Je, kuna haja ya kuendelea kutumia Sanduku la Posta (SLP) katika shughuli za kiofisi ukizingatia teknolojia imeshakua sana?

Je, kuna haja ya kuendelea kutumia Sanduku la Posta (SLP) katika shughuli za kiofisi ukizingatia teknolojia imeshakua sana?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,956
Reaction score
47,046
Kwa kuwa namba za simu zote zinaelekea kusajiliwa kwa alama za vidole na matumizi ya simu janja yakiwa yanaongezeka kwa kasi, nadhani ni wakati muafaka sasa kuacha kutumia S.L.P na badala yake namba za simu za mkononi na barua pepe (e-mail) zikawa ndio identity kuu ya namba za mawasiliano, ambapo barua zote zitakuwa zinatumwa kwa email au sms, nadhani kuendelea kuwa na masanduku ya posta ni upotevu wa rasilimali (redundant system).
 
Kwa kuwa namba za simu zote zinaelekea kusajiliwa kwa alama za vidole na matumizi ya simu janja yakiwa yanaongezeka kwa kasi, nadhani ni wakati muafaka sasa kuacha kutumia S.L.P na badala yake namba za simu za mkononi na barua pepe (email) zikawa ndio identity kuu ya namba za mawasiliano, ambapo barua zote zitakuwa zinatumwa kwa email au sms..., nadhani kuendelea kuwa na masanduku ya posta ni upotevu wa rasilimali (redundant system).
Daah siku zote nilikua najua hii ni ID moja.,basi sawa.
Umri wako?
Elimu yako?

dodge
 
Mimi nikitumaga barua lazima nindike na mamba za simu za sehemu husika ndo naridhika.. Haya ma S.L.P sasa no chenga tu.. Yamejaa kama ukoma
 
Kwa kuwa namba za simu zote zinaelekea kusajiliwa kwa alama za vidole na matumizi ya simu janja yakiwa yanaongezeka kwa kasi, nadhani ni wakati muafaka sasa kuacha kutumia S.L.P na badala yake namba za simu za mkononi na barua pepe (email) zikawa ndio identity kuu ya namba za mawasiliano, ambapo barua zote zitakuwa zinatumwa kwa email au sms..., nadhani kuendelea kuwa na masanduku ya posta ni upotevu wa rasilimali (redundant system).
Hakuna haja just weka namba yako ya WhatsApp na IG username
 
FRANCIS DA DON

Nchi zilizoendelea bado wanatumia masanduku ya posta kupata na kutuma barua.

Jiulize wito wa kuitwa kortini na majibu yake utatumia WhatsApp au email. Barua ya matibabu toka hospitali ya Rufaa au kuipeleka utatumia WhatsApp au baruapepe.

Online shopping inazidi kukua sasa wakitaka kuwasilisha mzigo au kifurushi itabidi wasitoe huduma za mlango kwa mlango kupitia SLP au ZIP / Post Code. Hivyo Tanzania itashindwa kupanua soko la online shopping and home delivery.

Si ajabu tunajazana ofisi za Uhamiaji , kadi ya mpiga kura, halmashauri , wilaya , ardhi n.k kufuata passport, nyaraka, kadi, leseni kwa vile hatuoni umuhimu wa SLP.

Kuna mifano lukuki ya umuhimu wa SLP ndiyo maana nchi za Kaskazini bado wanatumia sana barua pamoja na wao kuwa wapo mbele zaidi ktk teknolojia ya mawasiliano na habari pamoja na simu janja.
 
Ukiagiza mzigo alibaba au kwingineko lazima uandike sanduku la posta kwakuwa ni rahisi zaidi kukutres kuliko whatsapp. Jiulize ukiweka namba ya whatsap (tuchukulie inakubalika) halafu bahati mbaya mtu mwovu akashika simu yako na kugundua mzigo wwnye thamani unakuja na uthibitisho ni simu yako, hawezi kucheza na system (ujue tanzania umakini kwenye biashara ni kidogo sana hasa suala la usalama wa mali) na akakuzunguka?
 
Mimi nilijua utapendekeza ishu ya postcode na namba za nyumba(house number) ziboresheshwe zaidi.
Mtu akitumiwa kifurushi atakipataje
Ukitumiwa kifurushi si unaletewa nyumbani kwako kwa kuweka adress ya mtaa na namba ya nyumba pamoja na namba ya simu ili akifika akupigie? Sasa kisanduku cha posta (S.L.P) cha kazi gani?
 
Back
Top Bottom