Je, kipara husababishwa na nini na kuna dawa?

Je, kipara husababishwa na nini na kuna dawa?

An elect

Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
89
Reaction score
20
Habari za jumapili?

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, mkiendelea kusukuma gurudumu la maisha. Kama kichwa cha thread kinavyojieleza, leo nataka kushea nanyi juu ya jambo hili; upara/upaa ama head patch kwa kimombo.

Kwa kuangalia haraka haraka nimegundua kuwa hili limekuwa ni tatizo linaloongezeka kwa jamii yetu. Hasa kwa vijana wadogo, wengi wakiwa wa miaka ya ishirini(in their twenties), siku hizi hutokwa sana na vipara.(na kuficha hilo wengi wananyoa nywele zote).

Ninachotaka kujua toka kwenu wakuu ni kuwa je, upara ni ugonjwa / upungufu wa vitu fulani mwilini na je hali hiyo inaweza kurekebishika may be kwa kula vyakula fulani vyenye lishe fulani ama?

Naongea hivi kwa sababu niliwahi kusikia kuwa upara na kitambi ni magonjwa yatokanayo na lishe mbovu yenye upungufu wa virutubisho fulani. Wataalamu twaomba uhalisia wa jambo hili tafadhali.

Ifahamike kuwa hapa sizungumzii upara ambao huwa twachukulia ni hali ya kawaida hasa kwa watu wenye umri mkubwa, ama vya kurithi kama ambavyo husemwa,bali naongelea kwa vijana wadogo kabisa kama nilivyo kwisha eleza. Hata wengine watangulizi wao hawakuwa na vipara.

Karibuni kwa michango ya kitaalamu!

cc; Mzizimkavu,Riwa na wengine...
 
  • Thanks
Reactions: THT
Karibuni wataalamu,hakuna mwenye ujuzi juu ya hili?
 
Google tu mzee. Zipo huko kuanzia sababu za scalp infections, hormonal imbalances(excessive testosterone), the list goes on...
 
Google tu mzee. Zipo huko kuanzia sababu za scalp infections, hormonal imbalances(excessive testosterone), the list goes on...

Nashukuru kwa mchango,nimejaribu kugoogle lakini sijapata dawa ya kitanzania hata moja,na it was just about to share local experience.
Which i can not do with google.
Cant we get something more suiting our local circumstances ...?
Mfano unapo google unakutana na matangazo ya dawa za kihindi na madaktari wa india wakitoa namba uagize products zao. Hatuna wataalamu hao hapa hapa kwetu..?
 
  • Thanks
Reactions: THT
Dah. Unajua mkuu umri unapoenda nywele zinazidi kuwa nyembamba na kudhohofika ambapo huweza kupukutika kadri muda unavyozidi kuyoyoma. That is natural. Na dawa nyingi za kuzuia au kuotesha nywele ni artificial na zinatoka nje ya nchi. Sasa jamii za kiafrika hazichukulii swala la kuota upara mapema kwa uzito, sanasana wataangalia kama babu yako m1 anaupara ndipo waseme amerithi kwa babu yake huyo. Hii inazorotesha hata wataalamu wetu kufanya utafiti wa suala hilo. Bado halijaonekana kama ni tatizo.
 
Ndio mkuu,asante kwa kunielewa.Wataalamu wetu wana mengi ya kuyafanyia kazi.
 
Sababu

Matukio
ya upara wa kiolezo hutofautiana miongoni mwa idadi kubwa ya watu kwa misingi ya maumbile ya jeni, sababu za kimazingira hazionekani kuathiri sana aina hii ya upara.

Utafiti mmoja mkubwa uliofanywa katika Maryborough, Victoria, Australia ulionyesha kuwa kiwango cha ya upotezaji nywele ya mbeleni mwa kichwa-katikati hulingana na ongezeko la umri na huathiri asilimia 73.5% ya wanaume na 57% ya wanawake wenye umri wa miaka 80 na zaidi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Medem Medical Library, upara wa kiume huathiri takribani wanaume milioni 4 nchini Marekani. Takriban asilimia 25 ya wanaume huanza kupata upatara tokea umri wa miaka 20, theluthi mbili huanza kupata upara kuanzia miaka 60. Uwezekano wa kupata jeni ya upara ni 4 kwa 7.

