Je, kuna kabila la Wamasai na Waarusha?

Je, kuna kabila la Wamasai na Waarusha?

Baba Mama

Senior Member
Joined
Apr 1, 2018
Posts
107
Reaction score
138
Kuna mjadala ambao sijawahi kupata jibu la uhakika. Inasemekana kuna kabila na wamasai na kuna kabila la Waarusha.

Je, ukweli ni upi kwa wanaofahamu.
Screenshot_20180417-173319.png
 
Wacha nisubiri wenye Arusha yao waje wajibu, ila mtaani sisi Mmasai twamwita Masai, Mwarusha twamwita Muarusha, sijuagi kama ni kabila moja wale watu
 
Wacha nisubiri wenye Arusha yao waje wajibu, ila mtaani sisi Mmasai twamwita Masai, Mwarusha twamwita Muarusha, sijuagi kama ni kabila moja wale watu
Hebu nisaidie kuwaita basi
 
Hayo makabila ndio hao umeweka picha zao...[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Ndio yapo
Waarusha ni wamasai koko na wamasai ni wamasai original

MWARUSHA HAJUI HATA KUPANDISHA MORI AU KURUKA KIMASAI[emoji1] [emoji1]
 
Wamasai na Waarusha ni makabila mawili tofauti japo Yana muingiliano wa tamaduni kama mavazi, lugha (japo matamshi hutofautiana kidogo) vyakula, nk. Waarusha huwa wanapatikana maeneo ya Meru Arusha Mjini mpaka Namanga na watu huwachukulia kama class ya Wamasai walioendelea au civilised na sio kama wale wa porini. [HASHTAG]#Ninavyoelewa[/HASHTAG].
 
Wa arusha wengi walitokea Kilimanjaro wakawa wanatafuta fertile soil wakawa wanakimbilia mount meru na mount mery kule kulikuwa na wamasai tayari na kulikuwa na mapori na wa nyama. Wamasai hawalimi waarusha walienda kulima.
Ule muingiliano wakaanza kuingiliana kuona na lugha wakawa wanashare

Wamasai wakishaona sehemu watu wanalima na kuna waswahili kwenye mapori huwa wanahama mataokea Yake wakahama wakawaacha wageni.

Na mapori mengi yaliyo na fedha kuwaamisha wamasai ni kama unasukuma mlevi.

Unanunua eneo kama unataka kulima unalima alafu siku ng'ombe akaingia kwenye Shamba lako unakamata unapeleka Polisi unamtandika faini ya mil 5 kwasababu ni waoga wamahakamani baada ya miez mitatu wanaanza kuhama taratibu kutafuta eneo lengine.

Kimbilio la wamasai kwa sasa ni kwenye hifadhi pekee. Maana hifadhi huwezi nunua ardhi wala kufanya economic activity.
 
Back
Top Bottom