Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Japo nchi yetu ni masikini, nchi wafadhili wa maendeleo waliokuwa wanatusaidia kwa misaada mbalimbali, wao ndio huamua wasaidie nini. Enzi za Mwalimu Nyerere, kuna wakati tulikosana na wafadhali kutokana na kupewa misaada yenye masharti, hivyo Nyerere akakataa, Mwinyi alipoingia, akakubali kila kitu na ndio maana akaitwa Mzee Rukhsa.
Vivyo hivyo makampuni yanayotengeneza faida, yana sera za CSR, kurudisha kidogo kwenye jamii, sehemu ya faida. Ni makampuni hayo ndio huamua yafanye nini. Mengi ya makampuni hayo hufanya sherehe za milo mizuri kama sehemu ya CSR zao, lakini Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania LTD, yenyewe inafanya CSR ya aina yake ambayo ni CSR endelevu yenye faida kwa kuwajengea uwezo Watanzania kujitegemea wenyewe. Jee kuna haja sasa kwa serikali kufuata ule mtindo wa Nyerere kwa kuyalazimisha makampuni kufanya CSR za misaada endelevu na sio CSR za kugawa chakula, soda, pipi na peremende?
Kwa Maslahi ya Taifa leo, inazungumzia kitu kinachoitwa kwa lugha ya Kiingereza CSR, yaani Community Social Responsibility, ni kitendo cha makampuni, kurejesha katika jamii, sehemu ya faida ya faida inayopata, kwa kufanya jambo lolote kuisaidia jamii.
Tanzania tuna makampuni zaidi ya milioni, na yanatengeneza faida ya mamilioni ya shilingi, kwa baadhi ya makampuni hayo kutengeneza faida kubwa, kulipana mishahara minono, huku jamii iliyowazungunguka, wakiishi katika hali ya umasikini uliotopea.
Mimi natoka Kanda ya Ziwa, eneo lililojaliwa utajiri mkubwa wa madini, kuanzia, Almasi, dhahabu na madini ya vito. Madini hayo yanapatikana chini ya ardhi. Wakazi wa maeneo hayo ndio waliobarikiwa na Mwenyeenzi Mungu kuyamiliki madini hayo, ni yao, lakini kwa vile sio tuu walikuwa hawajui na hata baada ya kujua, hawawezi kuyachimba kwasababu hawana ujuzi.
Wakoloni wazungu walipokuja nchini, waliwakuta Wasukuma fulani wanatumia mawe ya almasi za mviringo zilizokuwa zinaokutwa mtoni, kuchezea mchezo wa bao. Wazungu hao, wakagundua kuwa mawehayo ni almasi, ambayo kwa wakati huo ndio madini yenye thamani kubwa kuliko madini yote ya vito. Wakarudi zao kwao ulaya, wakatengeneza gololi za chupa zenye mviringo mzuri kuliko yale mawe ya mtoni, wakazitia na nakshi nakishi za rangi rangi za kupendeza, wakazileta nchini kwetu hizo gololi na kwenda kuwagawia bure wale wazee wa Kisukumu, kwa kubadilishana na zile Almasi walizotumia kuchezea bao, Mababu zetu wakapewa gololi nzuri za kupendeza, wakafurahi sana na wao kuzitoa almasi zao zote walizokuwa nao na kuwapa wazungu hao, kumbe masikini mababu zetu, hawakujua, wamefanywa mazuzu!, na kule kufurahia gololi na kutoa almasi ulikuwa ni uzuzu, kwa sababu walikuwa hawajui.
Baada ya Wakoloni kugundua utajiri huo wa madini ya almasi, wenyeji wa maeneo hayo, wakahamishwa, ukajengwa mgodi wa kwanza nchini na mzungu Fred Williamson, eneo la Mwadui mkoani Shinyanga na kuitwa kwa jina lake. Kwa wale waliowahi kufika Mwadui, ukaingia mgodini, ukaona maisha ya wafanyakazi wa wa Mgodi wa Mwadui ukilinganisha na maisha ya wale Wasukumu wenye almasi zao, kama una machozi ya karibu, unaweza kulia!
Hali ni hiyo karibu maeneo yote yenye madini nchini, baada ya kugunduliwa madini, wenyeji huamishwa eneo hilo na kupewa wawekezaji, ambao huliendeleza kwa kujenga makambi yenye miundombinu ya kisasa, wafanyakazi wa migodini kulipwa vizuri, kuishi vizuri kama peponi, huku wenyeji ambao hao ndio wamiliki halisi wa madini hayo wakiiishi katika maisha ya umasikini uliotopea.
Hali hii ya makampuni kutengeneza faida kubwa, iko kwa makampuni mengi na sio tuu makampuni hata wafanyabisha wengi, ambao faida yao inatokana na jamii iliyowazunguka lakini ukilinganisha wanachopata na faida wanayorudisha kwa jamii ni mbingu nan chi!
Ili kuishi vizuri na jamii waliowazunguka, kakampuni haya ndio yamebuni sera ya CSR, kurudisha kidogo kwenye jamii, wakoloni wao walichorudisha kwenye jamii ya wale Wasukuma wa almasi ni gololi, kuna makampuni yanarudisha soda, peremende na mlo wa siku moja kwa jamii iliyowazunguka!
