Je, kuna haja ya Spika Ndugai kumjibu Mbowe juu ya tafsiri halisi ya Katiba na Kanuni kuhusu kiapo cha mbunge?

Huyo job kesho amuapishe chakubanga garage ya bunge ndio tutajua ni kanuni za bunge,hiyo picha hayo job hawezi kuhandle lazima aanguke tu cd4 zimepungua sana baada ya cdm kuwafukuza covid-19
 
Mimi naona hao wawili, kila mmoja ananukuu kifungu anachoona kinamsaidia zaidi. Inawezekana nikakosea, lakini mimi naona huenda spika yuko sawa. Kwanza Mbowe kakiri kwa namna moja kuwa hicho kifungu kipo na kilitokea kamati aliyokuwemo. Huu ni ushahidi kifungu hiki kipo. Kama kipo, basi Ndugai hakukosea. Kama kamati ilikitunga lakini Mbowe sasa anadai ni batili, ubatili huo utahitaji tafsiri ya kisheria na si mabishano kati ya Mbowe na Ndugai. Hii hoja ya Mbowe juu ya ubatili wa kifungu hiki kwa nini haikutolewa mapema? Mpaka sasa kifungu hiki ni sheria ingawaje kinaweza kuwa sheria mbovu, ni juu ya wahusika kwenda mbele kama kitaonekana kibovu kifutwe na mahakamma (unconstitutional).
 
Wafungulieni kesi mahakamani
 
Spika akamwapishe polepole kichochoroni kama alivyowaapisha covid 19
 
Napata shida Sana na baadhi ya wasomi wa Tanzania wakishajiingiza kwenye siasa,hata kama wana PHD wanakuwa hana tofauti na mwanafeunzi wa chekechea.Tatizo nini hasa?
Ukiingia ccm kichwa hufuta data zote na kusalia na darasa la awali na Elimu mpya inayopatikana mlemle ya kuwaandama wapinzani
 
Ndungai alijua anafanya makosa kuwaapisha covid 19 wasio na baraka za kamati kuu ya chadema ndiyo maana aliwapeleka vichochoroni akijua endapo kinanuka inakuwa rahisi kuwakwepa kuruka kimanga
 
Kuhusu viapo vya wabunge, katiba inasema hivi



Ingawa ni kweli kuwa Bunge siyo jengo au ukumbi, bali ni sehemu yoyote ambapo kikao cha bunge kifanyika kukiwapo na spika pamoja na wabunge; kwa mfano Bunge linaweza kukutana Karimjee hall au Msekwa Hall au ukumbi wowote lakini lazima awepo spika katika nafasi yake, pamoja na wabunge katika nafasi zao. Siyo lazima wabunge wote wawepo lakini kukisha kuwapo na spika pamoja na wabunge kiofisi basi ni halali. Fimbo ya spika, Nembo ya taifa, bendera ya taifa na picha ya rais ni alama zinazotakiwa kupo ili kuonyesha kuwa wapo pale kama kikao cha Bunge. Kukosekana kwa kimojawapo kati ya alama hizo kunatia shaka uhalali wa kikao kile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…