je kuna haja ya kuwa na tuzo za mwalimu bora mwaka huu??

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Kwenye vyombo mbalimbali vya habari niliona maandalizi ya kutoa tuzo ya walimu walio fanya vizuri kitaifa. Je kutokana na matokeo ya mwaka huu kuna haja ya kutoa hizo tuzo?. kwangu mimi naona kama ni sawa na kuwashukuru walimu kwa kufelisha.
Hata Mo Ibrahim mwaka 2012 hajatoa tuzo kwa rais yoyote sababu hakuna aliye kidhi vigezo. sasa iweje tanzania tuwape walimu tuzo wakati wamefanya vibaya?. ni hayo tu. mia
 
kwa hiyo na mwanafunzi bora asiwepo? we hujui learning inahusisha vitu vingi ikiwepo nature,narture ukiacha mwalimu,na juhudi za mwanafunzi ume assess vipi ukajua mwalimu ndo kafelisha? learning ni interactive process.
 
Vigezo gani unavyovitaka? Mi nadhani kuna shule zimefanya vizuri kwa kadiri ya uwezo wao na wanastahili kupewa motisha.
 
Why not, kufeli kwa wanafunzi siyo tatizo la walimu pekee ndio maana umesikia PM anaunda tume, kama ingelikuwa walimu tu kusingelikuwa na haja ya tume maana tatizo lingekuwa already clearly identified.
 
Wengine wameshajipa zawadi tayari,Singida Maafisa ofisi ya Elimu wiki iliyopita wali safiri hadi mbuga ya ngorongoro kwa gharama za walipa kodi kujipongeza japo ni miongoni mwa mikoa duni kabisa katika ufaulishaji.
Unataka wajilipe mara mbili?
 

Waliofanya vibaya ni Walimu au wanafunzi!pili 2zo zinawahusu walimu na sio wanafunzi.
 
Why not, kufeli kwa wanafunzi siyo tatizo la walimu pekee ndio maana umesikia PM anaunda tume, kama ingelikuwa walimu tu kusingelikuwa na haja ya tume maana tatizo lingekuwa already clearly identified.
unataka kusema kufeli kwa wanafunzi walimu hawahusiki?. una uhakika migomo ya walimu haiwezi kuwa sababu moja wapo ya wanafunzi kufeli?. mia
 
unataka kusema kufeli kwa wanafunzi walimu hawahusiki?. una uhakika migomo ya walimu haiwezi kuwa sababu moja wapo ya wanafunzi kufeli?. mia

Nimesema kufeli kwa wanafunzi siyo tatizo la walimu pekee rudi usome vizuri, hii sio kwamba walimu hawahusiki la hasha, ila lazima kuna sababu nyingine nyingi na nyingine kulingana na serikali hawazijui thus why wameunda hiyo tume mkuu. Nikaendelea kusema kama sababu ingelikuwa walimu pekee basi kusingelikuwa na haja ya kuunda tume, maana tatizo lingelifanyiwa kazi.

Labda nami niseme hapa, hakika kufeli kwa wanafunzi kuna changamoto nyingi sana ambazo nyingine zitachukua muda mrefu sana kutatuliwa mkuu. Tofauti na matatizo ya walimu kuna matatizo mengine mengi ambayo yanachangia watoto wetu kufeli ama kupata ufaulu hafifu,
mfano;
1.Upungufu wa vitabu mashuleni, maana hata huyo anayetupiwa lawama (Mwalimu) ili afundishe vizuri lazima awe vitabu vya kutosha ili asome na kuandaa nini afundishe.

2. Kwenye shule zetu hakuna maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi na hata baadhi ya shule chache zenye maabara hakuna vifaa vya kutosha (Laboratory apparatus) na chemicals kwa ajili ya testing, leo mwanafunzi anafeli hilo nalo atupiwe mwalimu, munamwonea bure

3. Wanafunzi na wazazi kwa upande wao nao hawatimizi wajibu wao ipasavyo, wajibu wa mwanafunzi ni kusoma kwa bidii na wajibu wa wazazi ni kutengeneza mazingira rafiki kuhakikisha mtoto anapata huduma za masomo na kusimamia mtoto nk.

4. Kuna upande wa Serikali ambao hakika nao umefanya madudu mengi, nenda mashuleni hakuna nyumba za walimu, hakuna office za walimu, vitabu vichache, walimu wachache, walimu hawana hata viti vya kukalia kazini hayo masomo yaandaliwe wapi, na mengine mengi.

5. Aidha pia ukumbuke hawa watoto waliofeli form four mwaka huu ni zao lile ambalo liliambiwa hata mkifeli form two hakuna kurudia mwaka, hivyo wakalemaa tangu wakiwa kidato cha kwanza. Asikundanye mtu uwepo wa mtihani wenye uwezo wa kufelisha unamfanya mwanafunzi kuongeza juhudi, sote tumepita huko tunalijua hili tusifike mahari tukasahau, tutaua taifa letu kwa mzigo wa ujinga.

Mwisho niliposema kwa nini hizo tuzo za walimu kwa nini zifutwe sikukurupuka mkuu, nilitafakari japo kidogo, ingawa mimi sio mwalimu lakini mimi ni mzazi na haya nayaona sana.

Kila la kheri katika tafakari yako
 
Kuna haja kwa 7b sio shule zote wfunz wake wamefel,pia mwl japo ni sehem ya kufel lakn pia sio mfelshaj,serkal na inahuska kwa kiwango cha hali ya juu kwa kupuuza matatzo ya walm kwa kuwafanya waish knyonge,namalza kwa kusema
"tuzo zna umuhm mkubwa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…