Kwa nchi za wenzetu zinazoitwa Tiger Nations, wanamsemo “Ukiwakuta watu wamezungukwa na samaki, huku wanalala njaa kwasababu hawawezi kuvua samaki, usiwavulie samaki na kuwapa mlo wa samaki, wale washibe walale, ukitaka kuwasaidia, ni badala ya kuwagavia bure samaki, wafundishe kuvua samamaki kwa kuwajengea uwezo na kuwapa vifaa”. Nchi hizo sisi Tanzania tulipata nazo uhuru wakati mmoja, ile miaka ya 60s, sisi tukiwa na kila kitu, wenzetu wakina na nothing!. Lakini leo tukijilinganisha nao ni mbingu nan chi!
Makampuni mengi wanafanya CSR za kugawa vyakula, au hata tafrija, na karamu. Kila Bunge jipya linapozinduliwa makampuni yanashindana kudhamini tafrija mchapalo ya uzinduzi wa Bunge jipya, enzi za JPM, alipoambiwa kiasi cha fedha kinachotumika kwenye tafrija hizo, huku mahospitalini wamama wajawazito wanalala chini kwa kukosa vitanda, aliwahi kuingilia kati kuifuta tafrija mchapalo na kuamuru fedho hizo zinunulie vitanda mahospitalini.
Juzi kati nilimsikia Spika wa Bunge akitangaza ile benki yetu kubwa kuliko benki zote nchini, iliamua kuwafutirisha Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, badala ya kuwafuturisha kwa mlo wa futari, benki hiyo ikaamua kuwafuturisha kwa kuwagawia bahasha nene zilizotuna, kila mtu atafuturu kwa wakati wake, hivyo Mhe. Spika akampisha Naibu Spika kuendelea kuendesha kikao nay eye kwenda kuzipokea bahasha nene za futari ya waheshimiwa Wabunge!
Kwa vile na mimi ni mteja wa benki hiyo, na ni sisi wateja ndio tunao iwezeshesha benki hiyo kutengeneza faida kubwa kupitia amana zetu, sikumbuki hata siku moja kwa sisi wateja kuwekewa hata senti tano ya kununulia soda na peremende kama shukrani kwa faida tunayoizalishia benki yetu, lakini Waheshimiwa Wabunge wetu ndio wanaogawiwa bahasha nene ya CSR ya faida ya benki yetu, faida ambayo tunayoizalisha ni sisi!. Ama kweli mwenye nacho ataongezewa!, badala ya kufurisha masikini, wanafuturishwa matajiri!
Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergiea ni moja ya makampuni makubwa ya mafuta nchini, yenye kufanya CSR ya kulisaidia taifa. Kila mwaka inafanya shindano la kubuni miradi mipya na kutoa shilingi milioni zaidi ya 100, kwa miradi inayoshinda, kuzitumia kujengea uwezo ili miradi hiyo iwe ni miradi endelevu.
Katika kuwatunuku washindi wa mwaka huu, serikali, imeendelea kusisitiza azma yake ya uzalishshaji wa ajira mpya , milioni 8, na katika kulifanyikisha hilo ni kwa kutumia ushirikishaji wa sekta binafsi, hivyo imeahidi itazifanyia mapitio sheria zote za biashara ili kuboresha zaidi mazingira ya kufanya nchini na kuiwezesha sekta binafsi kuzalisha ajira na kuchangia kukua kwa uchumi na kuongeza pato la taifa.
Ahadi hiyo imetolewa na jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Ashatu Kijaji, katika hafla ya kuwakabidhi zawadi za fedha taslimu Shilingi milioni 60, kwa washindi watatu wa kwanza wa shindano la ubunifu wa miradi kwa vijana wa Kitanzania, iliyofanyika jana usiku katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijjini Dar es Salaam.
Katika Hotuba ilityosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Ali Gugu, Waziri Kijaji amesema, sekta binafsi ndio injini ya uchumi wa taifa, hivyo serikali ya awamu ya 6, itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara ili wajasiriamali wadogo na wakati, nao wakuwe na kuzalisha kada ya mamilionea na mabilionea wazawa ambao watachangia katika uchumi wa taifa.
Ali Gugu, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies kwa shindano hilo, na kutoa zawadi za zaidi ya shilingi milioni 100, kati ya hizo, washindi watatu wa mwanzo, kila mmoja amepewa hundi ya shilingi 20 za Kitanzania kuboresha mitaji yao na kuwalea kwa mwaka mmoja kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo, na kuwaangazia fursa za masoko.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp, mesema lengo la kampuni ya TotalEnergies, isio tuu kufanya biashara na kuzalisha faida, bali kuitumia hiyo faida inayopatikana na kuwajengea uwezo na wengine ili kuwainua Watanzania na kuliinua taifa kiuchumi.
Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile, amesema Shindano hilo la “STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE BY TOTALENERGIES limefanyika katika nchi zaidi ya 50 barani Afrika, kwa Tanzania, wamejitokeza wajasiriamali zaidi ya 1000 kushiriki shindano hilo.
Kama makampuni mengine yote yanayofanya biashara Tanzania na kutengeneza faida, badala ya kufanya CSR za kugawa peremende, na badala yake zikafanya CSR za kujenga uwezo, Tanzania tungekuwa wapi?.
Wasalaam.
Paskali