Mkondo wa wanaume hudhihirisha upungufu wa nywele kutoka pande za paji la kichwa unaojulikana kama "upeo wa nywele unaopungua". Upungufu wa upeo wa nywele huonekana katika wanaume waliozidi miaka 20 lakini unaweza kuonekana mapema mwishoni mwa umri wa ujana pia.

Sehemu ndogo ya upara inaweza kujitokeza sehemu ya juu (vertex). Sababu za aina hii ya upara (uitwao androjenetic alopecia) ni DHT, homoni yenye msukumo wa nguvu za ngono , ukuaji wa nywele za mwilini na usoni , ambayo huweza kuathiri vibaya ya tezi kibofu pamioja na nywele za kichwani.

Bado haijafahamika kikamilifu namna DHT hutekeleza jambo hili. Kwenye ngozi za vichwa zinazoathirika na jeni hii, DHT huzua mchakato wa ukondefu wa nywele.

Kupitia mchakato wa ukondefu wa nywele, upana wa mzizi wa nywele huendelea kupungua kitaratibu hadi nywele kwenye ngozi ya kichwa kufanana na manyoya hafifu au "sufi za pichi" au hata kutoweka kabisa.

Mwanzo wa kupoteza nywele wakati mwingine huanza mapema mwishoni mwa kubalehe na hasa husababishwa na jeni . Upara wa mkondo wa kiume huainishwa katika kipimo cha Hamilton Norwood I-VII.

Iliaminika awali kuwa upara ulirithiwa kutoka kwa babu wa ukoo wa mama. Ingawa pana misingi ya imani hii, wazazi wote huchangia uwezekano wa vizalia wao kupoteza nywele.

Pana uwezekano mkubwa zaidi wa kurithi upara iwapo mchanganyiko wa jeni zinazosheheni kwa nguvu kutoka wazazi wote zina hali hiyo ( tazama 'masimulizi jadiya kuhusu upara' chini)

