Je? Kuku wa malawi yaani black australorp ni vipi?

malamsha shao

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
215
Reaction score
79
Wengine wanasema hawa kuku ni wa kisasa ila wengine wakienyeji na vp sokoni wanatambulika kama wakienyej au kisasa na vp bei yake dar.Naomba mchango wenu wana Jf
 
Mheshimiwa Malamsha, nikiwa nimezuzuka na ufugaji wa kuku wa kienyeji, niliwakuta hao Kuku wa Malawi wakiuzwa Nane Nane; rangi yao na umbile lao na ukubwa wao ulinipendezesha sana machoni, walidai ni kuku wa kienyeji wa Malawi! Nilinunua Jogoo Tsh 20,000 ulikuwa mwaka 2008, kwa vile uwezo wa kununua na jike sikuwa nao! Walisema majike wanataga mayai sana. Baada ya kuwafuga watoto waliozaliwa ni dhahiri walikuwa chotara, nilibaini kuwa ni kweli kuku hao ni watagaji wazuri sana wa mayai! Ila hawana sifa kabisa za kuku wa kienyeji! Pamoja na kuwa hawa kuku walikuwa ni chotara wa Malawi na kikwetu hawakuwa wanaatamia. Pia walikuwa dhaifu, mara nyingi vifo vya kuku vilivyokuwa vikitokea walikuwa hao weusi wa Malawi! Kana kwamba hitoshi ilibainika kuwa kukitokea uwepo wa viroboto ilishangaza kuona kuwa kuku wa Malawi walikuwa kivutio kikubwa cha kushambuliwa sana na viroboto ukilinganisha na kuku wa kienyeji wengine! Ninamaanisha kuwa kuku hawa walikuwa wanashambuliwa kupindukia kuliko wa kikwetu!

Baada ya kufuatilia nilibaini kuwa kuku hawa maarufu kama kuku wa Malawi ni Australorp, hawa kuku si kuku wa kienyeji kama tunavyoijua maana ya kuku wa kienyeji! Kuku wa Malawi wanasifa zote za kuku wahamiaji, yaani kuku wakigeni. Inawezekana kunamazingira ambayo kuku hawa wamekuwa wakifugwa kienyeji na wanastawi vizuri na imechukuliwa kuwa nao ni kuku wa kienyeji, si kweli!

Sina uhakika huko sokoni wanawachukuliaje, lakini ni rahisi sana kukubalika kama kuku wa kienyeji kwa muonekano wao! Na hapa ndipo tunapopigwa bao kuuziwa kwa bei kubwa, kuku lenyewe limejaa manyoya tu utadhani ni mkubwa kumbe wa kawaida tu! Nilipokuja kubaini si kuku wa kienyeji niliwauza wote nikasafisha banda! Nikaendelea na vishingo wangu! Hakuna sababu upoteze pesa labda kama unataka wa kupamba kama maua nyumbani kwako! Kwa kweli wakizaana kwa wingi hupendeza sana lakini ni presha tupu! JF hatufichani ukweli ndiyo maana naipenda JF, naomba na wengine mnaowajua ongezeeni hapa. Pengine yalinikuta peke yangu nami sijafanya utafiti kwa wengine.
 
Asante sana Kubota umenipa elimu kwani ningekuja pata hasara itabidi ninunue wachache na sio wengi kama nilivyopanga.
 
Mkuu si kwamba ulikuta walio closiwa? na kama ndo kweli absi nilikuwa sijui kwamba hawa kuku ni pure kisasa ila ni propaganda tu zinafanyika kwamba ni wa Kienyeji
 
Kaka nilikuta wamemwagwa kibao majike kwa madume, mijogoo ilikuwa mizinga kweli kweli sijapata ona na majike pia, weusi tii bila mabaka na wanapendeza sana! Si wastahimilivu wa magonjwa na wadudu kama hawa wa kienyeji na pia walikuwa hawaatamii mayai na hizo ni sifa kubwa za kuku wa kigeni. Na pia wanataga mayai sana na wanaanza mapema.
 
wastani wa utagaji wake ukoje kwa msimu mmoja wa kutaga? Na je mayai ya hawa kuku yana kiini cha njano kama ilivyo kwa hawa kuku wetu asilia? naomba majibu kwa mwenye uzoefu wa hawa kuku wa malawi.
 
kuna mtu nilimtembelea kweli yanapendeza na mayai yake ni kama ya kienyeji na kiini cha njano hata kuku wa kisasa wakipewa majani yaani gree stuff mayai yanakuwa na kiini cha njano
 
Kaka nilikuta wamemwagwa kibao majike kwa madume, mijogoo ilikuwa mizinga kweli kweli sijapata ona na majike pia, weusi tii bila mabaka na wanapendeza sana! Si wastahimilivu wa magonjwa na wadudu kama hawa wa kienyeji na pia walikuwa hawaatamii mayai na hizo ni sifa kubwa za kuku wa kigeni. Na pia wanataga mayai sana na wanaanza mapema.

ahhh!kumbe!nilinunua vifaranga mia moja mahali na aliyeniuzia akaniambia ni wa kienyeji,nilishangaa kukuta vifaranga vyote mia ni vyeusi kabisa kabisa,kwa sasa wana miezi sita na wamebaki hata ishirini hawafiki,na ni wepesi sana ila wakubwa kwa umbo la nje,niliwafuga pamoja na broilers kwa mtindo wa kienyeji yaani heri broilers nimekula ila si hawa,wananiumiza kichwa sana mpaka hamu ya kufuga imenitoka,nawaangalia tu.
 
