Je kuna benki inaweza kumkopesha mwalimu fedha nyingi kama 60m hadi 80m

Je kuna benki inaweza kumkopesha mwalimu fedha nyingi kama 60m hadi 80m

Vipi kuhusu kukopa tena kabla ya kumaliza deni?
Yeah inawezekana kama mkopo wako ukifika miezi 6 unaweza ukafanya top up deni, namaanisha kuwa unapata tena kile kiasi ulichokopa kama ulichukua million 10, baada ya miez sita unaweza kopa tena million kumi
 
Kwa kuanzia, hakuna benki inayokopesha waalimu. Ila benki karibu zote hukopesha watumishi wa serikali wakiwemo waalimu. Kiasi cha mkopo kinategemea na mshahara wa mtu. Kuna waalimu walioko H wana kipato kizuri tu na wanaweza kukopa mpa milioni thelathini. Akimaliza anakopa tena na tena mwisho wa siku atakuwa amekopa zaidi ya hizo milioni sitini.
Lakini benki pia hukopesha watu kwa ajili ya miradi ya kibiashara. Kama mchanganuo wako utaonyesha unahitaji mtaji wa milioni sitini na ukaainisha utakavyokuwa unapata faida na kurejesha mkopo, benki itakukopesha hata milioni mia moja, ili mradi ukidhi masharti yao.
Tatizo jamii ya kitanzania inadharau sana waalimu. Mimi sioni tofauti ya mwalimu na afisa utumishi kwa misingi ya mshahara.
Mkuu,hakuna benki Tanzania hii inayoweza kukukopesha hata milioni kumi tu eti kwa ajili ya kuanzisha biashara hata kama una mchanganuo ulioandikwa na malaika.Utakopeshwa tu katika biashara iliyohai na inayoonesha kukua ukiwa na hati ya nyumba yako unayomiliki
Bank gani nzuri kwa kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali tujilipue
 
Yeah inawezekana kama mkopo wako ukifika miezi 6 unaweza ukafanya top up deni, namaanisha kuwa unapata tena kile kiasi ulichokopa kama ulichukua million 10, baada ya miez sita unaweza kopa tena million kumi
Mkuu,haiwezekani ukope milioni 10,halafu baada ya miezi sita uruhusiwe kukopa tena milioni 10,unless ulikuwa mkopo wa mwaka mmoja,ambapo kwa miezi sita hiyo utakuwa umeshalipa zaidi ya milioni 5.5.Nadhani ni watumishi wachache wa serikali wanaolipwa mshahara wa zaidi ya milioni 3 ili kuweza kuhimili makato ya zaidi ya laki 9 kwa mwezi.
 
Sasa Ticha mpendwa, ukope milioni 80 ukiweka na riba hapo ya 21% si utakatwa hadi siku unastaafu? Manake hesabu za fasta fasta utarudisha almost 3 times ya uliyokopa!

Bank wanaruhusu mkopo wa miaka 30 ikiwa ni mortgage tu ili wabakie na hati. Usiwe na tamaa. Jijenge taratibu tu utafika.
 
Ahsanteni kwa ushauri, mchango na mawazo yenu, nimefikia uamuzi wa kuacha kazi nifanye biashara zangu
 
Back
Top Bottom