Je, kitu gani kilikufanya ukosane na rafiki yako?

Je, kitu gani kilikufanya ukosane na rafiki yako?

Simbamteme

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
804
Reaction score
2,131
Katika maisha tangu tunakua mpka tunafikia hatua ya utu uzima tunakutana na watu wa aina mbalimbali,miongoni mwao wanakuwa ni marafiki wetu wakubwa sana lakini kutokana na changamoto za hapa na pale tunajikuta tumehitilafiana pakubwa na kila mtu anashika 50 zake.

Mimi nilikuwa na rafiki yangu tuliivana sana..tulikutana mara ya kwanza wakati nasoma O level Kilimanjaro...hapa hatukushibana kivile...tulikuja kushibana baada ya kukutana Chuo..tuliivana sana,likizo zote za 1st year na 2nd year jamaa alikuwa anazimalizia home( mm wazazi washatangulia mbele ya haki) so uhuru ulikuwa mkubwa sana hasa kipindi kile ujana unasumbua kuliko

Baada ya kumaliza chuo tulikaa wote home,hustle za hapa na pale mimi nikasepa mkoani na yeye akasepa mkoa mwingine lkn tulikuwa tunawasiliana sana.Yeye alikuwa anamjua manzi wangu na mm nilikuwa namjua manzi wake...sasa mkoani nilipokuwa si nikapata ka manzi kengine,kalikuwa pisi hatari...katika stori 2,3 si nikamfungukia mwana,nikamtumia na picha whatsapp za bata(ujana tena)...sasa yeye alivyompuuzi, si akazi forward kama zilivyo kwa manzi wangu na caption kibaoo za kumshauri..Manzi wangu akaanza kuniwakia moto mm sijui sababu ni nini,alivyoona yamemshinda akani forwadia zile picha..moja kwa moja nikajua mshkaji wangu ameniua ingawa jamaa alimuomba demu iwe siri kati yao.

Aisee lile jambo liliniuzi sana ukizingatia jamaa alikuwa na videm kibao vya pembeni ambavyo nilikuwa navijua lkn sikuwahi hata siku moja kutamani kumwambia manzi wake

Tulikosana mazima,jamaa aliomba sana msamaha,nilimsamehe lakini nilimfuta kabisa kwenye list ya marafiki zangu mpk leo hatuongei,ingawa tupo kwenye group moja la O level!!

Yule manzi wangu alinipiga chini mazima

Ujana una mambo mengi sana!!
 
Aliniudhi sana.

Tuliishi Geto tukiwa tunasaka ajira miaka ya 2004

Jamaa akapata kazi kabla yangu. Akawa ana hemea baadhi ya huduma kama bili...maji, umeme nk. Sometimes ananisaidia menu..

Atakuwa alinichoka...akaamua kunimwaga...

Ilikuwa hivi aliamua kuhamia sehem nyingin. Mule ndani sikukuta kitu ..nilikuta mabox na nguo zangu. Nakumbuka niliuchapa usingizi kwenye mabox.

Nikamuita dem wangu aangalie nilivofanyiwa. Hadi leo imepita miaka 20 stori niliifunika mwanaharamu apite...tunawasiliana fresh tu
 
Nilikosana nae pindi alipojiunga na hawa viumbe.

20240319_163514.jpg


KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mnafiki mmoja hivi, nimemfuta kabisa katika maisha yangu. Mshkaji wa karibu lakini kila mtu nnayekosana naye yeye ndo anakuwa rafiki yake! Akiona/kusikia mafanikio yangu anaumia mno, anajaribu kuonesha kuwa siyo juhudi zangu, kuna mtu nyuma ya hayo mafanikio! Rafiki mwenye chuki na wivu kaa naye mbali.
 
Back
Top Bottom