Je, Kinana ni mzalendo?

Je, Kinana ni mzalendo?

Nikiwa mdogo mwaka 1986 jirani yetu ambaye alikuwa anakaa kwenye nyumba za msajili njia ya sanawari. Alikuwa mpole, mrefu na anaonekana tofauti sana kulinganisha na vijana wengine pale.

Mzee wangu ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa mkoa wa Arusha alialikwa kwenye harusi ya kinana! Cha ajabu huyu kijana alikuwa kapata ubunge na kuchaguliwa waziri mdogo wa ulinzi.

Mtaa mzima tulikuwa pilau karibu wiki nzima na waziri wa ulinzi wa wakati huu Salim Salim alikuja kwenye harusi ile ya mkeka na waligawa video tapes za harusi kila mahali. Kiukweli kinana alikuwa anapedwa kama mfalme wa Arusha mjini miaka hiyo.

Baadae tukaanza kuona dry cleaners za wasomali na kuambiwa za kinana!. Baadae Kinana akawa anajiona tofauti sana na wakazi wa kawaida nakumbuka vijiwe vya chai alikuwa hawezi kwenda tena.

Na ghafla kinana akaanza kuwa mwongeaji zaidi🤔 sio yule mpole. Lakini Arusha ikaanza kubadilika kutoka kuwa mji wa wamasai kuanza kuwa mji wa wachagga. Miaka ya 90’s Arusha mjini ukawa mji wa wafanyabiashara wahamiaji kutoka mji wa Moshi.

Wafanyabiashara wengi wa kimasai ambao walikuwa wana support sana CCM na kinana walihamia kwenye mashamba yao Arumeru, migodini na biashara nyingine baada ya wachagga kuleta ushindani mkubwa sana Arusha. Lakini wale wahindi wengi wa Arusha wenye pesa walibaki bila chama maana upepo ulikuwa unaenda upinzani.

Arusha walikuwa hawapendi serikali kwasababu ilikuwa haina mradi wowote pale mjini wa maana. Majengo yalikuwa na wauza mawe na wahindi na sio kampuni za serikali au za pesa kama Dar.

Kinana naye akaja kama mfanya biashara! Akafungua kampuni zake za utalii na uwindaji. Sawa kila majambazi wa kisomali wakishikwa kuna note inatoka juu zaidi serikalini inasema waachiwe… ni ndugu wa kinana! Hii ni mpaka leo hii🤔. Gafla miaka ya 90’s kinana akawa mfanyabiashara kuliko mwana siasa na alipoteza watu wote waliokuwa wana msupport pale mjini.

Wakati huo kulikuwa na kikundi cha wambulu wakiongozwa na tajiri wa magari verani ambaye ndiye alikuwa mbebaji wa ngano za kampuni ya bia Tanzania nzima kutoka pale karatu.

Wambulu wakalutana miaka iyo na kumchagua kinara wao ambaye ndiye Sumai awe mbunge ili nao wapate nguvu Arusha. Lakini baada ya kuona maji mazito sumay alienda kugombea kwao bahati nzuri akawa waziri! . Alivyokuja Mkapa na kumpa sumay waziri mkuu Sumay akaja Arusha na kusema yeye ndiye king mpya wa Arusha na sio kinana. Kitu cha kwanza sumay alifanya kushindana ni kuwapa vitalu wambulu mbuguni baada ya miaka michache akatokea king of Tanzanite ambaye alikuwa na jina na Sunda! ambaye alikuwa kijana wa sumay.

Hili la Sumay likamkimbiza kabisa Kinana na mpaka leo kinana sio yule mzalendo ambaye alikuwa mbunge 1986.

Nasema haya na kumwonya Raisi awe makini na kinana ni mfanyabiashara hana mapenzi na mtu. Yeye anaona kama vile ana kazi na sio wito
Hakika Kinana hajawahi kunishawishi lakini hii tabia ya Watanzania kusagiana kunguni ni rekodi ya dunia
 
Siku hizi wewe ndugu umebadirika sana, you are slave of faith,
Ungekosoa wapi nimeandika uongo...
Kinana rise ilikuja baada ya kuombwa kum replace Paul Sozigwa kama mwenyekiti wa Kampeni ya Mkapa ..1995..... vyeo vyote vilivyofata anaombwa na anapendekezwa ..
Wewe unaamini lazima tuongee nagative kuhusu Viongozi wa CCM ndo tuonekane tuko "focused"?
 
Mkuu @kamindu, Kinana ni mmoja wa wazalendo wa kweli wa nchi hii!. Ni Kinana na Nape ndio wameiokoa CCM ile 2010 to 2015 kwa zile ziara zao za amsha amsha, baada ya kusoma bandiko hili CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!, kwenye bandiko hili nilishauri

Ushauri huo ulifuatwa immediately, CCM wakamtoa Makamba, wakamuingiza Kinana, Nape na January na hapa ndio survival ya CCM ilipoanzia maana ilikuwa almost dead! Chadema ilikuwa wachukue nchi Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni! hapa ni Kinana ameiokoa CCM!.

Baada ya issue ya uraia wa Azim Premji kuibuka, Kinana alirekebisha uraia wake kwa official declaration kama Bashe na Jenerali Ulimwengu, ila kiukweli kabisa kuna watu kibao tuu ambao sio raia wa Tanzania lakini ni wazalendo kuliko Watanzania wenyewe!, watu kama Joan Wickens, Amiri Jamal, Dr. Leader Starring, Oscar Kambona, Michael Kamaliza, Chinyama Chiume etc, hivyo Kinana ni mzalendo wa kweli kabisa wa Taifa hili!.

Kitendo cha Kinana kutukanwa na yule kichaa ile 2015 na ule ukichaa wa voice notes ulimfedhehesha sana Kinana nami niliuzungumza hapa, Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity humu nilisema

Natumaini wale mnao ijua karma by now you can connect the dots usikute karma ya Kinana imechangia kwenye ile issue na huku kuwa elevated ni karmic consolations kumfidia!.
Nasisitiza Kinana ni mzalendo, and also karma is real, mtu akiwa mzalendo wa type kama ya Comred Kinana, mtu uki doubts uzalendo wake, ukaandika au kumshitumu, watu wakianza kum doubts kutokana na andiko lako, chochote negative kitakacho sababishwa na andiko lako, kitakuwa na karmic consequences
P.
Oscar kambona hakuwa raia wa Tanzania? Kwahiyo songea ni msumbiji?
 
Kinana ni fisadi hilo halina mjadala, ndio maana amerudi tu kwenye system na kelele za kuwahamisha wamasai Loliondo zikaanza, hana maarifa yoyote, hata huko CCM humtumia kwa ajili ya wizi wa kura tu, damu yake ina vimelea vya wizi.
 
Back
Top Bottom