Kuna aina nyingine nyingi za upara:
  • Alopeshia ya mvuto hupatikana kwa kawaida kwa watu wenye nywele ndefu zifungwazo kwa nyuma au mistari ambao huvuta nywele zao kwa nguvu nyingi.
  • Trikotilomania ni upoteaji wa nywele unaosababishwa na uvutaji ua ukunjaji shurutishi wa nywele. Hutokea zaidi kwa watoto kuliko watu wazima. Katika hali hii, nywele hazitoweki kichwani, bali ni hukatika. Nywele zinapokatika karibu na ngozi ya kichwa husababisha nywele fupi zenye umbo la "alama ya vishangao."
  • Kiwewe kama vile chakemotherapia, kujifungua, upasuaji mkubwa, sumu, na mfadhaiko kali kinaweza kusababisha upotevu wa nywele unaojulikana kama effluviamu ya telojeni.Mzizi wa nywele katika awamu ya kukua ni huathirika na kemotherapia wakati matibabu hayo hulenga kutenganisha seli za saratani. Kwa hivyo, karibu asilimia 90% ya nywele hudondoka punde tu baada ya kemotherapia kuanza.
  • Kupoteza nywele kunakotia shaka aghalabu hufuatia baada ya kujifungua pasipo kusababisha athari upara halisi. Katika hali hii, nywele kwa hakika hunawiri wakati wa mimba kutokana na ongezeko la estrojeni mwilini. Baada ya mtoto kuzaliwa, viwango vya estrojeni hushuka hadi viwango vya kawaida kabla-ya-mimba, nayo mizizi ya ziada ya nywele hudondoka. Hali kama hiyo hutokea kwa wanawake wanaotumia dawa ya -kuchochea ushikaji-mimba ya clomiphene.
  • Upungufu wa chuma ni sababu ya kawaida ya ukondefu wa nywele, ingawa upara halisi si kawaida kuonekana.
  • Mnururisho unaoangazwa ngozini mwa kichwa, kama wakati wa rediotherapia, hutumika kwa minajili ya kutibu baadhi ya saratani humo, nao huweza kusababisha upara katika maeneo yaliyoathirika.
  • Baadhi ya maambukizi ya maikoti yanaweza kusababisha upotevu mkubwa wa nywele.
  • Alopeshia areata ni mvurugiko wa mfumo wa kinga-mwili ambao pia hujulikana kama "upara wa doa" ambao unaweza kusababisha kupotea kwa nywele kuanzia eneo moja tu (Alopecia areata monolocularis) hadi kila nywele katika mwili mzima (Alopecia areata univesalis).
  • Upotevu wa nywele wa eneo moja au uliotawanyika huweza pia kutokea katika alopeshia sikatrishia (lupus erithematosu, licheni plano pilari , folliculitis dekalvansi , sentrifugi sikatrishia alopeshia ya kati , alopeshia fibrosi ya mbele baada ya kukoma uzazi, nk). Uvimbe na michipuko ngozini pia husababisha upara wa eneo moja (neva ya sebashia , seli ya msingi ya kasinoma, seli ya juu ya karsinoma).
  • Hipothairoidi inaweza kusababisha kupotea kwa nywele za mbele kwa kawaida, na huhushwa hasa na ukondefu wa thuluthi ya nje ya kope za macho (kaswende pia inaweza kusababisha upotevu wa thuluthi ya nje ya kope za macho)
  • Hipathoiroidi pia inaweza kusababisha kupotea kwa nywele, ambayo kwa njia sawa na siyo tu mbele.
  • Kupoteza nywele kwa muda kunaweza kutokea katika maeneo ambapo uvimbe wa ngozi umekuwepo kwa muda; kikawaida tokea urefu wa wiki moja hadi wiki kadhaa.
  • Alopeshia ya pembe tatu ya muda mrefu- Upotevu wa nywele ulio na umbo la pembe tatu au dura dufu kwa baadhi ya nyakati, katika eneo kandokando mwa kichwa ambayo hutokea hasa kwa watoto wadogo. Eneo lililoathirika hasa huwa na mizizi kondefu ya nywele au mizizi hiyo hutoweka kabisa, lakini halipanuki. Sababu zake hazijulikani na ingawa ni hali ya kudumu, haina madhara mengine yoyote kwa walioathirika.
Nadharia tete za mageuko ya kimaumbile

Hakuna makubaliano kuhusu maelezo ya mageuzi ya mkondo wa upara wa kiume. Madai ya kwamba mkondo wa upara wa kiume(MPB) hunuiwa kuwasilisha ujumbe wa kijamii unaungwa mkono na ukweli kwamba msambao wa vihisivu androjeni kwenye ngozi ya kichwani hutofautiana baina ya wanaume na wanawake.

Aidha waume na wake wazee walio na viwango juu vya androjeni mara nyingi hudhihirisha ukundefu wa nywele uliotawanyika, kinyume na ilivyo katika mkondo wa upara wa kiume.

Haipothesia moja, iliyotolewa na Muscarella na Cunningham, inaeleza kuwa upara ulijitokeza miongoni mwa wanaume kufuatia uteuzi wa jinsia kama ishara pevu ya uzee na ukomavu wa kijamii, ambapo uchokozi na tabia za kujihatarisha huongezeka.

Hii ilitoa taswira ya mwanamume aliyefikia hali iliyoimarika kijamii lakini aliyepungukiwa na uwezo wa kimwili wa kupata washirika wa kujamiiana na kukuza watoto hadi utu uzima.

Katika utafiti wa Muscarella na Cunningham , wanaume na wanawake walitazama wanamitindo 6 wa kiume waliokuwa na viwango tofauti vya nywele usoni (walio na ndevu na masharubu au bila) na nywele kichwani(kichwa kilichojaa nywele, zinazopungua na upara).

