Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,419
Mfululizo wa marais wa nchi jirani wanaokuja kutembelea Tanzania, kipindi hiki cha kampeni una lengo la kumpigia kampeni Magufuli?
Ukianzia kwa Rais wa Uganda, ukaja kwa Rais wa Burundi na sasa Rais wa Malawi, wote lazima waongelee 'Magufuli atashinda' kwani wana uhakika gani?
Natarajia marais zaidi wa nchi jirani kujitokeza kuja kumtembelea Mwenyeji wao.
Kura za Magufuli zitatokana na mambo aliyoyafanya tangu 2015 mpaka sasa. Sisi wananchi tunafahamu nini cha kufanya hapo Oktoba 28 kwasababu aliyeridhika na mambo hayo atampigia kura na ambaye hakuridhika basi atapiga kwingine.
Huu ni uchaguzi unaoenda kuamua ama tuendelee na hali kama ya 2015-2020 au tubadilishe upepo.