Je, kumuacha mtu umpendaye ni rahisi?

Je, kumuacha mtu umpendaye ni rahisi?

Je kumuacha mtu umpendae ni kitu rahisi? Na je kama ni rahisi ninjia gani hutumika kuondoa maumivu ya moyo?

Kama umeshawahi kupitia maumivu naomba uniambie ulivukaje (kiufupi kuna kiumbe anautesa moyo wangu) halafu kila nikipiga hesubu naona kama ananileta mapicha picha nazidi kuumia.

Sasa nataka nimuache na nimsahau Kabisa ila kila nikijaribu moyo unazidi kuuma.
Muda ni mwalim mzuri sana wa tatizo lako
 
Kumuacha mtu unayempenda maumivu yake hayaelezeki,hata kama una mademu miamoja.

Ukiona mpenzi wako mnaachana na haufeel chochote unaona ni kawaida ,hujapenda bado.

Niliwahi kupenda kiasi cha kuhurumiwa na majirani,huku wakiniambia mbona sina kasoro yeyote naliaje kisa mwanamke?

Kutokana na kaushawishi nilikonako pale mtaani wakina mama wakaingia chaka na kuibuka na pisi kali,
Elewa neno pisikali,
Wanaume wenzangu mwanamke anajua kuchagua mwanamke mwenzie ni shida.

Mtoto huyu walitaka aje kureplace nafasi ya mke wangu kipenzi na demu alikuwa tayari,binti msomi mwenye umbo zuri na sura ya kikaskazini lakini wapiiiiiiii.aliniongezea machungu tu licha ya kukutana naye kimwili lakini akili iko kwa......

Wapo majirani walikuwa tayari kunipa hata bure lakini wapiiiiii

Mapenzi yanauma wakuu
Maumivu yako yaliishaje nipe mbinu
 
Hakuna njia ya mkato. Kufa hutakufa ila kwa hakika cha moto utakiona!

[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Jipe muda. Hizo nati zinazokaza kwenye moyo zitaanza kuachia. Muda si muda maumivu yatapungua, utapata ahueni na hatimaye utaanza kumuona wa kawaida tu; na hata kuanza kujishangaa why it took you so long!

Muda ndiyo tiba sahihi ya yote!
Swadaktaaaaa!!!
 
Pole sana mkuu, punguza kupenda mtu deeply, kuna muda unaweza kuangalia zile picha mlizopiga pamoja na kujiuliza hiv ni huyu kweli anaeniletea mapicha au unakua huamini, akina komasava sio wajingaa.
 
Hii imenikumbusha nilivyompenda Sekela siku nikatikisa kiberiti eti tuachane mwenzangu akaniacha kweli akaniblock kila sehemu nilikuwa naamka usiku wa manane naenda kwenye uwanja wa wazi naita kwa sauti Sekela ,Sekela huku nalia .

Hapo ni baada ya kushauriwa na gujamaa gumoja gulijiita mwanasaikolojia lakini njia yake haikufua dafu nikawa nasikiliza nyimbo za kuumiza Ila sikumsahau na bahati mbaya akakwea pipa kwenda huko ,kiukweli alinitesa sana yule dada ,nikawa namtishia dada yangu nitajiua asipomtafuta Sekela amlete kuniona 😭😭

Tulikuja kuonana baada ya miaka minne amebadilika kawa Kama mmama alafu mda huo nishajua kwenda bar nikawa namuona Kama kituko kila akijivuta napiga alafu no simu ya salamu Wala kumjulia hali mwisho akajitoa mwenyewe .
 
kuna tofauti kumuacha mtu umpendaye na kuachana na mtu mnayependana.
Nazungumzia kuachana na mtu nimpendae maana Mimi najua moyo wangu unampenda sana ila yeye moyowake siwezi kuuzungumzia kwasababu mtu anaweza aka kuaminisha kwamba anakupenda lakini moyoni mwake hakupendi
 
Pole sana mkuu, punguza kupenda mtu deeply, kuna muda unaweza kuangalia zile picha mlizopiga pamoja na kujiuliza hiv ni huyu kweli anaeniletea mapicha au unakua huamini, akina komasava sio wajingaa.
Nawezaje kuugawa upendo? Nipe mbinu za kumpenda mtu kiasi
 
Hii imenikumbusha nilivyompenda Sekela siku nikatikisa kiberiti eti tuachane mwenzangu akaniacha kweli akaniblock kila sehemu nilikuwa naamka usiku wa manane naenda kwenye uwanja wa wazi naita kwa sauti Sekela ,Sekela huku nalia .

Hapo ni baada ya kushauriwa na gujamaa gumoja gulijiita mwanasaikolojia lakini njia yake haikufua dafu nikawa nasikiliza nyimbo za kuumiza Ila sikumsahau na bahati mbaya akakwea pipa kwenda huko ,kiukweli alinitesa sana yule dada ,nikawa namtishia dada yangu nitajiua asipomtafuta Sekela amlete kuniona 😭😭

Tulikuja kuonana baada ya miaka minne amebadilika kawa Kama mmama alafu mda huo nishajua kwenda bar nikawa namuona Kama kituko kila akijivuta napiga alafu no simu ya salamu Wala kumjulia hali mwisho akajitoa mwenyewe .
😂
 
kabisa,,ila nmeajiachilia kwa msamaha wangu mi mwenyewe
Msamaha wako mwenyewe kivip?

Ujue kwel sikukuona lkn sikujua kama lupango,yan hapa nilisikia harufu ya perfume yako nikajua mchuchu wangu yuko hapa ndo nikakuita
 
Msamaha wako mwenyewe kivip?

Ujue kwel sikukuona lkn sikujua kama lupango,yan hapa nilisikia harufu ya perfume yako nikajua mchuchu wangu yuko hapa ndo nikakuita
uyo jamaa inabid ajisamehe tu ,,aondoke na upendo wake,,nipo mbon nilikoment juu kabsa
 
Back
Top Bottom