Je, kumjadili Ruge na JD bungeni kama jana, si kuingilia uhuru wa Mahakama?

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Posts
1,334
Reaction score
989
Wakati bunge likiendelea kujadili bajeti ya Wizara ya habari, vijana, jana jioni wabunge wawili Ester Bulaya na Vicky Kamata walichangia mzozo kati ya Lady JD na Ruge.

Wote wametoa maoni umalizwe nje ya mahakama.

Maana yake nini? Maana yake yule aliyetumia uhuru usioingiliwa kikatiba wa kufungua kesi, aliona amefanya uamuzi sahihi.

Anayajua yote hayo ya kufamaliza nje ya mahakama. Lakini akili yake imechagua uamuzi wa mahakamani kwa sababu ambazo sisi hatuwezi kumpangia.


Sasa, tunapotoa maoni tena public kwamba aangalie uamuzi mwingine. Binafsi nilidhani ilikuwa ni sahihi kama angekuwa yuko katika hatua ya kutafakari options nyingi za suluhu.

Kwamba kama katika options hizo za mawazo, tungekuwa na haki ya kusema, Bwana, tumia option fulani achana na option ya mahakamani.

Sasa, mwenzetu ambaye hatuwezi kumfundisha options zinazomfurahisha, kaamua kwenda mahakamani. Sasa, baadhi yetu, tunasema option aliyochagua aachane nayo, achukue tunayoitaka.


Tuliona hansard, ilivyotumika kama ushahidi kwenye kesi ya Prof. Costa Mahalu. Hansard ya jana inaonyesha majadiliano na mapendekezo hayo kwa suala la JD na Ruge.

Je, mle bungeni, hili si jambo ambalo linajadiliwa mahakamani na haliruhusiwi kama yalivyowahi kugomewa mengi mle bungeni kwa sababu yana kesi Mahakamani?

Huu ndiyo wasiwasi wangu.

SAIDIA KUONDOA WASIWASI HUO
 
Ingekua siasa ndo mabunyenye wa ccm wangekimbia kusema ni kuingilia uhuru wa mahakama
 
ukisikia kitu kinakataliwa kujadiliwa bungeni kwamba kiko mahakamani basi ujue kimewakalia magamba vibaya,
 
Ingekua siasa ndo mabunyenye wa ccm wangekimbia kusema ni kuingilia uhuru wa mahakama

Nadhani usikwepe hoja bunge letu limepoteza mwelekeo baadaye watataka waende mahakamani na mbaya zaidi washiriki kama mahakimu, pia tumeona wanavyongilia majukumu ya utendaji na kuacha kazi yao ya msingi. kama kesi iko mahakamani wao inawahusu nini? nini haswa lady JD na Ruge kwa wabunge na watanzania mpaka kuacha kuchambua budget na kuendeleza mipasho hiyo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…