Dr Adinan
Member
- Jul 11, 2021
- 14
- 22
Kama una miaka 30+ uko katika hatari ya kupata kisukari. ๐๐ฒ, ๐ธ๐ถ๐๐๐ธ๐ฎ๐ฟ๐ถ ๐ธ๐ถ๐ป๐ฎ๐๐ถ๐ฏ๐ถ๐ธ๐ฎ? ๐ ๐ฝ๐ฎ๐ธ๐ฎ ๐๐ฎ๐๐ฎ ๐ต๐ฎ๐ถ๐ท๐ฎ๐ณ๐ฎ๐ต๐ฎ๐บ๐ถ๐ธ๐ฎ ๐ฑ๐ฎ๐๐ฎ ๐ถ๐ป๐ฎ๐๐ผ ๐๐ถ๐ฏ๐ ๐ธ๐ถ๐๐๐ธ๐ฎ๐ฟ๐ถ
Wengine wakiwa na imani kwamba kila ugonjwa una tiba yake, kwasasa dunia bado haijapata dawa ya kutibu ugonjwa huu mbaya na hatari. Kisukari inaongoza kwa kusababisha ulemavu kwasababu ya kukatwa miguu. Ya pili nyuma ya ajali.
Dawa zilizopo, nyingi zikiwa ziko kwenye majaribio, hupunguza kiwango cha sukari kwenye damu. Hivyo mtu hutakiwa kunywa dawa hizi kulingana na ufanyaji kazi wa dawa anazotumia na muda dawa inapoisha nguvu.
Ndiyo maana utakuta wengine hunywa/ kujichoma mara mbili kwa siku au mara moja.
Kwakuwa lengo ni kushusha sukari na kuwa katika kiwango kinachokubailka kwamba hakina madhara, njia mbalimbali zinatumika kukamilisha lengo hili.
Ikumbukwe kwamba tiba ya kisukari ina malengo matatu:
1. kushusha sukari kwenye damu mpaka kiwango kinachokubalika ki afya;
2. Kudhibiti madhara ya kisukari, na
3. Kukinga madhara ya kisukari.
Tiba ya kisukari kwahiyo nayo imegawanyika katika mafungu hayo matatu.
Yafaa kukumbuka pia, kitabibu, tiba hujumuisha ugunduzi wa tatizo la kiafya, tiba yenyewe/dawa, kisha ufuatiliaji / tathmini ya tiba
1. Tumeshafahamu namna ambavyo mtu huweza kufahamu kama ana kisukari na vipimo vinavyotumika. Glucose (Glucometer), HbA1C.
2. Pia tukasoma vifaa ambavyo mtu huweza kutumia kubaini kama ana madhara ya kisukari au yuko katika hatari ya kupata madhara ya kisukari, mizani ya uzito, kipimo cha hisia miguuni, BMI, kipimo cha presha, vipimo vya moyo na figo, na macho, vinavyofanyika hospitali.
Ya kuzingatia katika tiba ya kisukari ni kwamba tiba hii ni jumuishi: dawa + mabadiliko ya mfumo wa maisha - Mfumo wa maisha nikimaanisha kuacha yale ambayo hukuwekea kwenye hatari zaidi na kufanya yale ambayo yanaboresha afya yako na, + kufanya vipimo muhimu kufuatilia hali yako kwa ukaribu. Mfano kuacha sigara, kuacha kutumia sukari kwa wingi, kufahnya shughuli zinazochangamsha mwili/mazoezi na kupanga mlo wako.
Kuhahikikisha kwamba kila wakati unafanya tathmini ya tiba yako. Je, umeweza kudhibiti sukari? Je, umeweza kudhibiti vihatarishi vyote vya kupata madhara ya kisukari? Je, dawa inafanya kazi kama ilivyokusudiwa?
Hapa namaanisha kupima hali yako na kuhudhuria kliniki kwa tarehe zilie mlizokubaliana na tabibu wako.
Kuhakikisha unatumia dawa kama ulivyoelekezwa na tabibu wako .
Na kuhakikisha uko makini kutambua vihatarishi vyote vya madhara ya kisukari kama vile kucha kubwa miguuni au kutokuvaa viatu vinavyo kubana sana miguu ambavyo vyote vinaweza kusababisha kupata vidonda miguuni.
Umuhimu wa kuweza kujipima ukiwa nyumbani unajitokeza hapa, Kwasababu kikawaida huwa mgonjwa anahudhuria kliniki angalau kila baada ya mwezi. Kwa mtu anayejali afya yake angependa kufahamu hali yake inavyoendelea kabla ya kuenda kliniki.
Rafiki yako,
Dr. Adinan J.