Mimi naona hao wawili, kila mmoja ananukuu kifungu anachoona kinamsaidia zaidi. Inawezekana nikakosea, lakini mimi naona huenda spika yuko sawa. Kwanza Mbowe kakiri kwa namna moja kuwa hicho kifungu kipo na kilitokea kamati aliyokuwemo. Huu ni ushahidi kifungu hiki kipo. Kama kipo, basi Ndugai hakukosea. Kama kamati ilikitunga lakini Mbowe sasa anadai ni batili, ubatili huo utahitaji tafsiri ya kisheria na si mabishano kati ya Mbowe na Ndugai. Hii hoja ya Mbowe juu ya ubatili wa kifungu hiki kwa nini haikutolewa mapema? Mpaka sasa kifungu hiki ni sheria ingawaje kinaweza kuwa sheria mbovu, ni juu ya wahusika kwenda mbele kama kitaonekana kibovu kifutwe na mahakamma (unconstitutional).