unataka kusema kufeli kwa wanafunzi walimu hawahusiki?. una uhakika migomo ya walimu haiwezi kuwa sababu moja wapo ya wanafunzi kufeli?. mia
Nimesema
kufeli kwa wanafunzi siyo tatizo la walimu pekee rudi usome vizuri, hii sio kwamba walimu hawahusiki la hasha, ila lazima kuna sababu nyingine nyingi na nyingine kulingana na serikali hawazijui thus why wameunda hiyo tume mkuu. Nikaendelea kusema
kama sababu ingelikuwa walimu pekee basi kusingelikuwa na haja ya kuunda tume, maana tatizo lingelifanyiwa kazi.
Labda nami niseme hapa, hakika kufeli kwa wanafunzi kuna changamoto nyingi sana ambazo nyingine zitachukua muda mrefu sana kutatuliwa mkuu. Tofauti na matatizo ya walimu kuna matatizo mengine mengi ambayo yanachangia watoto wetu kufeli ama kupata ufaulu hafifu,
mfano;
1.Upungufu wa vitabu mashuleni, maana hata huyo anayetupiwa lawama (Mwalimu) ili afundishe vizuri lazima awe vitabu vya kutosha ili asome na kuandaa nini afundishe.
2. Kwenye shule zetu hakuna maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi na hata baadhi ya shule chache zenye maabara hakuna vifaa vya kutosha (Laboratory apparatus) na chemicals kwa ajili ya testing, leo mwanafunzi anafeli hilo nalo atupiwe mwalimu, munamwonea bure
3. Wanafunzi na wazazi kwa upande wao nao hawatimizi wajibu wao ipasavyo, wajibu wa mwanafunzi ni kusoma kwa bidii na wajibu wa wazazi ni kutengeneza mazingira rafiki kuhakikisha mtoto anapata huduma za masomo na kusimamia mtoto nk.
4. Kuna upande wa Serikali ambao hakika nao umefanya madudu mengi, nenda mashuleni hakuna nyumba za walimu, hakuna office za walimu, vitabu vichache, walimu wachache, walimu hawana hata viti vya kukalia kazini hayo masomo yaandaliwe wapi, na mengine mengi.
5. Aidha pia ukumbuke hawa watoto waliofeli form four mwaka huu ni zao lile ambalo liliambiwa hata mkifeli form two hakuna kurudia mwaka, hivyo wakalemaa tangu wakiwa kidato cha kwanza. Asikundanye mtu uwepo wa mtihani wenye uwezo wa kufelisha unamfanya mwanafunzi kuongeza juhudi, sote tumepita huko tunalijua hili tusifike mahari tukasahau, tutaua taifa letu kwa mzigo wa ujinga.
Mwisho niliposema kwa nini hizo tuzo za walimu kwa nini zifutwe sikukurupuka mkuu, nilitafakari japo kidogo, ingawa mimi sio mwalimu lakini mimi ni mzazi na haya nayaona sana.
Kila la kheri katika tafakari yako