Je, Kipi ni bora na Imara kujenga "Flat roof" au "normal Roof"

Ahsante sana Mkuu, inaonekana una idea na haya mambo. Pls, fafanua zaidi hapo kwenye 0 to 10 inclination kwa kutumia bati. Pia, ulipoandika "bata* ulimanisha bati??
Hahaha replace bata with bati aise mambo ya typing error hayo.
Mi ni Quantity Surveyor by professional ndio maana nna idea ya hizi mambo.
Kuhusiana na nyuzi namaanisha angle yani inayotengenezwa kati ya ile bati na imaginary horizontal line,i hope umenisoma hapo Mhe.
 
Ahsante sana Mkuu, nimekupata vizuri
 
kwa knowledge niliyo nayo mpaka hivi sasa,
Nadhami flat roof sio nzuri kwa mazingira yetu ya Tz, mana maeneo mengi yana mvua nyingi sana per year,
flat roof inafaa maeneo yasio na mvua nyingi.
Nipe mfano hai nikupe solution.Tanzania flat roof haina shida ila kwa zege ina cost kwenye jua kali maana nyakati za usiku zege linatoa heat iliyolunywa mchana so kipengele cha running cost katika feni ai AC kupambana na hiyo hali inakuwa changamoto.
Kuhusu mvua hamna shida kama umetreat vzr top surface ya zege au kama ni flat ya bati basi fanya namna ucollect maji vzr.
 
Yaaa kwa treatment nisawa, ila bado kuna maeneo yana mvua almost mwaka mzima,
Mfano TUKUYU hukooo, mvua nikama niyakila cku yani
 
Mvua nyingi zinaathiri vipi kama zege ni imara?
madhara sio ya cku, au mwez au mwaka,
Madhara yanakuja miaka mingi mbeleni,
Nandomana wengi wanao weka flat roof hua wanaongezea kabati (BATI) kwa mbaaaaali
 
Na mimi nitoe mchango wangu.
Flat roof gharama yake ipo chini sababu ya materials. Lakin pia zipo za aina nyingi kulingana na muonekano ambapo unaweza jikuta unarud kwenye gharama zile zile au hata kuzidi.
Mfano,wapo wanaozungushia kwa tofali na wengine kuacha wazi. Je wewe wapenda ipi?
 
Mara ya kwanza hizo flat roof nilijua huko juu ni full zege.Niliona moja ikijengwa na nikaenda kushuhudia ile iliyokuwa imejengwa.Pale juu wameweka bati ila surface ya mbele na pembeni inakuwa imeinuliwa so ww huwez kuona hilo bati.Yani huko juu..mbao zinalazwa na bati linawekwa ila zinakuw tilted kuweka mteremko kwa ajili ya incase mvua ikija basi maji yachuruzike na kuweza kuyakusanya bila kutuama huko juu.Kwa design hii ya kutumia flat roof ya bati, gharama yake ni ndogo kulinganisha zile za kawaida ...kwani ukitumia flat roof ya design hii utatumia bati chache na mbao chache sana kulinganisha zile za kawaida na unajua jinsi mbao zilivyo ghali..yani kwenye kuezeka mbao ndio zinamaliza pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…