Washiriki walitathmini kila mafungu kwa kutumia vivumishi 32 vilvyohusiana na mitazamo ya jamii. Wanaume waliokuwa na upara ama waliokuwa na nywele usoni au nywele zinazopungua walichukuliwa kuwa walio na umri mkubwa zaidi kuliko wale ambao waliokuwa wamenyolewa kabisa au waliokuwa na nywele nyingi kichwani.

Ndevu na kichwa kilochojaa nywele zilionekana kama hali ya ujasiri zaidi na kutokomaa kijamii, nao upara ukahusishwa na ukomavu zaidi kijamii. Hariri ya maoni ya kijamii kuhusu mikondo ya upara wa kiume umetolewa na Henss (2001).

Nadharia tete nyingine za mageuko ya kimaumbile ni pamoja na miunganiko baina ya jeni kwa sifa bainishi zenye manufaa zisizohusiana na nywele wala utofauti wa jeni.

Upara usio wa binadamu

Upara sio tu ni sifa bainishi ya binadamu. Viumbe wengine wa jamii ya nyani , kama vile masokwe, makakiu wenye mikia minene , na uakari wa Merekani ya Kusini hudhihirisha ukondefu taratibu wa nywele kichwani baada ya kubaleghe .

Makakiu wazima-wenye mikia minene, kwa kweli, hutumika mara nyingi maabarani katika kutafiti matibabu yasaidiayo ukuaji wa nywele.
Watangulizi mbalimbali wa taiwa Ulimwengu wa Kale na Ulimwengu Mpya waligeuka kwa kipindi cha wakati na kupata upara kichwani, iliyozuia manyoya kushika vipande vya nyama zilizooza kutoka mlo wa tai , na kusaidia pia kupunguza joto.

Jenetiki

Makala kuu ya: Androgenic alopecia
Utafiti mwingi ulifanywa kuhusu maumbile ya jeni zinazohusiana na mkondo wa upara wa kiume, au (AGA) - androgenetic alopecia . Utafiti unaonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa, uwezekano wa kupatwa na upara wa mapema wa kiume hutokana na jeni za X. Jeni nyingine zisizohusiana na ngono pia hushirikishwa.

Watafiti wa Kijerumani wanataja jeni pokezi ya androjeni kama kiungo muhimu zaidi cha upara. Wanahitimisha kwamba aina fulani ya jeni pokezi ya androjeni huhitajika kwa ukuaji wa AGA.

Mwaka huo huo matokeo ya utafiti huu yalithibitishwa na watafiti wengine. Jeni hii ni dhaifu, kwa hivyo mwanamke huhitaji kromosomu mbili za X zenye kasoro ili kuonyesha alopeshia ya mkondo sawa na wa kiume.

Kwa vile androjeni na mahusiano yake na kipokezi cha androjeni ndiyo sababu za AGA inaonekana jambo la kimantiki kuchukulia kuwa jeni hisivu ya androjeni ina jukumu muhimu katika ukuaji wake.

Utafiti mwingine katika mwaka 2007 ulipendekeza kuwa jeni nyingine katika kromosomu X, iliyo karibu na jeni pokezi ya androjeni, ilikuwa na jukumu muhimu katika mkondo wa upara wa kiume.

Walipata kuwa eneo la Xq11-q 12 katika kromosomu X- lilihusiana pakubwa na AGA katika wanaume. Walisisitiza kuwa EDA2R ndiyo jeni inyohusiana zaidi na AGA. Utafiti huu umeigwa katika angalau tafiti tatu huru zifuatazo.

Jeni nyinginezo zinazohusika na upotevu wa nywele zimegunduliwa. Mojawapo ikiwa jeni ya kromosomu 3. Jeni huwa iko katika 3q26.Jeni hii pia huchangia katika aina ya upara unaohusishwa na ulemavu wa akili. Jeni hii ni dhaifu.

Jeni nyingine ambayo inaweza kushiriki katika upotevu wa nywele ni P2RY5. Jeni hii inahusika na muundo wa nywele. Baadhi zinaweza kusababisha upara wakati wa kuzaliwa ilhali aina nyinginezo husababisha "nywele za sufu".

