Je, kulikuwa na ulazima gani Tanzania kuchukua wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wimbo wa Taifa? Kwanini tusingetunga wa kwetu?

The vice versa is true. Ni SA ndio walikopi toka TZ.
 
Upo mwingine pia wa kizalendo, sikumbuki 'title' yake.

AHAAAA: Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote---

Watunzi wa nyimbo hizi wanastahili tuzo na heshima ndani ya nchi yetu.

Anayejuwa watunzi na historia ya nyimbo hizi, tafadhali simulia.
Pia kuna mwingine tulikuwa tunaimba shule ya msingi, huu ni wa kuisifia zaidi unaimbwa hivi;

"Tanzania Tanzania, nchi yenye mali nyingi... Watu wengi wa ulayaaaa wanaililia sana, niliona ndege wengi...chini wametia fora...walinipendeza mlio kama mtoto wa nyumbani...Ngooorongoro ile ngoorongoro ile ngoorongoro ileee ngoorongoro ileee.."

Sijui ndo hivi
 
Uzalendo namba moja unaanza kwa kuwa na wimbo wa taifa uliotungwa na sisi wenyewe, sio wimbo mtumba
 
Tazama ramani ni bonge la wimbo! Na una sifa zote za kuwa wimbo wa Taifa la Tanganyika! Sema tu unatakiwa pia kufanyiwa maboresho kwenye mashairi yake! Kusiwepo mstari wowote ule wa kutaja majina ya viongozi! Sijui Nyerere, sijui Karume!!

Tena kama huyo Karume ndiyo hatakiwi kabisa kutajwa! Maana tayari Zanzibar wana wimbo wao wa Taifa.

Kiukweli hui wimbo wa sasa hauna mvuto! Eti Mungu ibariki Afrika! For what!! Wimbo wa Taifa uiongelee Tanzania tu na watu wake.
 
Kwani TANZANIA na South Afrika, ipi Hasa ilianza kupata Uhuru???

Tuanzie hapo .
 
Well said brother
 
Bro, South Africa imepata uhuru mwaka 1994 kutoka kwa kaburu. Sisi Tanganyika tumepata uhuru 1961 na muungano 1964. Sasa sijui hapo unahitaji taarifa gani zaidi kujua nani kamuiga nani?!
 
Kuna watu mnaweweseka sana na kipande kinachosema "Mungu ibariki Afrika kwa sababu ya ufinyu wa elimu ya kiroho. Kimaandiko unapowaombea wengine kwanza halafu wewe ukajiombea mwisho kwa Mungu wewe ndio unabarikiwa zaidi. Wengi hawafanikiwi kwa kuweka ubinafsi mbele halafu wengine baadae.

"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa". Yakobo 5:16
 
Bro, South Africa imepata uhuru mwaka 1994 kutoka kwa kaburu. Sisi Tanganyika tumepata uhuru 1961 na muungano 1964. Sasa sijui hapo unahitaji taarifa gani zaidi kujua nani kamuiga nani?!
Bro,
Maneno katika wimbo huo yalitungwa na mtunzi Enoch Sentonga huyu ni Raia wa Afrika Kusini.

Wimbo huo aliutunga mwaka 1897 ukiwa na maneno "Nkosi sikelel i'Afrika wenye tafsiri yake "Mungu Ibariki Afrika katika lugha ya Kiswahili.

Wimbo huo ni wimbo maarufu Afrika ukitumiwa katika harakati za ukombozi kwa baadhi ya nchi za Afrika. Sontonga alizaliwa 1873 na alifari tarehe 18-04-1915 huko nchini Afrika kusini.
 
Hakika
Tazama ramani mrefu kinoma, ni kheri tuache hivyo hivyo maana hizo kamati sijui wanakway wa kutunga, kuhariri na kupata wimbo wa taifa watakula pesa zaidi ya pesa ya sensa. Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume waambie waache tu hasara ni kubwa kuliko faida.
 
Unaendeshwa na roho za mapepo wachafu wewe. Kwa hiyo tuutumie wimbo mtumba, huoni huo ni umasikini kabisa wa fikra?
 
Alishiriki nani kutoka Tanzania kuutunga wimbo huo?
Tulishiriki Idea ya wimbo wao wakatunga mashairi na kuimba.

Uhuru wa S.Afrika tumehusika pakubwa.

By the way waasisi Nia Yao Hasa wimbo Ule uje kuwa wimbo wa Africa nzima maana tulidhamiria kuanzisha Dola moja ya Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…