Je, kuna gharama gani nyingine pale bandarini kwa mtu aliyeagiza gari nje?

Kwani bandarini wanaingia watu wa aina gani
Ngoja nikusaidie wasikutishe, cha msingi andaa elfu 50 ya kuLog In Tancis, wewe nenda kampuni ya clearing and forwarding waombe uwalipe hiyo hela wata log in kisha utasubiria karatasi ya makadirio toka tra, utaenda lipia ila pia lazima ujue gari itakuja kwa meli ipi, ukiijua meli beba hela yako kama dollars 15-25 hivi, utalipia hapo, kisha utaenda kwa kampuni ya clearing uta log in, utapata reference number ukiwa unasubiria karatasi ya tra mtandaoni ukizipata, utaenda lipia benk, pale bandarini tafuta reflector unazamia tena pita geti no 2(omba wale askari tu kuwa unaenda kula pale kwenye mghahawa kisha huyo unaenda pale kwenye jengo lao utaona agents kibao wamezagaa nje na reflectors zao ukitaka kuoita geti no 1 utafeli) kupeleka ili nao waLog In utakaa kusubiria ila tu uwe na subira, kuhusu gharama za bandarini hazifiki laki 3, wewe komaa tu mimi nilitoa gari pale kibishi, hawa maajent wazinguaji tu, jamaa alitaka mil 1 atoe gari mbali ya kodi wakati nikalipa laki 2 naa... nikalitoa.
Komaaa
 
Mara nyingi haiwi tofauti sana na ile wanayokupa TRA kwenye assessment yao.
Kwa kutumia hiyo link mfano wa gari la mwaka 2007 na cc 2400 ni Tzs 12,570,141.84, actual gharama inaweza kuwa Tzs ngapi? Natanguliza shukran.
 
Kwa kutumia hiyo link mfano wa gari la mwaka 2007 na cc 2400 ni Tzs 12,570,141.84, actual gharama inaweza kuwa Tzs ngapi? Natanguliza shukran.

Mkuu haitacheza mbali na hapo, kuna factors/ vigezo vyao wanavitumia. Hii ni indicative tu. 2007 gharama imekua kubwa kutokana na uchakavu.
 
Hahahaha eti mguu kwa mguu jmn kuliwa Bandar in ni kawaida sanaaa
 
Ahsante kwa maelezo yako
 
Kauliza swali la msingi sana [emoji3][emoji3]
Ni kweli mkuu lazima uzijue kila hatua ili usije ukaachwa ferry,halaf baadae ukaja kuanzisha uzi wa vishoka wa bandari[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ngoja nifanye mchakato nimepata ndugu wa kuniongoza nikifanikiwa nitaleta mrejesho hapa
 
Nawezaje kuagiza gari ndogo kama rav4 au starlet toka nje? Used toka Japan inaweza kuwa Tsh ngapi?
 
binafsi huwa sioni maana ya hiyo calculator ya tra. ilitakiwa mtu anapo angalia makadirio ya tozo zote zisipishane kipindi anapokwenda chukua mzigo wake. vinginevyo hiyo calculator haina maana waitoe tuu.
 
Samahani mkuu hivi km nimeagiza gari alafu tin ninayoitumia ina madeni kadhaa ya nyuma sikulipia ya biashara zingine...

Kuna usumbufu wowote ule utatokea!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…