Je, kuna aliyewahi kupona chronic gastritis & GERD (ACID reflux)? Naomba msaada

Je, kuna aliyewahi kupona chronic gastritis & GERD (ACID reflux)? Naomba msaada

Joined
Nov 10, 2025
Posts
9
Reaction score
6
Habari zenu wana jukwaa. Mimi ni kijana wa kiume nina changamoto ya maradhi (chronic gastritis & acid reflux) mwenye ufafanuzi naomba anisaidie

BACKGROUND
Nimekua nikisumbuliwa sana na tumbo ever since nipo mdogo sana. Tumbo limekua ni kitu kinachonisumbua na kuniumiza sana kana kwamba likianza hua napata joto, mwili unakua dhaifu, mikono naona hai function hata kufanya chochote siwezi mostly kazi zinazo involve kujikunja kunja inakua inataka nijilaze tu sehemu yenye upepo mkali ndiyo kupata kwangu ahueni au ikitokea nimeenda toilet kwa haja kubwa, kupumua (kujamba) au kubeua angalau kidogo linapunguza maumivu but not guaranteed

Pia mimi sio kama watu wanaoumwa ulcers wakila wanakaa sawa mimi nikila bado tumbo litauma after while. Na tumbo linaniuma chini ya kitovu sio juu ya kitu wala maeneo ya karibu na diaphragm kama watu wengi wa ulcers wanapoumia. Na tumbo langu liko too sensitive kana kwamba kuna muda hata nikiumwa kitu kingine naogopa kunywa dawa nahisi zitavuruga tumbo lilichokoze nianze hangaika na tumbo instead of kutibu huo ugonjwa

Nimekua katika hiyo hali ila nilichokua nakosea ni kwenda kwenye hospitali na kuonana na ma Dr wa kawaida ambao sio specialist wa tumbo. Majibu waliokua wananipa ni una bacteria/wadudu wengi sana kwenye choo chako, tumbo lako lina gas mno (niliwahi fanya ultra sounds) etc. Lakini nikipewa dawa hali inarudi nakuta sijatibu hiyo ndiyo ilikua kosa langu

Miaka 6-7 nyuma nilianza pata symptom nyingine sio frequently ila inatokeaga nakua naharisha, kutapika na choo hua ni njano inayotaka fanania khaki na maji maji tu hutoka, naona kikawa kinaniletea na migraine headache (kichwa cha upande upande)

Mnamo 2024 nilifanikiwa kwenda Muhimbili kukutana na specialist wa tumbo na kufanya kipimo cha kumeza ambacho hua precisely ku determine changamoto za tumbo. Majibu waliyonipa ni kwamba;
  1. Walikuta kuta za tumbo langu lina michubuko kidoogo. Wakadai ni very minor case
  2. Wakasema koo linalopeleka msosi tumboni halifungi vizuri (GERD). Hivyo hupelekea shida ya acid reflux
Niliwashangaa sana sababu sikutegemea kukutana na majibu ya hivi. Mimi tumbo ni kitu kinachonitesa lifetime yangu yote na hata hivyo dawa walizonipa ni Mebeverin ila still tatizo liliendelea ku persist. Kitu kikubwa walichokisema ni kwamba hali ikiendelea na kuzidi urudi ufanyiwe kipimo kingine cha kupitisha torch via haja kubwa kinafika tumboni kwa ajili ya uchunguzi zaidi. (Kiukweli sikufanikiwa fanya hivyo sababu ya financial constraints)

Dawa nazotumiaga sometimes kupata relief ni Omeprazole na Pantoprazole ila kuna muda hali inazidi zinakua hazitulizi. Sipendi kujizoesha sana madawa hivyo natafuta mtu anaejua dawa ya mitishamba ya uhakika niweze kulitibu hili tatizo.

Nimeshajaribu unga wa mlonge nilifuatilia thread humu watu waliuongelea ila sikupata matokeo makubwa hivyo kikubwa ilikua ilinisaidia kwenda chooni (may be ku smoothen choo sababu kuna time nilikua napata choo kigumu), kutoa gas kidogo, kebua ila still nikifanya shughuli za kutumia energy (especially mazoezi yani bado nitalichochea tu). Nina tendency ya kunywa maji ya moto & uvugu vugu kila niamkapo asubuhi, jioni nikishatoka kukimbia, kutafuna tangawizi mbichi na asali niliwahi kutumia kulamba

Najua inabidi nizingatie lifestyle kwanza kwenye ulaji (kutokushiba kwa mkupuo kula ado ado, kuepuka baadhi ya misosi, kula na kutulia 2 - 3 hrs before kulala etc. Lakini hapo kwenye msosi ni ngumu sana navyoona kwa sababu misosi mingi inanileta shida na ndiyo vyakula vyetu waTz. Nimejaribu dawa baadhi za mitishamba lakini matokeo sikuyapata makubwa na nilivyotarajia hivyo msaada mwenye ushuhuda na dawa yeyote ya asili nitashukuru akiweza nisaidia kunitajia, kunipa hints.

