Je, kuna Dawa au Mafunzo ya kumsaidia mtu kutoshikwa haja ndogo mara kwa mara hasa awapo Safarini au Mkutanoni?

Je, kuna Dawa au Mafunzo ya kumsaidia mtu kutoshikwa haja ndogo mara kwa mara hasa awapo Safarini au Mkutanoni?

Yupo Mheshimiwa mmoja aliwahi tokwa mkojo, hii pia inasababishwa na diabetes ni kama inaua mishipa.

Pia ukijijua hivyo angalia na unywaji wako wa viminika.

But anyways, ngoja doctors waseme.
Nakubalina nawe kama kuna Bingwa wa Kunywa Vimiminika (Soda / Juice) duniani basi naweza kuwa katika 10 bora.
 
Sikia GENTAMYCINE
Mwanaume unaweza kuhold maxmum 750mls za mkojo, ukiona unakojoa mkojo hauishi mwingi unabaki ndani hii ndo shida ila kukojoa mara kwa mara inaeza kutokana tu na unywaji wako wa maji, size ya kibofu kua ndogo au misuli iliyotanuka.
Tatizo ni pale utakapogundulika hali yako inasababishwa na maambukizi kwenye kibofu au Uvimbe au Tezi dume inayokisukuma kibofu (kubwa zaidi ya 30mls)

Mimi kwa Taaluma na uzoefu wangu kafanye vipimo vya maabara na Ultrasound unaweza kua diagnosed kua na Cystitis au Prostatomegaly(BPH) utapata tiba mapema na hata kama ukikutwa uko Normal utashauliwa namna gani ya kuhandle hiyo Changamoto yako.

Angalizo: Sijakufanyia Diagnosis nimekupa uzoefu ambao hua nakutana nao kwa watu wenye changamoto kama yako unaweza usiwe mmoja wao.
Kwahiyo katika hii sijui Cystitis au Prostatomelogy ina maana hapa Dokta itabidi azipime na Pumbu / Kende zangu au?
 
Tabia ya kubana mkojo muda mrefu ilinisababishia UTI.. Usijaribu

Ila kama unataka kupata mkojo kiasi, binafsi huwa nakunywa maji ya kawaida siku moja kabla ya safari. Ila siku yenyewe huwa sinywi kabisa maana nikinywa hata nusu lita lazma isumbue

Kingine niliambiwa umri unavyozidi kwenda, mishipa nayo hulegea hivyo uwezo wa kubana mkojo unapungua.. Sijui madaktari watasemaje
Naomba niige hii yako ya Kunywa tu Maji ya kawaida Siku moja kabla ya Safari na Siku ya Safari kutokunywa kabisa.
 
Usinywe maji,au juisi au vyakula vyenyye msjimaji kama tikiti maji sometimes hata matango.

Kula vitu vikavu kama korosho kidoogo,biskuti,kuku aliyekaangwa n.k then unashushia na maji kidoogo ili chakula kiende tumboni.

Ukila vyakula vyenye maji mengi maana ýake unaongeza maji mwilini,na mwili kikawaida hujiondolea maji yanayozidi kupitia kukojoa mkojo.
Mkuu Shikamoo hapo ulipo na Saluti kwani kwa 75% ni kama vile umeshanipa Tiba Tukuka ninayoianza kuanzia hii Leo.
 
Mimi Nina changamoto Hiyo, Madaktari wamenambia ni Bora wewe unapokunywa Maji na baada ya muda si mrefu unaenda kukojoa, means unaondoa Sumu Kwa haraka Mwilini.

Wakanambia Kukaa masaa 6 ama 10 bila kukojoa sio Sifa, wakanambia usihofu.

So mm ninachofanya, nimezoea kunywa Maji kila siku asubuhi, nikiwa nasafiri sinywi Maji asubuhi, ila ntakunywa Maji kidogo pale wakati wa Chakula, pia kama Safari tunapata nasafi kwenda Haja Ndogo, tukirudi ndo nakunywa Maji kidogo.

So kama unasafari ama vikao vya muda mrefu, hakikisha unakunywa Maji kidogo.
 
