Je, kumuacha mtu umpendaye ni rahisi?

mj909

Member
Joined
Aug 1, 2024
Posts
86
Reaction score
204
Je, kumuacha mtu umpendae ni kitu rahisi? Na je kama ni rahisi ninjia gani hutumika kuondoa maumivu ya moyo?

Kama umeshawahi kupitia maumivu naomba uniambie ulivukaje (kiufupi kuna kiumbe anautesa moyo wangu) halafu kila nikipiga hesubu naona kama ananileta mapicha picha nazidi kuumia.

Sasa nataka nimuache na nimsahau Kabisa ila kila nikijaribu moyo unazidi kuuma.
 
Kumsahau mwanamke / mwanaume ni vigumu mno endapo mlipendana au ukimpenda kwa Sana kutoka moyoni.

kikubwa ni kumwomba mola mlezi apate kukutoa machungu na huzuni katika nafsi yako hakika yote yanawezekana kwa maana mapenzi ni fumbo kubwa kwetu wanadamu. Mungu mtukufu akusaidie.
 
Only time can heal broken hearts
 
Hakuna njia ya mkato. Kufa hutakufa ila kwa hakika cha moto utakiona!

➑️➑️➑️ Jipe muda. Hizo nati zinazokaza kwenye moyo zitaanza kuachia. Muda si muda maumivu yatapungua, utapata ahueni na hatimaye utaanza kumuona wa kawaida tu; na hata kuanza kujishangaa why it took you so long!

Muda ndiyo tiba sahihi ya yote!
 
Amen
 
Kumuacha mtu unayempenda maumivu yake hayaelezeki,hata kama una mademu miamoja.

Ukiona mpenzi wako mnaachana na haufeel chochote unaona ni kawaida ,hujapenda bado.

Niliwahi kupenda kiasi cha kuhurumiwa na majirani,huku wakiniambia mbona sina kasoro yeyote naliaje kisa mwanamke?

Kutokana na kaushawishi nilikonako pale mtaani wakina mama wakaingia chaka na kuibuka na pisi kali,
Elewa neno pisikali,
Wanaume wenzangu mwanamke anajua kuchagua mwanamke mwenzie ni shida.

Mtoto huyu walitaka aje kureplace nafasi ya mke wangu kipenzi na demu alikuwa tayari,binti msomi mwenye umbo zuri na sura ya kikaskazini lakini wapiiiiiiii.aliniongezea machungu tu licha ya kukutana naye kimwili lakini akili iko kwa......

Wapo majirani walikuwa tayari kunipa hata bure lakini wapiiiiii

Mapenzi yanauma wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…