Je, kuna Dawa au Mafunzo ya kumsaidia mtu kutoshikwa haja ndogo mara kwa mara hasa awapo Safarini au Mkutanoni?

Je, kuna Dawa au Mafunzo ya kumsaidia mtu kutoshikwa haja ndogo mara kwa mara hasa awapo Safarini au Mkutanoni?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kikubwa hapa nataka kujua hasa Kitaalamu je, kuna ama Dawa yoyote ile ya Hospitalini au ya Kiutamaduni (Mitishamba) au Mafunzo yoyote yale Mtu anaweza Kutumia au Kuyatumia ili ayatumie na yaweze Kumsaidia asiwe anashikwa na Mkojo mara kwa mara hasa awapo Safarini au akiwa Mkutanoni na kila mara kutaka au kuomba kwenda Kujisaidia Haja Ndogo / Kukojoa?

Na Kiafya au Kibaiolojia nini husababisha Watu wengine Kutoshikwa kabisa na Mkojo (Haja Ndogo) wawapo Safarini au Vikaoni kwa muda mrefu? Hawa Miili yao huwa ina Kitu gani cha ziada kinachowazidi hawa Wengine ambao hukumbwa mara kwa mara na Haja Ndogo (Mkojo) wawapo ama Safarini au Mikutanoni?

Na naomba pia kujua (hasa kutoka kwa Wanajeshi) je, hawa huwa wanatumia nini kwani sijawahi kuona Wanajeshi ama wakiwa katika Magwaride yao au hafla zao za Kijeshi au hata Safarini wakiwa wanaomba kwenda Kukojoa (Kuchimba Dawa) kama Abiria wengine.

Nitashukuru leo nikipata Elimu Kubwa juu ya hilo nililouliza au haya ya Msingi na Muhimu niliyoyauliza nikiwa na uhakika yanaweza pia Kusaidia wengi wenye Kukumbwa sana na Changamoto hii.

Nawasilisha.
 
Ndio dawa zipo, Katibiwe UTi Sugu.
Amoxclav 625mg ni dozi ya siku 7 utameza 1×2.
Hakikisha unakula sawa sawa na unywe maji mengi mara kwa mara.
 
Tuelimishe hapa zaidi Mkuu.
What is a diuretic? Diuretics ― also known as water pills ― are medicines that help you move extra fluid and salt out of your body. They make you pee more frequently, which is why you should take them in the morning if you can. You may need to take diuretics once or twice a day at the same time each day. - nimeikopi Cleveland Clinic

What foods have a diuretic effect?
Zumpano recommends adding these diuretic foods into your diet:
Lemons.
Celery.
Garlic.
Onions.
Bell peppers.
Watermelon.
Cucumbers.
Ginger.

Hivyo yawezekana huyo myu anatumia vyakula hv usiku.

-nimeikopi Cleveland Clinic
 
Yupo Mheshimiwa mmoja aliwahi tokwa mkojo, hii pia inasababishwa na diabetes ni kama inaua mishipa.

Pia ukijijua hivyo angalia na unywaji wako wa viminika.

But anyways, ngoja doctors waseme.
 
Tabia ya kubana mkojo muda mrefu ilinisababishia UTI.. Usijaribu

Ila kama unataka kupata mkojo kiasi, binafsi huwa nakunywa maji ya kawaida siku moja kabla ya safari. Ila siku yenyewe huwa sinywi kabisa maana nikinywa hata nusu lita lazma isumbue

Kingine niliambiwa umri unavyozidi kwenda, mishipa nayo hulegea hivyo uwezo wa kubana mkojo unapungua.. Sijui madaktari watasemaje
 
Usinywe maji,au juisi au vyakula vyenyye msjimaji kama tikiti maji sometimes hata matango.

Kula vitu vikavu kama korosho kidoogo,biskuti,kuku aliyekaangwa n.k then unashushia na maji kidoogo ili chakula kiende tumboni.

Ukila vyakula vyenye maji mengi maana ýake unaongeza maji mwilini,na mwili kikawaida hujiondolea maji yanayozidi kupitia kukojoa mkojo.
 
What is a diuretic? Diuretics ― also known as water pills ― are medicines that help you move extra fluid and salt out of your body. They make you pee more frequently, which is why you should take them in the morning if you can. You may need to take diuretics once or twice a day at the same time each day. - nimeikopi Cleveland Clinic

What foods have a diuretic effect?
Zumpano recommends adding these diuretic foods into your diet:
Lemons.
Celery.
Garlic.
Onions.
Bell peppers.
Watermelon.
Cucumbers.
Ginger.

Hivyo yawezekana huyo myu anatumia vyakula hv usiku.

-nimeikopi Cleveland Clinic
GENTAMYCINE

Hivyo mwenye tatizo atatakiwa atumie Antidiuretics

Antidiuretic
Kundi la dawa
A hormone that helps blood vessels constrict and helps the kidneys control the amount of water and salt in the body. This helps control blood pressure and the amount of urine that is made. Antidiuretic hormone is made by a part of the brain called the hypothalamus and is secreted into the blood by the pituitary gland.

Nimekopi kutoka Cancer.gov
 
Dokta mbona kama vile unakuwa Mkali? Wagonjwa tutapona Kweli?
Sikia GENTAMYCINE
Mwanaume unaweza kuhold maxmum 750mls za mkojo, ukiona unakojoa mkojo hauishi mwingi unabaki ndani hii ndo shida ila kukojoa mara kwa mara inaeza kutokana tu na unywaji wako wa maji, size ya kibofu kua ndogo au misuli iliyotanuka.
Tatizo ni pale utakapogundulika hali yako inasababishwa na maambukizi kwenye kibofu au Uvimbe au Tezi dume inayokisukuma kibofu (kubwa zaidi ya 30mls)

Mimi kwa Taaluma na uzoefu wangu kafanye vipimo vya maabara na Ultrasound unaweza kua diagnosed kua na Cystitis au Prostatomegaly(BPH) utapata tiba mapema na hata kama ukikutwa uko Normal utashauliwa namna gani ya kuhandle hiyo Changamoto yako.

Angalizo: Sijakufanyia Diagnosis nimekupa uzoefu ambao hua nakutana nao kwa watu wenye changamoto kama yako unaweza usiwe mmoja wao.
 
Back
Top Bottom