Je! Kilevi kinatuweka HURU kusema hisia zetu? Ziwe Chanya au Hasi?

Bbade

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
6,725
Reaction score
21,818
Kwa yeyote yule aliyekwsiha kukaa karibu na mnywaji/wanywaji pombe, mtanielewa/mtaelewa pale kinywaji kinapo anza kumwagika mdomoni na siri zinapoanza kutoka nje.

Huu ni ukweli kwa wale tunao kunywa kila siku au wale tunao onja siku moja kwa mwezi…..

Kilevi kina kuweka huru kuonyesha hisia zako, ziwe nzuri za kupendeza au mbaya za kuumiza/kuudhi .

Je kuna ukweli kuwa yale maneno ni ya kweli na tunapaswa kuyachukulia maanani…..japokuwa yanatoka kwenye ubongo wenye kilevi?
 
ingekua hivyo bbade then kilevi kingetumika kama njia ya kupata ushahidi kwa wahalifu,ingekua kitu muhimu kwenye vituo vya police na magereza,unapiwa ka bia unatililika tu uovu wako wote (Imagine),lol 😀😀😀😀😀😀😀😀
 


Kisheria najua huruhusiwi kuamini akili ya mtu iliyo under influence.....
Tukirudi huku kwenye mambo yetu mengine....
Uko na shosti au mshikaji mnakunywa mara anaanza kukuambia siri za wengine.....
 
Tupe ukweli kwa mifano basi...maana naamini ni Mingi
Kilevi kinatabia ya kumpeleka mtu kwe 'Free Mind State' hii ni hali ya kuwa huru kimtazamo, hisia na matendo, hivyo basi katika hali hii mtu haoni shida kuwasilisha hoja zake binafsi ama mitazamo yake ama hisia zake, katika hali hii pia mtu huwa hajali madhara/matokeo ya kuwasilisha mitazamo yake.

Hapa ndipo kama kuna mtu alikua anampenda na anaogopa kumwambia kwa kuhofia 'atanifikiriaje' atamwambia ukweli, kama kuna kitu kilikua kinamkwaza moyoni pia atakisema n.k

Kilevi kina raha yake ukikitumia kwa kiasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napaswa kuyaamini?
Au kuyachukulia ni kilevi?
Maana kuna watu wanajua kutiririka acha kabisa. ..
 

Hii ni mbinu inatumika ku-extract information kutoka kwa wahalifu, mfano makundi ya kigaidi au madawa ya kulevya nk, inatumiwa zaidi na intelligence teams.

Ingawa huwezi kutumia maelezo ya mlevi mahakamani.

Kuna kitabu kinaitwa The Search For Manchurian Candidate, anasema baadhi ya team members wa makundi walikuwa wana expose information za makundi wanapokuwa wamepewa kilevi, tena kama ni bangi au pombe mnakunywa wote na CIA agent, unakuwa kama friends hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…