Je, kitambulisho cha taifa na cheti cha kuzaliwa havitoshi mpaka tena uwe na barua kutoka serikali za mitaa?

Kumbe hata kwenye job application wanataka utamnulisho wa serikali ya mtaa? sasa huku ni kukariri vibaya.Unatambulishwa nini?ni nini kikubwa kati ya NIDA na sahihi ya mzee AMANZI (baba mudi) mwenyekiti wangu wa mtaa?.nilidhani kama huna ID ndiyo utambulishwe na mamlaka za serikali za mtaa
 
Wengine hulipa posho za usafiri au usafiri au nyumba kujua unaishi wapi kwao muhimu
Pia ni njia ya kukujua kuwa unakoishi kuna watu wanakujua wasijeajiri mtu asiyejulikana akaleta shida mbele
Wanaolipa posho za usafari watakudai ticketi za safari.
 
Wanaolipa posho za usafari watakudai ticketi za safari.
Sio kweli kwenda kazini na kurudi wengi ama wanatoa usafiri,au posho flat rate kutegemea unaishi wapi

Inawasaidia kwenye hiyo mipango pia
 
Sio kweli kwenda kazini na kurudi wengi ama wanatoa usafiri,au posho flat rate kutegemea unaishi wapi

Inawasaidia kwenye hiyo mipango pia

Ndiyo waanze kupanga wakati wa recruitment stage kweli? Bwana HR unawamislead wawajili.mtu anaweza akawa amepanga mbagala akipata kazi msakuzi anahamia karibu huko huko.
 
Wewe unahisi hizo barua watu wote wanazichukulia mahali walipozaliwa au kwenye makazi yao ya kudumu? Mtu anachukua barua mahali ambapo tangazo la kazi limemkuta anaishi kwa wakati huo
Hizo barua si lolote. Zinapatikana kirahisi tu.
 
As long as katiba inasema mtanzania anayo haki ya kuishi kufanya kazi mahali popote Tz, hakuna sababu ya kudai vitu vyote hivyo kama mhusika anacho kitambulisho cha Taifa. Naamini taarifa zote zipo kwenye hiki kitambulisho. Tuache kutengeneza mazingira ya kupotezeana muda, muda ni mali.
 
Ila ndugu mleta uzi kwani hujui kuwa watu wanahama. Mfano Ulizaliwa hospitali fulani iliyopo kata A, then ukajiandikisha kata B, sasa hivi unaishi kata C.

Na hapo ni kama hujawahi kuhama mkoa au wilaya uliyozaliwa
 
Deadline 28 mwezi wa saba ndio kwanza january 3 muda gani unapotezwa.
Nida bado haijastabalize bongo bado sana.
Wenzetu marekani ukihama tu kitongoji unaweza badirisha kila kitu. Na ukubwa wao wote, huwezi vuka boda tu kiuwepesi ila rahisi sana kufake utambulisho kwa kutumia naturalization certificate.
 
Ndiyo waanze kupanga wakati wa recruitment stage kweli? Bwana HR unawamislead wawajili.mtu anaweza akawa amepanga mbagala akipata kazi msakuzi anahamia karibu huko huko.
Mtu huwezi ajiriwa bila referees hakuna kitu kana hicho duniani kote

Lazima waweko watu wanaokujua.Jama hutaki kujulikana usiombe ajira endelea tu na mambo mengine achana na ajira iwe binafsi au ya umma .

Ndio maana hata kwenye kuomba kuna referess na baadhi ya watu wanakujua ni wa mahali unapoishi wakitaka taarifa zinginene za ziada waweza fika eneo unaloishi kuhakiki

Pia ukifanya uhalifu iwe rahisi pia kukudaka
 
Verification ya wapi unaishi lazima hutaki usiombe kazi sio.lazima kila mtu aajiriwe kafanye shughuli zingine

Tena sekta binafsi ni balaa.ukiomba kazi unaweza daiwa hadi barua ya mjumbe wa nyumba kumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…