishi waliopatikana kwa kujihusisha na rushwa na walipata adhabu inayostahili kwenda jela hivyo tunategemea haki itatendeka kwa huyu mkware aliyeshobokea milioni tano ili kuhujumu nchi kwa kuachia mabilioni ya kodi za sticker za vinywaji vikali na hivi huyu Mwanasheria anajua kweli ni kwa sababu zipi serikali inaweka kodi kwenye vinywaji vikali?
Iwapo haki haitatendeka basi tutarajie rushwa itaendelea kujichimbia katika jamii yetu, juhudi za kupambana na rushwa itakuwa ni swala la kinadharia wale wanaohusika kulishughulikia hili shauri waelewe kwamba macho yetu yapo kwao.
Kuanzia hakimu, mwendesha mashtaka, maaskari wote wanaohusika tutawapiga darubini kwa nia njema.Haki itatendeka au tukubaliane kwamba nchi yetu ni ya kibaguzi.
Jambo hili litakapomalizika basi tutatoa tathmini yetu halisi.
Mwisho
Wasalaam,
,ni mimi “Mzee wa nikune huku nikune kule” 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