pole sana hawa kuku mie nilinunua kama 15 kupitia mitiki blog wakiwa miezi 5 kwakweli alikuwa wazi kuwa ni chotara na hawana tabia ya kuatamia labda nitumie incubator. Niseme kweli hawana tatizo lolote kwangu na wanataga almost daily at a rate of 8/10. Hawana magonjwa niliyiowahi kuwatibu ingawa nilipewa wakiwa wakubwa na kila miezi mitatu ninawapa chanjo ya newcastle. Hawa nimewachanganya na cornish brown wamekrosiwa na kuchi wote nawalisha kawaida tu pia nawapa majani, mayai yao ni madogo na yana kiini (kumbuka kuna majogoo pia). Kifupi mimi naona ni kuku bora ukilinganisha na wa kienyeji wanavyokua taratibu na maumbo madogo na wa kisasa wanavyohitaji chakula ghali, madawa na vitamini. Bahati mbaya ni kuwa mliaminishwa ni wa kienyeji ila ukijua wazi kuwa ni cross breeding ungefaidika na ukuaji wao haraka huku wakiwa hawahitaji utanzaji wa hali ya juu kama wa kisasa.
 
sasa bei yake iknje?
 
sasa bei yake iknje?

bei inategemea idadi, mahali na msimu. Mimi nawafuga dar, tetea wanauzwa elfu kumi jogoo elfu kumi na tano kama sio sikukuu. Wanaotaka kuchinjiwa kuletewa home au office tunaongeza elfu moja. kuna wanaonunua wengi mnaelewana ila kumi na kumi na tano ndo bei ya kuku wakubwa kwa maeneo mengi. Mayai tray elfu kumi.
 
Mama Joe tray la mayai Sh elfu 10 !? Hawa kuku kweli ni mkombozi! Hii bei imenisisimua sana!
 
Ni kweli ujue tu kutafuta soko. Sikuizi watu hawapendi mayai au kuku wa kisasa wanaogopa madawa na vitamini . Wenye Watoto. Wajawazito wananunua sana haya mayai. Pia kuna wafugaji wa kienyeji na wanaouza vifaranga wanabahatisha ya kutotolesha hivyo soko lipo.
 
pole sana hawa kuku mie nilinunua kama 15 kupitia mitiki blog wakiwa miezi 5 kwakweli alikuwa wazi kuwa ni chotara na hawana tabia ya kuatamia labda nitumie incubator. Niseme kweli hawana tatizo lolote kwangu na wanataga almost daily at a rate of 8/10. Hawana magonjwa niliyiowahi kuwatibu ingawa nilipewa wakiwa wakubwa na kila miezi mitatu ninawapa chanjo ya newcastle. Hawa nimewachanganya na cornish brown wamekrosiwa na kuchi wote nawalisha kawaida tu pia nawapa majani, mayai yao ni madogo na yana kiini (kumbuka kuna majogoo pia). Kifupi mimi naona ni kuku bora ukilinganisha na wa kienyeji wanavyokua taratibu na maumbo madogo na wa kisasa wanavyohitaji chakula ghali, madawa na vitamini. Bahati mbaya ni kuwa mliaminishwa ni wa kienyeji ila ukijua wazi kuwa ni cross breeding ungefaidika na ukuaji wao haraka huku wakiwa hawahitaji utanzaji wa hali ya juu kama wa kisasa.

asante sana Mama Joe,angalau umenipa ari mpya ya kuendelea kuwahudumia hawa waliobaki,kwa sasa wanatetea ila ni wepesi sana au nakosea wapi?wewe unapowauza wanakuwa na uzito wa kuridhisha?naomba ujuzi wako tafadhali,asante sana ndugu.
 
Kusema kweli mimi nimefuata maelezo ya chakula chao kwa RETI kuna uzi ameelezea vifaranga wa kienyeji utafaidika sana. Nimewauza hao weusi kwakweli walikaribia kg 2 believe me. Unachotakiwa kama unataka watage walishe layers mash. Kama unataka wauzwe tu kama wa nyama endelea kuwalisha kama wa miezi 3-4 ambao wanaendelea kukua. Kwenye maduka ya vyakula kuna mfuko inaitwa concentrates ni elfu ishirini unachanganya kwenye pumba gunia moja. Kuna ya layers na ya wa nyama hivyo unachagua kama unataka kuku wako uwauze vipi. Nakushauri walishe watage wakichoka wanenepeshe uuze. Kama unawatoa nje jaribu kuwatibia minyoo. Ukiweza tengeneza chakula mwenyewe kuna formula umu jf. Pia wape mabaki ya nyumbani be flexible. Msome Kichwa mbovu, Reti na Gazeti. ALL THE BEST
 
Ma Joe za siku mpendwa!
Ni kweli hawa kuku ni wazito vizuri tu kama unatunza vizuri, zaidi hawa wekundu.
 
Nzuri mpendwa
Yaani hawa kuku unakuwa huna pressure kabisa hao wekundu /cornish wanakuwa hadi basi mie nikaogopa maana nimeona wakubwa hawatagi lakini wameanza kutaga wote sasa hivi, nasubiri batch yangu tu ya pili
 
Back
Top Bottom