Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
Tuna tatizo kubwa la kuziona fursa na kuzitumia si Serikali tu bali na Watu wake pia.
Wananchi wanaitegemea serikali itengeneze fursa hili vijana na watu wote wenye uwezo au sifa za kuajiriwa na kujiajiri waweze kufanya kazi kwa mustakabali wa maisha yao na ustawi wa taifa.
Cha ajabu level ya ufahamu wa mtawala na mtawaliwa ukiulinganisha kwenye mizania vinalandana na hamna kati yao wa kumnasua mwenzie shimoni.
Nadhani imefikia wakati serikali iwe na kitengo cha watu wenye ufahamu wa juu (GT) ambao wataajiriwa na kazi yao kuu itakuwa ni kufikiri nje ya box nakuleta majawabu juu ya namna gani hasa serikali ifanye kutengeneza fursa mbalimbali za ajira kulingana na uchumi wa taifa letu na nguvu kazi yake.
Ili litawezekana endapo jopo hili la think tankers litashirikisha au litashirikiana kwa ukaribu na jopo la wataalamu, magenius, wanasayansi, matajiri, wabunifu/wenye uthubutu(wajasiriamali), wavumbuzi,wenye vipawa, wachumi n.k
Endapo kitengo hiki kikitumika vyema kuchangia mtizamo wao na maoni yao yakawa yanazingatiwa na kutekelezwa siyo ajabu tunaweza kutoka kwenye mkwamo wa ajira kwa watu wetu.
Miaka nenda rudi ajira kwa majority ya watu wetu zimebaki kuwa kuzalisha mazao kwa zana duni na kuuza malighafi bila kuprocess, ufundi katika level ya chini, usafiri i.e bodaboda,utalii usio na ukomavu, uchimbaji mdogo wa madini na biashara inayopotelea nchi za jirani, ufugaji wa mifugo mingi ila tija kidogo,n.k
Kiukweli tunahitaji watu wanaofikiri tofauti na kuona njia nyingi tofauti za kupita wakati ambapo wote tumefumba macho tunaimizana tuchape kazi wakati kazi zenyewe hazipo.
Jambo hili la kukosa watu wenye upeo na mitizamo chanya ya kuona fursa ambazo zinaweza kutumiwa kusaidia nchi ndiyo kikwazo cha serikali zote za nchi masikini especially bara la Afrika,
Unaweza dhani kuwa watawala hawa hawana mapenzi au uzalendo na maendeleo ya mataifa yao kama viongozi wa nchi za magharibi na kwingineko kumbe hapana,
Ni level yao ya ufahamu na kufikiri ndiyo inawa-limit wakomee hapo na mwisho wa siku nikufuata mfumo wa kiuchumi ule ule usio na matunda wakiombea mabadiliko yatokee na kujipa matumaini kuwa kufuatia miradi kadhaa wanayoitekeleza kwa mikopo au uwekezaji uliofanyika utaweza kuajiri idadi kubwa ya watu wao kumbe ni kinyume chake na matokeo ni kuendelea ku-suffer.
Kiufupi hawa watu wa ajabu wanaoweza kuleta mabadiliko katika suala la ajira na uchumi wa nchi hawatoki kwingineko bali miongoni mwetu Watanzania kuna watu wenye akili kubwa na tunachopaswa kufanya ni kuwa-identify na kuwatumia kwani wengine wapo serikalini humo humo, sekta binafsi na wengine ni majobless.