Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 208
- 91
Ni kawaida mtu anapotuma maombi ya kazi atatakiwa kuambatanisha baadhi ya nyaraka, lakini hizi nyaraka zote kwa wakati mmoja ni kwa ajili ya nini?
Mtu anatuma maombi anatakiwa aambatanishe kitambulisho cha taifa, cheti cha kuzaliwa na hapohapo tena barua kutoka serikali za mitaa. Ina maana kitambulisho cha taifa hakitoshi au hakijitoshelezi mpaka tena kuwepo na barua kutoka serikali za mitaa?
Mimi naona hizi barua kutoka serikali za mitaa zibaki kwenye maombi ya kazi ambazo zinahitaji mzaliwa wa eneo fulani (mwenyeji) na isitumike kwenye maombi ya kazi za kitaifa ambazo mtu yeyote anaweza kuajiliwa mahala popote pale.
Hali hii inaleta usumbufu na mlolongo mrefu kwa waombaji wa kazi husika na usumbufu pia kwa waombaji na hata kwa viongozi wa serikali za mitaa.