Utafiti wa hivi karibuni ulithibitisha jeni pokezi X zinazohusiana na androjeni kuwa za muhimu zaidi. Huku jeni katika kromosomu 20 ikiwa ya pili kwa umuhimu wa kuchangia hali hiyo (snpedia)

Upotezaji nywele kwa wanawake

Ingawa upara si kawaida sana katika wanawake kama ilivyo kwa wanaume, athari za kisaikolojia za kupoteza nywele huwa kubwa zaidi. Kwa kawaida ukanda wa nywele za mbele hudumu ilhali uwingi wa nywele hupungua katika maeneo yote kichwani.

Hapo awali iliaminika kuwa ilisababishwa na testosteroni sawa na katika upara wa kiume, lakini wanawake wengi ambao kupoteza nywele huwa na viwango vya kawaida vya testosteroni .

Hata hivyo, upotezaji nywele kwa mwanamke umekuwa tatizo linaloendelea, ambalo kwa mujibu wa Akademia ya Marekani ya Matibabu ya ngozi, huathiri karibu wanawake 30,000,000nchini Marekani.

Ingawa upotezaji nywele kwa wanawake kwa kawaida hutokea baada ya umri wa miaka 50 au hata baadaye, isipoambatana na matukio kama ujauzito, maradhi sugu, ya mlo, na mfadhaiko kati ya nyinginezo, kwa sasa inatokea miaka ya mapema na huku ripoti zikionyesha kuwa hutokea hata wanawake wachanga kama wa miaka 15 au 16.

Sababu za upotevu wa nywele mingoni mwa wanawake zinaweza kutofautiana na zinazoathiri wanaume. Kuhusiana na alopeshia androjeni, upotevu wa nywele za wanawake hutokea kulingana na athari za homoni za androjeni (testosteroni, androsteinedioni, na dihaidrotestosteroni (DHT)).

Homoni hizi za kiume, kwa kawaida hutokea kwa kiasi kidogo kwa wanawake. Hata hivyo, kulingana na Ted Daly, MD, tabibu wa ngozi kutoka Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Long Island, alopeshia androjeni sio sababu kuu ya kupotea kwa nywele kwa wanawake na wataalamu wa ngozi kwa sasa hupendelea kuita hali hii mkondo wa upotevu wa nywele.

Kwa wanawake badala ya kutumia neno androjeni alopeshia. Anaongeza kuwa mkondo wa kike ni wa mtawanyiko na hudhihirika katika eneo lote la juu ya kichwa na waweza kuathiri wanawake wakati wowote.

Wakati mwingine pia mchakato wa homoni huweza kusababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke. Baadhi ya mifano ni: uja uzito, kufikia kutoweza kuzaa, uwepo wa uvimbe wa ovari, dawa za kudhibiti upataji mimba na kiwango juu cha androjeni , dalili za vimbe nyingi za ovari.

Pia matatizo ya tezi , anemia, ugonjwa sugu na baadhi ya dawa husababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke

Dawa utaweza kwenda London kwenye clinic Harley Street Hair Clinic aliyotibiwa Rooney
 
Habari za jumapili?

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, mkiendelea kusukuma gurudumu la maisha. Kama kichwa cha thread kinavyojieleza, leo nataka kushea nanyi juu ya jambo hili; upara/upaa ama head patch kwa kimombo.

Kwa kuangalia haraka haraka nimegundua kuwa hili limekuwa ni tatizo linaloongezeka kwa jamii yetu. Hasa kwa vijana wadogo, wengi wakiwa wa miaka ya ishirini(in their twenties), siku hizi hutokwa sana na vipara.(na kuficha hilo wengi wananyoa nywele zote).

Ninachotaka kujua toka kwenu wakuu ni kuwa je, upara ni ugonjwa / upungufu wa vitu fulani mwilini na je hali hiyo inaweza kurekebishika may be kwa kula vyakula fulani vyenye lishe fulani ama?

Naongea hivi kwa sababu niliwahi kusikia kuwa upara na kitambi ni magonjwa yatokanayo na lishe mbovu yenye upungufu wa virutubisho fulani. Wataalamu twaomba uhalisia wa jambo hili tafadhali.

