Je, kuna haja ya Tanzania kutoa Tamko la Wananchi kukaa ndani kwasababu ya COVID-19?

Je, kuna haja ya Tanzania kutoa Tamko la Wananchi kukaa ndani kwasababu ya COVID-19?

Quinn

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
473
Reaction score
1,184
Kwa maoni yangu ni HAPANA:

Wananchi wengi Tanzania au Africa kwa ujumla wana kipato cha chini ambacho utokana na shughuli za biashara ndogo ndogo hivyo kumzuia kutotoka nje ni sawa na kusababisha janga lengine la njaa pengine wengi watakufa kuliko hilo gonjwa lenyewe la COVID-19.

Watanzania wengi ni hand to mouth earners yaani inampasa afanye shughuli fulani ili mkono uende kinywani, je kumzuia mtu uyu akae nyumbani si ni swala la kutaka kumuua kabla ya hata ugonjwa huo na pengine ugonjwa huo angepona lakini njaa haina kupona usipopata chakula.

Uhalifu utaongezeka sana maana watu watakosa vyakula ndani na ukizingatia kama ni mfanyabishara basi kipato kimesimama na hivyo itawashawishi watu kuvunja nyumba za watu hasa wenye vipato vya kati na juu ili wapate chakula kwa lugha rahisi itakuwa kama Congo wale wapiganaji ya makundi ya waasi wanavyo vamia makazi ya watu kupora vyakula.

Ugonjwa wa COVID-19 kutokana na majibu ya maabara za China inaonyesha kuwa vijidudu vyake vinastawi vizur kwenye ubaridi au low temperatures hvyo hakuna haja ya kuchukua hatua kali haraka ambazo utawapoteza wananchi wako kwa njaa.

Kwa hali ya kawaida ugonjwa huu una low prevalence kwenye nchi za joto hivyo maamuzi ya kukurupuka haitakiwi hata kidogo. Corona virus ni kama Dengue ya kipindi kile ambacho kwa nchi zilizokuwa kwnye joto basi hali ilikuwa mbaya ila kwa wenzetu Dengue ilikuwa haipo na wala kutokuwa na madhara kma ilivyokuwa huku.

Maamuzi yaliyochukuliwa na Uganda , Rwanda na Kenya ya wananchi kukaa nyumbani na kutumia dola kuzuia wanaotembea ni ya kukurupuka.

Picha hii chini ni mwanamama mfanyabiashara wa kiganda akitoa machozi baada ya kufukuzwa na polisi yaani arudi nyumbani ili kupambana na maambukizi ya corona lakini kinachomliza ni atapata wapi pesa ya chakula kwa ajili ya familia yake??

IMG_7458.JPG



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ipo haja kulingana na hatari ya ugonjwa wenyewe ila halitekelezeki kwa hiyo hamna haja ya kutoa tamko!
 
Kwa kuna tamko la kulala kwenye mawe na kunywa chai....... Endelea kusubiri matamko mengine yanayofanana na hayo
 
hand to mouth earners wanakula viboko kwenye nchi ambazo viongozi wake ni masikini wa akili!
1585490123_1585490123-picsay.jpeg
 
hand to mouth earners wanakula viboko kwenye nchi ambazo viongozi wake ni masikini wa akili! View attachment 1403197

Sijui viongozi wengine wanatumia nini kufikiria... ni wavivu wa kufikiria kwani wanashindwa kusoma mazingira ya maeneo wanayo yaongoza ili kutumia njia mbadala za tofauti na mataifa yaliyo endelea.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ipo haja kulingana na hatari ya ugonjwa wenyewe ila halitekelezeki kwa hiyo hamna haja ya kutoa tamko!
Njia ya kuzuia watu mitaani wataipenda ni wale walioajiriwa serikalini au sehemu nyingne ambao hata wakikaa nyumbani mshahara unaingia.....ogopa sana kitu kinachoitwa majukumu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Njia ya kuzuia watu mitaani wataipenda ni wale walioajiriwa serikalini au sehemu nyingne ambao hata wakikaa nyumbani mshahara unaingia.....ogopa sana kitu kinachoitwa majukumu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Korona nayo ni hatari sana aisee sijui utumike utaratibu gani kwa sababu hata wenye mishahara wana mishe,rwanda wanagawa chakula labda ndo way forward kwa muda hadi hatari ipite!
 
Lockdown haitamwathiri raia tu hata serikali yenyewe ndio maana Trump amesema watu waendelee na shughuli ili kuepusha kudondoka kwa uchumi kwhyo tunaona kabsa endpo nchi inaamulu lockdown basi hat uchum wa nchi utashuka..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom