Je, kuna binadamu yeyote anaweza kuishi eneo lenye viumbe hawa?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Binafsi kuna wadudu au wanyama ambao siwapendi na siwezi hata wagusa hata ukinambia wamekufa.

Nimewaza chukulia mfano unatakiwa kuishi kwenye sehemu ambayo ni makazi ya kudumu ya viumbe hawa:

1. Nyoka
2. Tandu
3. Nge

Can you sleep in that area? Mi nakumbuka miaka fulani nlikuwa chuo nikawa nimepanga nyumba flani mtaani, ile nyumba ilikuwa na shida kuu mbili.
1. Tandu
2. Nge

Hawa walikuwa ni kama wamefugwa around the house. Nlikuwa nafululiza kuwaona karibia week tatu, funga kazi siku hiyo nmetoka chuo nmevua viatu nataka nivae sandals namwona kijana/ binti wa nyoka kakaa chini ya sandals na carpet.

Nikajua tu hapo wazazi wake watakuwa around. Na wasije wakawa wananiangalia wakaona nambughudhi mtoto wao. Nilitoka taratibu sikurudi tena, kesho yake nilituma watu waniondolee vitu vyangu nikarudi tu home. Kile chumba nilirudisha baada ya miezi sita kwisha ila nilikaa muda usiozidi mwezi mmoja.

Ilikuwa "Inshu" (issue) mara unamwona N'ge unamuua mara unakuja muona tandu, basi ukiua kesho tena au kesho kutwa ukinyanyua ndoo unamwona mwingine ame-chill chini ya ndoo. Ukisogeza kabati unamkuta tandu yaani ilikuwa shida, unalala kwa mashaka sana hata shuka likikugusa unatuka haraka kuwahi kuwasha taa. Hapo unatoka na net yote ukifika kule ukutani unaitoa net kwanza mwilini then unakagua kitanda kwa kitumia fimbo ya mfagio.

Ukiona shwari basi unafanya utaratibu wa kufunga net ili ulale upya. Hapo utakesha kutafuta usingizi. Nikaona shida yote ya nini, nikarudi home.

Nyoka nawachukia, nyoka nawachukia kinyama. Hadithi za ana sumu au hana I don't care. Nyoka siwapendi; tandu na ng'e I hate them too. Kama yupo ndani any of them na sijafanikiwa kumuua sitolala humo ndani.
 
Pamoja na yote hayo hujaongelea kunguni, aisee huwezi kulala kabisa. Nyoka kunguni, sitamani hata kuwaona.
 
Mtu huyo ni mu asia peke yake maana atapata kitoweo
 
Hakuna kitu kinanifurahisha kama kuua nyoka.Nikiwa natembea njiani halafu nimeshika fimbo huwa naomba sana nikutane na nyoka nimpe kichapo.

Kanuni yangu ni moja, nikikutana nyoka halafu akaanza kunikimbia huyo ni halali yangu lakini akinikazia macho na kuanza kunifukuza hapo natoka mbio zaidi ya H.Bolt.

Kuna braza anaitwa kunguni huyu namheshimu sana, mziki wake sio wa nchi hii sema tu hapendi 'shoo ofu'
Nge na tandu wachumba tu.
 
Niliwahi kwenda sehem tandu ni wengi mbaya zaidi mpaka vitandani asubh nikaaga kurudi kwetu nawaogopa sana tandu niko kama wewe yan nimuone tandu sikai kwa amani mpaka auliwe na maiti yake niione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…