Je kuna lugha bora kuliko nyingine?

Je kuna lugha bora kuliko nyingine?

Kazi kubwa ya lugha ni mawasiliano...yanaweza kuwa ya kuhimiza kulazimisha, kushauri, kuuliza,kueleza, na mengineo...Hivyo kama lugha haikidhi mawasiliano katika nyanja mbali mbali ndipo tunasema haina ubora...ila kama inakidhi mawasiliano bhas hiyo lugha ni bora.

Hakuna lugha bora kuliko nyingine..lugha ni bora kwa watumiaji atakaesema sema lugha ya mtu sio bora basi sio mtumiaji wa hiyo lugha..mfano kisukuma ni bora kwa wasemaji wake, kiingereza ni bora kwa wasemaji wake,kiswahili hivyo hivyo
 
Muwafaqa !

Sawa mimi nitatumia hoja zifuatazo ambazo pia hutumiwa na wataalamu mbalimbali wa lugha ya kiswahili;
1. Kufanana kwa msamiati wa msingi wa lugha ya kiswahili na ule wa lugha za kibantu.
Mfano: kiswahili neno mtu
Kindali mundu
Kiwanji munu
Kiswahili maji
Kinyakyusa misi
Kisafwa minzii
Hii nitofauti na lugha nyingine mfano kiingereza- water(maji), a person (mtu)au lugha ya kiarabu pia ukapata maneno tofauti.
N.k pia unaweza kutumia lugha nyingine za kibantu kwa maneno hayo au mengine ukaona jinsi yanavyofanana au kukaribiana matamshi, na tofauti yake huwa ni ndogo sana.

2. Muundo wa sentensi za kiswahili na zile za kibantu.
Sentensi za lugha hizi huwa na muundo wa kiima(mtenda) arifu( taarifa ambayo huanzia kwenye kitenzi katika sentesnsi.
Mfano.
Kiswahili. Juma/ analima shamba
Kiima/ kiarifu
Kinyakyusa Juma/ ikulima kyalo
Kiima/kiarifu
N.k
3. Vitenzi vya lugha ya kiswahili na vile vya lugha za kibantu,hapa tunaangalia vipengele vifuatavyo;
A)mwanzo mwa vitenzi,
a)viambishi awali vya nafsi
b)viambishi awali njeo(wakati)
Mfano:
Kiswahili: a-na-lim-a
Kinyakuyusa. i-ku-lim-a
Kindali. a-la-lem-a
1(a-,i- na a-), 2(-na-, ku- na la-) 3(lim-,lim- na -lem-) 4(-a) Namna vilivyotumika;
Na(1) ni kuambishi awali cha nafsi. Ambapo hapo zote ni nafsi ya tatu (3)umoja,
Na(2)ni kiambishi awali cha njeo(wakati). Ambapo hapo umetumika wakati uliopo unaoendelea kwa luhga zote.
Na(3) ni mzizi wa neno katika lugha zote.
Na(4) kiambishi tamati maana. Maelezo zaidi yapo kipengele hiki hapa cha B).
B)mwisho mwa vitenzi. Hapa mwisho wa vitenzi vyote vya kiswahili na vile vya kibantu huishia na irabu mara nyingi ni irabu "a". Jaribu kutunga kitenzi chochote cha kibantu alafu kibadilishe kwa kiswahili.
4) mwisho pia ufanano hujitokeza katika sarufi ya lugha ya kiswahili na ile ya kibantu. Hapa tunaangalia mambo (2) mawili;
a) upatanisho wa kisarufi na
b) maumbo ya umoja na wingi.

Kwa mifano ya hoja ya 1,2 na ya 3 unaweza kutumia mifano ya lungha nyingine za kibantu unazozifahamu ukafananisha/ kuthibitisha.
Hoja ya nne (4) nitaifafanua baada ya kupata hoja zako ambazo pia ni za msingi kuhusiana na Chimbuko la kiswahili. Hasa mtazamo wako kuwa kiswahili ni kiarabu. Kwako Zamiluni Zamiluni. (Mtoa uzi utatusamehe bure kwa kudiverse uzi huu).
 
Hivi ipi ni lugha bora au zote ni sawa?

YES!

Lugha bora kuliko zote ni ile lugha uliyokuwa unaitumia wakati unakua (0-5 years old) au your mother tongue.

