HOJA Je, kiwanda cha Maranile Group Ltd cha Misugusugu kipo juu ya sheria au kuna watu wamepigwa milungula? Hakikustahili kujengwa kilipo

HOJA Je, kiwanda cha Maranile Group Ltd cha Misugusugu kipo juu ya sheria au kuna watu wamepigwa milungula? Hakikustahili kujengwa kilipo

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Kwa Viongozi na Mamlaka Husika,

Ujumbe huu ninauandika kwa masikitiko makubwa na kwa niaba ya jamii ya waathirika wa eneo la Misugusugu, Kibaha, ukiwa na lengo la kuomba msaada wa haraka kutoka kwa mamlaka husika ili kuokoa maisha, afya, na mustakabali wa jamii na watoto wetu.

Kabla ya ujio wa kiwanda hiki cha pombe cha Maranile Group Ltd, mazingira ya eneo hili yalikuwa safi na salama sana ambapo wananchi walikuwa wakiishi kwa amani, na shughuli zao bila usumbufu au matatizo yoyote. Lakini tangu kiwanda hiki kianze kufanya kazi ya kutengeneza pombe kwa kutumia kali, maisha ya jamii hii yamegeuka kuwa mateso makubwa yanayotokana na uchafuzi wa hali ya juu.

Kiwanda hiki hakikustahili kabisa, kwa namna yoyote ile, kujengwa katikati ya makazi ya watu. Kinaathiri wananchi mchana na usiku kutokana na harufu kali sana ya pombe na kemikali inayosambaa mtaa mzima hadi barabarani wakati wa kuchemsha molasi na kupunguza presha ya mitambo yao.

Harufu hii ni kero kubwa inayozuia watu kupumua vizuri, na hata nyakati za usiku wananchi wanashindwa kabisa kupata hewa safi wakiwa ndani ya nyumba zao. Hali hii inatengeneza swali kubwa kwa mamlaka: Kwanini mnaendelea kuruhusu uwepo wa kiwanda hicho katika eneo hili ilhali athari zake ziko wazi na zinaonekana kila siku?

Ushahidi wa kiwango cha juu kabisa cha athari hizi ni ukweli kwamba kuna Shule ya Sekondari ya Kata iliyokuwa jirani ambayo sasa inahamishwa kwa sababu wanafunzi hawawezi kabisa kusoma kutokana na harufu hii kali ya pombe.

Badala ya mamlaka kukiondoa kiwanda kinachochafua mazingira, mnaacha watoto wetu wakimbie shule yao waliyokuwa wakitafuta elimu. Ikiwa taasisi kubwa kama shule inakimbia uharibifu huu, wananchi wa kawaida na watoto wao waliopo majumbani Misugusugu watakimbilia wapi?

Mbali na hewa chafu, kiwanda hiki hakina mfumo wowote wa kueleweka wa kudhibiti maji yake machafu ya uzalishaji. Wanachofanya ni kufungulia maji meusi hasa mvua inaponyesha, yenye harufu mbaya na sumu kali, na kuyaacha yatiririke kuelekea kwenye mashamba na vyanzo vya maji.

Maji hayo yakipita yanakausha kila kitu, kiasi kwamba mpunga na bustani za mboga za wananchi zote zinakufa. Uwekezaji mkubwa wa mabwawa ya samaki umeharibiwa kwa kuuliwa kwa samaki wote kama kambale na perege, na mifugo kama ng'ombe inakufa baada ya kunywa maji hayo. Hali ni hatari zaidi kwa sababu baadhi ya wananchi wanategemea vyanzo hivi kwa ajili ya kunywa na matumizi ya nyumbani.

Uongozi wa kiwanda hiki umekuwa ukifanya ujanja wa makusudi ili kukwepa uwajibikaji na sheria za nchi. Walipoona kelele za wananchi zimezidi, walificha lile bomba lao la wazi na kuweka mabomba ya chini kwa chini wakayapeleka mbele zaidi kwenye manyasi ili isijulikane maji yanatoka wapi. Isitoshe, hivi sasa wanasubiri nyakati za mvua kubwa ili wafungulie yale maji yao machafu kwa wingi yakachanganyike na maji ya mvua kuelekea kwenye mashamba na mabwawa, wakiamini kuwa jambo hilo halitagundulika.

Inafahamika kuwa huko nyuma mamlaka za NEMC na DAWASA zilifanya ukaguzi, wakajionea uharibifu huu na kukifunga kiwanda hiki pamoja na kukipiga faini, ambapo walitakiwa wasifanye kazi mpaka wajenge bwawa rasmi la kudhibiti maji hayo. Lakini cha kusikitisha bado uzalishaji unaendelea kwa kificho na ujanja ujanja, kwani bado kuna siku harufu ileile inasikika na bado wanafungulia maji hayo kwa siri bila kuheshimu mamlaka.

Msisitizo wa jumuiya yetu ni mmoja tu na haubadiliki: Kiwanda hiki hakitakiwi kuwepo kwenye eneo la makazi ya watu. Hakuna maboresho yoyote ya ndani yatakayomaliza kero hii ya hewa na maji yenye sumu. Viwanda vya namna hii vinatakiwa vikawa mbali sana na jamii.

Tunaomba mamlaka mchukue hatua za mwisho na za kudumu za kukihamisha kiwanda cha Maranile Group Ltd kutoka hapa Misugusugu ili kulinda uhai, afya, na haki ya watoto wetu kupata elimu katika mazingira salama. Tunaamini sauti hii ya kilio cha jamii itasikiwa na hatua zitachukuliwa mara moja.​
 
Imeeleweka lakini kwa wananchi kuna shida pia kielimu.

Maeneo mengi ya viwanda mamlaka za ardhi imedesignate kabisa “INDUSTRIAL AREA” mtu akiona kiwanda kinaanza kujengwa anaenda kujenga nyumba yake mpakani / karibu na kiwanda akiamini ardhi itapanda thamani zaidi kwa sababu ya mradi.

Kama umejenga baada ya eneo hili kusajiliwa kisheria kuwa ni la viwanda basi usilalamike kuhusu kelele/harufu/moshi etc kwa sababu ukifuata mwenyewe na document zipo wazi.

Kama eneo la kiwanda lilisajiliwa baada ya kusajiliwa kwa eneo la makazi pembezoni mwake basi hapo shida ipo kwa kiwanda.

Tathmini lazima iangalie pande zote
 
Aisee hiki kiwanda ni shida, leo nimetembelea ndugu, na harufu ya chemicals sio ya kitoto, naona bwawa la kemikali ndio liko nyuma ya ukuta.
Sio pia, na nyumba ni ya muda sanaa kabla kiwanda
Screenshot_20261103-102927.jpg
 
Back
Top Bottom