Prof_Adventure_guide
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 533
- 1,499
Silaha dhidi ya wanaohoji mfumo.Kesi inayomkabili Mheshimiwa Tundu Lissu kwa mara nyingine tena mbele ya Mahakama ya Tanzania inazua hoja nzito kuhusu matumizi ya sheria kwa malengo ya kisiasa badala ya haki. Hii ni kwa sababu msingi wa mashitaka yanayomwandama unaakisi mtindo wa kurudiarudia mashitaka yenye muktadha wa kisiasa kuliko uhalisia wa jinai.
Kwa mujibu wa Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, kila mtu ana haki ya kusikilizwa mbele ya mahakama huru na isiyoegemea upande wowote. Vilevile, Ibara ya 18(a)-(d) inamlinda raia dhidi ya mateso ya kisheria kwa sababu ya kutoa maoni. Kesi hii inaashiria ukiukwaji wa kanuni hizo, kwa kuwa inaonekana dhahiri kuwa dhamira ya Jamhuri si kutafuta haki, bali kufifisha sauti ya kisiasa inayokinzana na mfumo uliopo.
Kwa kutumia nguvu ya mashtaka na vyombo vya usalama, Jamhuri inaelekea kubadili mantiki ya sheria kuwa chombo cha kudhibiti wapinzani badala ya kusimamia haki kwa wote. Hili linapunguza hadhi ya Mahakama kama chombo huru cha haki na linaweka doa katika historia ya kisheria ya nchi.
Katika mazingira haya, tunapaswa kujiuliza: Je, tunashuhudia haki ikitendeka, au sheria ikigeuzwa kuwa silaha dhidi ya wale wanaohoji mfumo?
Kinga yao nimeshangaa Jaji Mkuu Juma kuteuliwa kule Chuo Kikuu na kule kunamambo machafu je ikitokea kashfa Kinga Ile itaendelea!Kuna watu wanafurahia hii Hali lakini mioyoni wakiwa na hofu ya kinga Yao itakapotoweka vipi watakavyoishi
Amepelekwa akawahukumu waliofikisha ujumbe wa no reform no election kwa uongozi wa juu wa sirikali.Kinga yao nimeshangaa Jaji Mkuu Juma kuteuliwa kule Chuo Kikuu na kule kunamambo machafu je ikitokea kashfa Kinga Ile itaendelea!
Nchi imepatwa mambo fululu fululu
Aibu naona Mimi kapuku
Hilo lipo waziKesi inayomkabili Mheshimiwa Tundu Lissu kwa mara nyingine tena mbele ya Mahakama ya Tanzania inazua hoja nzito kuhusu matumizi ya sheria kwa malengo ya kisiasa badala ya haki. Hii ni kwa sababu msingi wa mashitaka yanayomwandama unaakisi mtindo wa kurudiarudia mashitaka yenye muktadha wa kisiasa kuliko uhalisia wa jinai.
Kwa mujibu wa Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, kila mtu ana haki ya kusikilizwa mbele ya mahakama huru na isiyoegemea upande wowote. Vilevile, Ibara ya 18(a)-(d) inamlinda raia dhidi ya mateso ya kisheria kwa sababu ya kutoa maoni. Kesi hii inaashiria ukiukwaji wa kanuni hizo, kwa kuwa inaonekana dhahiri kuwa dhamira ya Jamhuri si kutafuta haki, bali kufifisha sauti ya kisiasa inayokinzana na mfumo uliopo.
Kwa kutumia nguvu ya mashtaka na vyombo vya usalama, Jamhuri inaelekea kubadili mantiki ya sheria kuwa chombo cha kudhibiti wapinzani badala ya kusimamia haki kwa wote. Hili linapunguza hadhi ya Mahakama kama chombo huru cha haki na linaweka doa katika historia ya kisheria ya nchi.
Katika mazingira haya, tunapaswa kujiuliza: Je, tunashuhudia haki ikitendeka, au sheria ikigeuzwa kuwa silaha dhidi ya wale wanaohoji mfumo?
Kazi wanayoKesi inayomkabili Mheshimiwa Tundu Lissu kwa mara nyingine tena mbele ya Mahakama ya Tanzania inazua hoja nzito kuhusu matumizi ya sheria kwa malengo ya kisiasa badala ya haki. Hii ni kwa sababu msingi wa mashitaka yanayomwandama unaakisi mtindo wa kurudiarudia mashitaka yenye muktadha wa kisiasa kuliko uhalisia wa jinai.