Je, kipi kifanyike kupunguza ukosefu wa ajira nchini?

Kama unataka tufananishe nchi na nchi. Kabla hatujaendelea je unaifamu unemployment rate ya Qatar? Na kama unaifamu je hatuwezi kuwapita hawa?.

Kuna wakati mwingine tunatakiwa tuende mbali zaidi sio kuanza kufananisha hata nchi furani inayo. Twende in deep.

NB. uzi unasema nini kifanyike ili kupunguza tatizo la ajira nchini. Kama huna maoni juu ya hili, nyamaza
 
Ja
Hamna Cha kufanya nakwambia hili tatizo ni duniani kote wewe kwa ufahamu wako unataka kifanyike nini sasa ivi connection za unapewa kutokana na kamba ya urefu wako wewe unazani serikali itafanya nini? Graduate wangapi wako mtaani na wengine tuko nao wanajuta muda waliopoteza wanaingia mtaani wanakuta walioyatarajia hayapo na hayatakuwepo maisha
 
Fanya mpango wa kuyatoa Ma CCM madarakani. Yashaishiwa mbinu
 
Mipango ya muda mrefu, ni kujenga viwanda, weka mazingira mazuri kwa wawekezaji,
Mipango ya muda mfupi, hapa inahitajika diplomasia aggressive kweli kweli,
Kuna MOU Kati ya India na USA, UsA inachukua na kuajili vijana kibao kutoka India, kwenye nyanja za IT, uhandisi, udokta,
Pili mfumo wa elimu,urekebishwe kidogo, kuna vijana kibao, wangeweza kujiajiri kwenye music, tatizo, kuna vikwazo vingi,
Music, IT, kilimo(sio ule upuuzi wa Bashe kupeleka vijana kwenye makambi ya Julia, kama watumwa),
Tunahitaji impact ya kilimo kama ya Ukraine, nchi IPO vitamin kwa miaka miwwili, lakini inatoa msaada, wa tani 500! Kwa sylia
 
Asante kwa mchango wako. Je hizo kazi ambazo zipo serikali inatoa mchango gani ili VIJANA ambao hawana ajira wazipate?
lazima ujue kutofautisha kazi na ajira mkuu, Kazi zipo sana ni wewe tuu unaamua uishije, kama unasubiri ajira utasubiri sana, ila ukiamua kufanya kazi, kazi zipo nyingi shida ni uthubutu na kuchagua
 
Hili sio tatizo la kidunia, na kama lingekuwa tatizo la kidunia basi kusingekuwa na migrant
 
 
lazima ujue kutofautisha kazi na ajira mkuu, Kazi zipo sana ni wewe tuu unaamua uishije, kama unasubiri ajira utasubiri sana, ila ukiamua kufanya kazi, kazi zipo nyingi shida ni uthubutu na kuchagua
Ni kweli mkuu
 
Bro hatumaniishi biashsra ya kuuza mahindi, na ramba ramba za Azam, tunamaanisha biashara ya kukupatia kuanzia milioni 17 kwa mwaka, ili uweze usomeshe watoto hata shule za milioni 2 ,
Wapo vijana kibao wamemaliza ualimu,wapo kitaa, unsfikri hawaoni hizo "fulsa"unazozisema, kuku unafugia wapi? Unalima wapi? Hewani!? Ardhi unapata wapi? Unaenda morogoro kuomba tu, au unarudi kijijini massive, nachingwea, ufuge kuku, harsfu uwasafilishe mpaka Dar, upigwe Bao na traffic, mpaka ufike sokoni,uuze mzigo faster, upate mamilioni yako, ununue bati,cement, ukajenge mjengo bab kubwa madale!
Hz ni story unaleta baada ya kushiba,ukiwa umeshika smartphone, haupo field bro, vijana wa bongo wanapambana Sana, hizo biashara unazozisema, hazina mfumo kwa sababu, zina kero,urasimu mwingi, Bora nikope milioni 7,ninunue bajaji, kuliko kujenga banda la kufuga kuku,
Fika kahama, kalumwa migodini, uone vijana wanavyochapa kazi, degree zimewekwa pembeni, watu wamejaa tope,
 
Tanzania unababaika utafuga nini wapi na umesoma? hivyo vya traffic sijui kutoka nanchingwea na wapi sijui huko, ni story za kujikatisha tamaa gentleman, hakunaga kilimo biashara au biashara ya mahesabu ya kujitisha mwenyewe hivyo,

miaka yote tangu umemaliza chuo miaka 10 iliyopita unazurura tu mjini bila uhakika wa kesho huku unatumia biadhaa na mahitaji ya kila siku hususan vyakula, yanayazalishwa kutoka vijijini hususan kijinini kwenu? Kwanini usifanye maamuzi magumu yenye tija na ukatambua kwamba mjini ni soko kubwa la uhakika la kila kitu kutoka kijijini kwenu?

what is milioni 17 ukifuga nguruwe wako 10 kwa kuanzia, kuku 100 wa kienyeji na ngombe wa saizi ya kati madume hata 10 tu ya kunenepesha, achilia mbali kulima mazao biashara ya chakula kama vile alizeti na ufuta, mahindi, maharagwe, karanga mbaazi au mpunga? au kadiri uwezavyo?

mbona ardhi bwerere tu kijijini kwenu gentleman?
acha kubabaika na ualimua ambao unaweza kuanzisha shule yako kijijini na ukafundisha.

acheni uvivu acheni visingizio dhaifu kabisa hivyo my friends ladies and gentlemen πŸ’
 
Duuuuuh
 
Hiki ni kuzaa zaa
 
Ila mkuu kuna baadhi kwako hawana ardhi.

Ila bado kwa kuazima ardhi inapatikana mtaji hata kuanzia eka moja inatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…