Je, kuna haja ya kuwa na timu ya Taifa Stars?

Mugabe one

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Posts
2,327
Reaction score
1,683
Kila wakati timu yetu ya taifa haifanyi vizuri kwny mashindano! Je ni kwann? Je kwnn tusiifute tu Na tusiwe Na timu ya taifa ya Mpira wa miguu?
 
Ukiwa na baba asiye na mchango wowote na familia utamuuza au utamtafutia sababu uumue?
 
Labda ungeuliza kuna haja ya kuwa na waziri wa Michezo na utamaduni anayelipwa mamilioni kwa kodi za wanyonge wakati ubunifu ni ziro?
Kazi yao ni kukimbizana na watu wanaowakosoa kwenye Sanaa wakati hawana jamba jipya wanalobuni au kuanzieha lenye manufaa na taifa.
 
Walifuta umiseta!wairudishe umiseta wataipua vipaji!
Waje mitaani pia kuna vipaji kibao
Waachane na wakina yondani etc
Kutwa tunakesha nao kwenye kuvesha mitungi

Ova
 
Mechi nyingine wapelekwe wanajeshi
 
Hivi Tz tunaweza nini cha kujivunia Africa ?!
Labda uswahili . Uwezo wetu mdogo sana kwa almost kila kitu.
 
Hata chama cha mapinduzi a.k.a ccm sioni kama kuna haja ya kuwa nacho maana tunaongozwa na vichaa sasa chama gani hicho cha vichaa
 
Mi huwa najiuliza sana, inakuwaje tunakosa watu wanaojua kucheza mpira vizuri kama kwa wenzetu? Timu yetu ya Taifa kufungwa ni kawaida, vilabu vikienda nje, ni kufungwa tu, mbona majirani zetu au nchi za Afrika magharibi zinafanya vizuri, kwann tusiende kujifunza wanavyofanya? Tujue wanakula nn, wanafanya mazoezi gani, wafundishwa nn! Kama kuna kizazi maalum cha mpira, basi tupeleke dada zetu huko wakatiwe mimba waje watuzalie hicho kizazi na huku tupate wachezaji!!
 
Mpeleke mkeo kwanza ili upate mbegu nzuri ya mcheza mpira
 
Hivi Tz tunaweza nini cha kujivunia Africa ?!
Labda uswahili . Uwezo wetu mdogo sana kwa almost kila kitu.
Hatuwezi jambo lolote kwa sababu ya wenzetu na dugu zetu waliogeuka kuwa Wanyonyaji na wakoloni halafu wanasingizia wazungu na nchi za magaharibi kuwa wao ndio wanatukwamisha.

Leo hii kila kitu ni siasa tu. Mashindano ya michezo kama zamani yamebaki yale makombe ya wanasiasa tu huko vijini ambapo kuna vipaji.
Maeneo yenye vipaji lakini wakigundulika kuwa sio wapiga kura wa CCM basi hata michezo itaonekana ni mikutano ya hadhara na maandamano na atakayefadhili mashindano ataandamwa na wakuu wa wilaya mpaka alie kilio cha mbwa koko.

Vipaji vya soka vinajulikana kuwa vipo Vijijini. Na kuna mikoa soka likifundishwa wanafundishika na kuna mikoa soka ni Kipaji.
Kigoma soka ni kipaji
Mtwara soka ni kipaji,
Tabora soka ni kipaji
Tanga soka ni kipaji
Shinyanga soka ni kipaji
Morogoro soka ni kipaji.
....Kilimanjaro na Arusha wakifundishwa wanafundishika vizuri na kuwa wachezaji wa kisasa.
Mwanza wakifundishwa wanafundishika.
Kagera wakifundishwa wanafundishika.
Mbeya na Iringa wakifundishwa wanafundishika .
Ruvuma wakifundishwa wanafundishika . Pemba wakifundishwa wanafundishika.

Hayo maeneo mengine wabaki tu kama washangiliaji na wachezaji wa mdomoni na midadi.
Waelekeze nguvu zao kwenye Michezo mingine kama riadha , ngoma , ngumi n.k.
 
Unajua soka letu limetawaliwa na siasa.
Kuna Timu zimeundwa kisiasa kabisa. Sasa unategemea nini?
Hapo wanasiasa ndao wanaoharibu kila kitu kwenye nchi hii kwa sababu tu wameshindwa kulifanya taifa liwe moja.
Uchama umekua ni kitu cha muhimu sana kwa wanasiasa kuliko utaifa.

Siku mavyama haya yakisiasa yatakapokufa na kuzaliwa mengine itakua ndiyo siku nchi hii itakua na maono kwenye kila kitu na kufanikiwa.
Sera ya michezo iko kisiasa. Waziri wa michezo yupo kichama chama na anawaza chama chake tu na kupata umaarufu. Kazi yake imekua kutunga sheria tu kandamizi badala ya kutumia zile zilizopo kuja na ubunifu wa namna ya kujenga soka na michezo kwa ujumla akishirikiana na waziri wa Elimu badala yake ni matamko tu yasiyoisha.
 
Reactions: Bal
Taifa stars Wachezaji Wengi Wana Uwezo Mdogo.

Hiyo ni ishara moja wapo ya Mifumo iliyooza ya baadhi ya Taasisi na Sekta nyingi hapa bongo.

Wengi Wenye Uwezo na vipaji wapo nje ya Mifumo huku Wenye uwezo mdogo sana wapo lukuki ndani ya Mifumo.


Nani anakujua, Na sinini Unajua (Ujuzi,Maarifa na kipaji).
 
Reactions: Bal
Walifuta umiseta!wairudishe umiseta wataipua vipaji!
Waje mitaani pia kuna vipaji kibao
Waachane na wakina yondani etc
Kutwa tunakesha nao kwenye kuvesha mitungi

Ova
Hata wachezaji wa Ulaya wanalewa pombe
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kwa wenzetu mpira kazi na ndio maana wanaithamini kazi yao.

Ila hawa wa kwetu njaa zinawahangaisha wamekosa cha kufanya hawajasoma wameamua kucheza mpira tutarajie nin?

Kupiga hatua kma ilivyo team kma nigeria,morroco na team nyengine bdo sana.
 
Mkuu unasema tukifundishwa tunafundishika.

Wakati team ya taifa imechukua wachezaji wawili watatu kutoka visiwani.

Huku ball nature sema tu bara wanatubania sana ndio maana tukapokonywa uanachama CAF.
 
Walifuta umiseta!wairudishe umiseta wataipua vipaji!
Waje mitaani pia kuna vipaji kibao
Waachane na wakina yondani etc
Kutwa tunakesha nao kwenye kuvesha mitungi

Ova
Wakati wa UMISETA tulifanya nini?
 
Kabla ya vyama vingi hao wenye vipaji waliifanyia nini Tz? Wewe ni mmoja wa hao wachawi wanaoconnect kila kitu na siasa.
 
Kilichotokea Cape verde tukaja tukakisawazisha nyumban, sasa kimetokea kilekile cha Cape Verde huko LESOTHO. Ukiunganisha waweza pata image chonganishi na hasa ukiangalia jamii janja janja kutoka kule linapozama jua.
NB: Mpira una matokeo matatu, ila kuna matokeo mengine hata shetani anaweza likataaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…