- Source #1
- View Source #1
Nimekutana na hii Taarifa wakuu imenishtua kidogo, kwahiyo sisi huwa tunakula mahindi ya wanyama?
- Tunachokijua
- Mahindi ni zao maarufu sana ulimwenguni ambali limekuwa linatumika kwa shughuli mbalimbali kulingana na eneo husika.
Madai
Mtumiaji mmoja kupitia tandao wa Instagram alichapisha kipande cha video yenye taarifa kuwa “Sweet Corns ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu na Maize ni kw aajili ya mifugo”. Ujumbe huo kwa kiingereza ulisomeka kuwa;
MZUNGU MAN GIVES THE DIFFERENCE BETWEEN SWEET CORN & MAIZE - ‘SWEET CORN IS FOR HUMAN CONSUMPTION WHEREAS MAIZE IS FOR LIVESTOCK CONSUMPTION’’
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa yanapotosha uhalisia.
Tovuti mbalimbali za kilimo zinaeleza kuwa kumekuwa na mvutano mkubwa wa maana kati ya Maize na Corn ambapo kwa ufupi ni kuwa yote haya ni majina ya mahindi na yanarejelea kitu kimoja kutegemea na taifa ama lahaja ya eneo husika, ambapo kwa kiswahili yanaitwa mahindi.
Tovuti ya Hotculture ya nchini Uingereza inaeleza kuwa Corn na Maize ni misamiati inarojelea mmea mmoja ambapo kitaalamu hujulikana kama Zea Mays. Wanaendelea kuandika kuwa;
Maize (Mahindi) ndilo jina linalotumika zaidi kwa zao hili nchini Uingereza ni nafaka na ni sehemu ya familia ya mimea iitwayo Poaceae. Hili ni zao lenye matumizi mengi sana, ambalo binadamu wanalitumia kuanzia kama chakula hadi katika utengenezaji wa plastiki.
Tovuti ya Garden Betty inaeleza kuwa Kwa kawaida neno mahindi (maize) hutumika likimaanisha zao lenyewe katika mazingira ya kilimo. Wakulima hulima mahindi, lakini huuza mazao hayo sehemu mbalimbali kama corn, hasa pale yanapotumika kama chakula.
Machapisho yanaendelea kueleza kuwa Kwa neno corn ndilo linalotumika zaidi likihusishwa na vyakula, kama vile popcorn, ilhali neno maize halitumiki sana kuelezea vyakula hivyo—ingawa vyote vinatokana na zao moja la mahindi.
Britanicca wanaeleza kuwa Corn ambayo pia hujulikana kama Maize, Indian Corn au Zea Mays ni Mahindi ambayo hutumika kama chakula cha binadamu, chakula cha mifugo, nishati ya biofuel, na pia kama malighafi katika viwanda.
Aidha inataja kuwa kuna aina tano za mahindi kutokana na muundo au ugumu wa punje ambazo ni dent corn, flint corn, flour corn, sweet corn na Popcorn.