Hii ndio lugha unayoitumia wakati unafikiria.

Unafikiria ki-matumbi (mfano) kwanza halafu una-verbalize (sema) katika lugha nyingine kama kiswahili, kiingereza, nk.

Haya ni mawazo yangu tu. Nothing scientific.

NOTE: Utapata majibu mengi tofauti kwa sababu hujaainisha ni vigezo gani tutumie tunapopima U-BORAwa lugha.
 
Kuna lugha zilizoendelezwa zaidi ya zingine... Kwa mfano lugha zote za ulaya zina misamiati mingi ya kisaiyensi, kisheria, na kibiashara. Lugha hizi hazianzi hivyo lakini watuw wao wameendeleza baada ya muda mwingi.
 
Sawa mimi nitatumia hoja zifuatazo ambazo pia hutumiwa na wataalamu mbalimbali wa lugha ya kiswahili;
1. Kufanana kwa msamiati wa msingi wa lugha ya kiswahili na ule wa lugha za kibantu.
Mfano: kiswahili neno mtu
Kindali mundu
Kiwanji munu
Kiswahili maji
Kinyakyusa misi
Kisafwa minzii
Hii nitofauti na lugha nyingine mfano kiingereza- water(maji), a person (mtu)au lugha ya kiarabu pia ukapata maneno tofauti.
N.k pia unaweza kutumia lugha nyingine za kibantu kwa maneno hayo au mengine ukaona jinsi yanavyofanana au kukaribiana matamshi, na tofauti yake huwa ni ndogo sana.

2. Muundo wa sentensi za kiswahili na zile za kibantu.
Sentensi za lugha hizi huwa na muundo wa kiima(mtenda) arifu( taarifa ambayo huanzia kwenye kitenzi katika sentesnsi.
Mfano.
Kiswahili. Juma/ analima shamba
Kiima/ kiarifu
Kinyakyusa Juma/ ikulima kyalo
Kiima/kiarifu
N.k
3. Vitenzi vya lugha ya kiswahili na vile vya lugha za kibantu,hapa tunaangalia vipengele vifuatavyo;
A)mwanzo mwa vitenzi,
a)viambishi awali vya nafsi
b)viambishi awali njeo(wakati)
Mfano:
Kiswahili: a-na-lim-a
Kinyakuyusa. i-ku-lim-a
Kindali. a-la-lem-a
1(a-,i- na a-), 2(-na-, ku- na la-) 3(lim-,lim- na -lem-) 4(-a) Namna vilivyotumika;
Na(1) ni kuambishi awali cha nafsi. Ambapo hapo zote ni nafsi ya tatu (3)umoja,
Na(2)ni kiambishi awali cha njeo(wakati). Ambapo hapo umetumika wakati uliopo unaoendelea kwa luhga zote.
Na(3) ni mzizi wa neno katika lugha zote.
Na(4) kiambishi tamati maana. Maelezo zaidi yapo kipengele hiki hapa cha B).
B)mwisho mwa vitenzi. Hapa mwisho wa vitenzi vyote vya kiswahili na vile vya kibantu huishia na irabu mara nyingi ni irabu "a". Jaribu kutunga kitenzi chochote cha kibantu alafu kibadilishe kwa kiswahili.
4) mwisho pia ufanano hujitokeza katika sarufi ya lugha ya kiswahili na ile ya kibantu. Hapa tunaangalia mambo (2) mawili;
a) upatanisho wa kisarufi na
b) maumbo ya umoja na wingi.

Kwa mifano ya hoja ya 1,2 na ya 3 unaweza kutumia mifano ya lungha nyingine za kibantu unazozifahamu ukafananisha/ kuthibitisha.
Hoja ya nne (4) nitaifafanua baada ya kupata hoja zako ambazo pia ni za msingi kuhusiana na Chimbuko la kiswahili. Hasa mtazamo wako kuwa kiswahili ni kiarabu. Kwako Zamiluni Zamiluni. (Mtoa uzi utatusamehe bure kwa kudiverse uzi huu).
Nixon, wewe kiboko!!
lakini Baba ni Baba habadiliki wala habadili hadhi yake...ila mtoto anaweza badili jina au nickname au jina la utaani !!
Good luck.
 
Back
Top Bottom