Plus; niliponunua unga wa mlonge aliyeniuzia alisema usiponisaidia nirudi anipe mafuta ya msufi. Anaejua pia hii aliyewahi kujaribu anaweza nielekeza matokeo. Ahsanteni kwa muda wenu mliosoma, kutoa maelekezo 🙏🏿
 
Pole. Kuna thread humu ktu alisema kuwa alitibiwa CCBRT. Itafute hiyo thread . Au nenda CCBRT ujaribu. Usikate tamaa!
 
Mm nilipona kabisa, but nilitumia dawa moja ya tiba lishe / herbs, kwa dawa hizi za hospital zinatuliza tu tatizo au zinatibu tu maumivu shida inaendelea kuwepo
 
Pole mkuu kwa hiyo shida,najua unga wa ubuyu( ule mweupe ambao haujatiwa makorokoro) unasaidia wenye vidonda vya tumbo labda unaweza kujaribu, unachanganya na maji kidogo unakunywa kila siku, kila siku bila kuacha.
Pia kwa shida hiyo, nadhani matibabu zaidi ni lifestyle hasa misosi maana sio mdudu kwamba utakunywa dawa umuue, ni sehemu ya mwili kwenye hiyo misuli ya kufunga tumbo imelegea. Kupata dawa ya kufanya sehemu ya mwili iliyolegea irudi kawaida si mchezo.
Kingine usiache kunywa Omeprazole au hizo pantoprazole kwa hofu ya kujizoeza dawa, kukaa na maumivu ndo unajiumiza zaidi na unaweza kuzalisha tatizo jingine kubwa eg uvimbe au kuvuja damu ambalo kulitibu itakuwa gharama kubwa sanaa. Ukijisikia maumivu, wewe meza Omeprazole, tumbo lisiumie zaidi. Hayo mambo ya " kujizoeza dawa" ni maneno tu ya watu.
Mwisho kuwa makini na matapeli maana hadi kwenye dawa za asili siku hizi matapeli wapo.
 
Pole mkuu kwa hiyo shida,najua unga wa ubuyu( ule mweupe ambao haujatiwa makorokoro) unasaidia wenye vidonda vya tumbo labda unaweza kujaribu, unachanganya na maji kidogo unakunywa kila siku, kila siku bila kuacha.
Pia kwa shida hiyo, nadhani matibabu zaidi ni lifestyle hasa misosi maana sio mdudu kwamba utakunywa dawa umuue, ni sehemu ya mwili kwenye hiyo misuli ya kufunga tumbo imelegea. Kupata dawa ya kufanya sehemu ya mwili iliyolegea irudi kawaida si mchezo.
Kingine usiache kunywa Omeprazole au hizo pantoprazole kwa hofu ya kujizoeza dawa, kukaa na maumivu ndo unajiumiza zaidi na unaweza kuzalisha tatizo jingine kubwa eg uvimbe au kuvuja damu ambalo kulitibu itakuwa gharama kubwa sanaa. Ukijisikia maumivu, wewe meza Omeprazole, tumbo lisiumie zaidi. Hayo mambo ya " kujizoeza dawa" ni maneno tu ya watu.
Mwisho kuwa makini na matapeli maana hadi kwenye dawa za asili siku hizi matapeli wapo.
okay sawa nashukuru sana BOSS
 
Ndio, karibu naweza kukuekeza pa kuipata
Sasa kama ni dawa na Kuna sehemu inapatikana Kwa Nini usandike hapa watu wengi wakajua jinsi ya kuipata?
Maana hospitali sio Siri.
Ukielekeza inakopatikana ni faida kwa muuzaaji au hospitali na mgojwa.
Maana hospital zipo kwa ajili ya kutoa huduma na kupata faida,na mgonjwa shida yake apone
 
mkuu unaendeleaje? vii umeshapata tiba?

fweshi tu BOSS


kuna dawa ya asili nilitumia nililetewa kutoka DOM ilikua ime blend-wa unga wa mlonge na vitu vingine somehow ilikua inafanya nipate pate choo kimtindo. Ila tumbo kuuma still lilikua lina persist sometimes. Na hiyo dawa kwa sasa imeniishia ila in a meantime natumia tiba yangu ya siku zote kunywa maji ya uvugu uvugu & maji ya moto pamoja na kutafuna tangawizi mbichi. Ila tumbo likizidi sana nameza tu vidonge vyangu Omeprazole & pantoprazole. Besides unga wa mlonge wenyewe nimewahi kuutumia hapo awali matokeo yake hayakupishana sana na hii niliyotoka kumaliza juzi iliyokua blended na ingredients zingine. Ila hii ya mara ya mwisho ilikua inaleta improvements zaidi ya unga wa mlonge wenyewe
 
Back
Top Bottom