Huwa siachi kujiuliza. Tangu CCM itekwe na mafisadi, kuna kitu cha maana au kizuri tunaweza kujivunia kama watanzania? Kila uchao, tunatekwa, tunauawa, tunapotezwa, tunatishwa, tunayonywa, tunadharauliwa, tunauzwa na kubinafsishwa, tunanyamazishwa, tunachanganywa na kuchanganyikiwa bila kusahau wanaotuchanganya nao wakajichanganya. Tumegeuka kituko bila sababu japo wahusika wanaendelea kufanya vituko na kutaka wasifiwe kwa hilo. Leo ukiulizwa wazi wazi au sirini, kipo kweli cha kujifunza au kujivunia toka kwa CCM ya sasa?