Je, Kiwango chako cha fedha kikubwa cha kusave kwa mwezi ni kipi na nini kinakukwamisha usisave?

Je, Kiwango chako cha fedha kikubwa cha kusave kwa mwezi ni kipi na nini kinakukwamisha usisave?

Financial freedom
Financial education
Financial literacy

Sijapata kiswahili fasaha cha hayo maneno hapo juu, ila elimu ya fedha ama ya kudhibiti uchumi binafsi ama wa familia inatakiwa ifundishwe nyumbani, mtoto aifahamu na kuielewa hiyo elimu pamoja na kanuni za fedha tqngu akiwa mdogo akue anaifahamu hivyo na wakumuelekeza na kumpa hiyo elimu/ huo ujuzi na udhibiti wa fedha ni wazazi ama walezi waliomlea.

Ukitegemea kupata hii elimu ukiwa shule ama chuo pia utafanikiwa ila hautakuwa nguli kama aliyekuwa na hiyo hulka tangu anatambua pesa haitoki hadi iingie na inayotoka inatakiwa iwe ndogo kuliko inayoingia ama laah ikitoka kubwa kuna matarajio itaingia kubwa zaidi kuliko iliyotoka na mduara unaendelea.

Tafakari mtoto anakua anafundishwa kusema uongo na walezi/wazazi wake ili kusavaivu maisha ama kuwa mjanja mjanja kukwepa kulipa vitu, kuwa mbabe, kuwa mdhulumishi.... what if mtoto huyohuyo angelelewa kila uchao anaona na anaambiwa kiwa na nidhamu ya fedha/kudhibiti uchumi.... akifika miaka 20 sio mwenzako
Ujumbe mzuri sana kupitia hii thread tutajua level ya financial literacy ya watu wengi
 
Habari wana JF

Natumaini tuna vipato tofauti tofauti humu ndani embu leo tupeane utaalamu kidogo wewe unaweza kusave kiasi gani kwa mwezi na ni asilimia ngapi ya kipato chako kwa mwezi hiyo ela unayosave na Je kama huwezi kusave kabisa ni nini kinakukwamisha.?

Binafsi kwa mwezi nimejiwekea kusave angalau Laki tatu(3) ambapo hadi sasa nina kama 2M za savings ambazo nnategemea kufungulia miradi huko mbele zikijaajaa.

Vipi wewe unayeweza kusave umefikia kiwango gani na lengo ni kiwango gani na unategemea kufanyia nini hyo pesa ukifikia hilo lengo?

Tujuzane hapa chini.👇👇👇
Pesewa 20
 
Unasave wapi na kipato chako ni kiasi gani kwa mwezi mzee

1.5M salary kabla ya makato, ila kazi yangu ni flexible muda mwingi nakuwa field inapelekea maslahi kuongezeka nje ya salary. From there naweka nidhamu ya matumizi ya pesa.
 
1.5M salary kabla ya makato, ila kazi yangu ni flexible muda mwingi nakuwa field inapelekea maslahi kuongezeka nje ya salary. From there naweka nidhamu ya matumizi ya pesa.
Safiii vzuri natumaini kwa salary hyo unaeza kusave si chini ya 400k..
 
Back
Top Bottom