Financial freedom
Financial education
Financial literacy
Sijapata kiswahili fasaha cha hayo maneno hapo juu, ila elimu ya fedha ama ya kudhibiti uchumi binafsi ama wa familia inatakiwa ifundishwe nyumbani, mtoto aifahamu na kuielewa hiyo elimu pamoja na kanuni za fedha tqngu akiwa mdogo akue anaifahamu hivyo na wakumuelekeza na kumpa hiyo elimu/ huo ujuzi na udhibiti wa fedha ni wazazi ama walezi waliomlea.
Ukitegemea kupata hii elimu ukiwa shule ama chuo pia utafanikiwa ila hautakuwa nguli kama aliyekuwa na hiyo hulka tangu anatambua pesa haitoki hadi iingie na inayotoka inatakiwa iwe ndogo kuliko inayoingia ama laah ikitoka kubwa kuna matarajio itaingia kubwa zaidi kuliko iliyotoka na mduara unaendelea.
Tafakari mtoto anakua anafundishwa kusema uongo na walezi/wazazi wake ili kusavaivu maisha ama kuwa mjanja mjanja kukwepa kulipa vitu, kuwa mbabe, kuwa mdhulumishi.... what if mtoto huyohuyo angelelewa kila uchao anaona na anaambiwa kiwa na nidhamu ya fedha/kudhibiti uchumi.... akifika miaka 20 sio mwenzako.
Alamsiki.