A
Anonymous
Guest
Nimekuwa mtumishi wa Serikali katika Idara ya Afya kwa zaidi ya miaka minne.
Sina imani kubwa na vyama vya wafanyakazi kutokana na uzoefu wangu wa kuona watumishi wengi wakikumbana na changamoto mbalimbali kazini, ikiwemo kusimamishiwa mishahara, bila kupata msaada wa kutosha kutoka kwa vyama vyao.
Pamoja na hali hiyo, kila mwezi watumishi wanaendelea kukatwa fedha moja kwa moja kwenye mishahara yao kwa ajili ya kuchangia vyama hivyo.
Naomba kufahamu, kisheria, je, mtumishi wa Serikali ana haki ya kujitoa katika uanachama wa chama cha wafanyakazi na kusitisha makato ya ada ya uanachama?
Kwa mfano, sisi watumishi wa afya tuna chama cha TUGHE. Je, mtumishi anaweza kuamua kujitoa katika chama hicho na kuacha kuchangia ada ya uanachama kupitia mshahara wake?
Naomba ufafanuzi kutoka kwa wenye uelewa wa sheria za kazi au watumishi ambao wamewahi kupitia hali kama hii.
Asanteni.