Ifahamike kuwa hapa sizungumzii upara ambao huwa twachukulia ni hali ya kawaida hasa kwa watu wenye umri mkubwa, ama vya kurithi kama ambavyo husemwa,bali naongelea kwa vijana wadogo kabisa kama nilivyo kwisha eleza. Hata wengine watangulizi wao hawakuwa na vipara.

Karibuni kwa michango ya kitaalamu!

cc; Mzizimkavu,Riwa na wengine...
Upara sababu ya maradhi ya moyo

10151433_10153977350380198_713651326_n.jpg



Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tishio la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani. Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan.

Utafiti huu uliowahusisha watu 37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo. Hata hivyo, watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.

Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume .

Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80 ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya kuwa na upara na maradhi ya moyo.

Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo. Hii ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri, na historia ya familia.

Daktari, Tomohide Yamada, wa chuo kikuu cha Tokyo alisema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi ya moyo."tuliona hili kama jambo muhimu, lakini halina athari kubwa kama mambo mengine yanayosababisha maradhi ya moyo kama vile uvutaji sigara, unene kupita kiasi na mafuta mengi mwilini pamoja na shinikizo la damu.

''Alisema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo. Aidha alisema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.

Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.

Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.
 
Dawa ipo mkuu.Hakikisha unachukua mavi ya jogoo ya asubuhi kabla hajawika,unaloweka kisha unachuja ile juice unakunywa glasi 1 asubuhi na 1 jioni,alafu huyo jogoo unamchinja unakula supu yake,unakula na nyanya chungu.fanya hivyo kisha nipe feedback.Alafu ukinywa juice iwe ni siri yako tu.Mkuu hata kama una upara kama wa mheshimiwa mzee Kingunge baada ya miezi 2 utakuwa na nywele kama za Michael Jackson.
 
Dawa ipo mkuu.Hakikisha unachukua mavi ya jogoo ya asubuhi kabla hajawika,unaloweka kisha unachuja ile juice unakunywa glasi 1 asubuhi na 1 jioni,alafu huyo jogoo unamchinja unakula supu yake,unakula na nyanya chungu.fanya hivyo kisha nipe feedback.Alafu ukinywa juice iwe ni siri yako tu.Mkuu hata kama una upara kama wa mheshimiwa mzee Kingunge baada ya miezi 2 utakuwa na nywele kama za Michael Jackson.

Wooooow...so amazing mkuu!!
Kweli Africa will still be Africa.
Anyways atleast u've contributed and i hope u will lead by example on this.
 
Wooooow...so amazing mkuu!!
Kweli Africa will still be Africa.
Anyways atleast u've contributed and i hope u will lead by example on this.

Hiyo ni dawa ya wa Thailand sio Africa.Mimi nilitumia na upara ukaondoka nina nywele kibao kwa sasa.
 
Dawa ipo mkuu.Hakikisha unachukua mavi ya jogoo ya asubuhi kabla hajawika,unaloweka kisha unachuja ile juice unakunywa glasi 1 asubuhi na 1 jioni,alafu huyo jogoo unamchinja unakula supu yake,unakula na nyanya chungu.fanya hivyo kisha nipe feedback.Alafu ukinywa juice iwe ni siri yako tu.Mkuu hata kama una upara kama wa mheshimiwa mzee Kingunge baada ya miezi 2 utakuwa na nywele kama za Michael Jackson.

Hi dawa haijapata tokea.
 
Wakuu,

Wanaume wengi hua wana vipara vichwani vyao, wengine kwenye utosi, wengine nyuma kidogo juu ya kisogo, wengine kuanzia utosin mpaka juu ya kisogo etc. Na wengine hua hawana kabisa vipara vichwani mwao.

Sijapata kuona mwanamke akiwa na kipara, sasa nauliza chanzo cha kipara ni nini? Hicho chanzo kinahusiana na wanaume tu?

Maswali haya nayauliza kwa hisani ya lukelo sakafu wa JF.
 
Back
Top Bottom