Kwahiyo katika hii sijui Cystitis au Prostatomelogy ina maana hapa Dokta itabidi azipime na Pumbu / Kende zangu au?
Yah peleka Pumbu hizo kina Dr.Diddy wazichungulie.

Ila ni Pelvis bhana ko utashusha tu suruali kidogo chini ya kibofu hapo wanafanya yao.
 
Mimi Nina changamoto Hiyo, Madaktari wamenambia ni Bora wewe unapokunywa Maji na baada ya muda si mrefu unaenda kukojoa, means unaondoa Sumu Kwa haraka Mwilini...!

Wakanambia Kukaa masaa 6 ama 10 bila kukojoa sio Sifa, wakanambia usihofu...!

So mm ninachofanya, nimezoea kunywa Maji kila siku asubuhi, nikiwa nasafiri sinywi Maji asubuhi, ila ntakunywa Maji kidogo pale wakati wa Chakula, pia kama Safari tunapata nasafi kwenda Haja Ndogo, tukirudi ndo nakunywa Maji kidogo..!

So kama unasafari ama vikao vya muda mrefu, hakikisha unakunywa Maji kidogo.
Shukran Mkuu. Nitafanya hivyo.
 
Kudadadeki zako umenifanya Nicheke sana Wewe Jamaa. Yaani kabisa nizipeleke Pumbu / Kende kwa Dokta akague?
Si bora wewe kuna hawa wa Scrotal yani zinatawanywa pumbu kule, mjeredi kule sasa hapo ukutane na Dr mwanamke na vile unapakwa KY unaezarusha bao🤣
 
Chukua majani ya mihogo funga kwenye pindo la suruali boksa chupi sketi n.k uwapo safarn au mkutanoni utakuja kunishukuru baadae
 
Si bora wewe kuna hawa wa Scrotal yani zinatawanywa pumbu kule, mjeredi kule sasa hapo ukutane na Dr mwanamke na vile unapakwa KY unaezarusha bao🤣
Umeshanitisha siendi tena Kuchekiwa huko bora nitamfute tu yule Mganga Hatari Demu wa Yanga SC Bagamoyo anitibu.
 
Chukua majani ya mihogo funga kwenye pindo la suruali boksa chupi sketi n.k uwapo safarn au mkutanoni utakuja kunishukuru baadae
Ama hakika leo nimemini kuwa Bange / Bangi ni mbaya sana.
 
Umeshanitisha siendi tena Kuchekiwa huko bora nitamfute tu yule Mganga Hatari Demu wa Yanga SC Bagamoyo anitibu.
Nenda kacheki Mkuu Cash 15k tu kama hutumii bima, kwa kujihakikishia Afya nenda tu kwa maana haiumi wala haina madhara afu hawakuchungulii kama unavyofikiri.

Wazee mliochimbachimba visima vingi mpaka umri wenu uko chini kunakuaga Nyang'anyang'a
 
Nakubalina nawe kama kuna Bingwa wa Kunywa Vimiminika (Soda / Juice) duniani basi naweza kuwa katika 10 bora.
Mchana amua utakojoa mara mbili tu, kunywa vikombe viwili tu vya chai au juisi au maji.

Usiku amua utakojoa mara tatu, kunywa lita moja ya kimiminika chochote.

Acha ushamba. 😎😎
 
Nenda kacheki Mkuu Cash 15k tu kama hutumii bima, kwa kujihakikishia Afya nenda tu kwa maana haiumi wala haina madhara afu hawakuchungulii kama unavyofikiri.

Wazee mliochimbachimba visima vingi mpaka umri wenu uko chini kunakuaga Nyang'anyang'a
Ndiyo umezidi Kunitisha kabisa Mkuu kwani Sisi Watu wa Pwani huwa hatumli Samaki upande Mmoja bali Kote Kote tu.
 
Mchana amua utakojoa mara mbili tu, kunywa vikombe viwili tu vya chai au juisi au maji.

Usiku amua utakojoa mara tatu, kunywa lita moja ya kimiminika chochote.

Acha ushamba. 😎😎
Naona umenitibu na Kunipiga pia na Dongo vile vile Mkuu.....!! Haya bhana.
 
Back
Top Bottom