kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Taifa linalia na ufisadi, Wapo watu wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi wa mali za umma. Kuna watu waliochukua fedha za umma na kwenda kulewea na kuzitoroshea ng'ambo zisijulikane, lakini wako watu waliochukua fedha za umma bila idhini na wakaziwekeza nchini kwa kujenga mahoteli, viwanda, mashule, na kulima mashamba makubwa na kutoa ajira kwa watanzania wengi na kulipa kodi mbalimbali serikalini. Je, watu hawa 2 kiuchumi na kisheria wametenda makosa yaliyo sawa? wanahitaji adhabu sawa?