Je, kuna mtu anafahamu ndonya moja ni sawa na kg ngap?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
nipo kijijini week ya pili hii. nilikuwa nataka kununua bidhaa flani ya nafaka. ila kitu ambacho kinanipa shida ni kuwa upimaji wa watu wa huku unasumbua. mfano nataka kununua ulezi wao hawapimi kwa kilo. wana kipimo flani kama kibakuli wanaita NDONYA.
hivyo wanauza kwa ndonya.. badala ya kusema kilo kadhaa wao wanakwambia ndonya kadhaa... shida ni kuwa sifaham ndonya moja ni sawa na kg ngap.

lingine ni kuwa wanakipimo kikubwa cha debe. kama ndoo ya bati ya pembe nne. wanaita debe. hivyo wanakwambia debe moja tsh kadhaa.

swali je kuna mtu anafaham ndonya moja ni sawa na kg ngap?
debe moja ni sawa na kgs ngap?
gunia moja linajazwa kwa debe ngapi?

tupeane msaada katika hili tafadhali.
 
Nunua ndonya moja na debe moja weka ktk mifuko tofauti. Nenda dukani mpe buku akupimie. Case closed
huu ushauri ni mzuri ukubwa wa ndonya na debe zinatofautiana naweza kukupa makadilio yangu yakawa tofauti na ndonya za uko uliko
 
Ebu wenye lugha waje waseme huwa wanamaanisha nn ?? Nadhani itaondoa utata
 
Mkuu nunua sample nenda madukani kapime kwenye kilo mfano hicho kipimo vikiwa kumi then nenda navyo mpaka shop kapime utajua ujazo huo ni kg ngapi!
 
Mbeya moja hiyo,Chukua nenda kwenye mzani kapime ili upate uhakika.
 
Mkuu, hili nalo mpaka uje kuuliza jf kweli?
Chukua/ nunua hiyo nafaka yako ndonya 1 then tafuta mzani (nenda hata dukani au sokoni) omba mhusika akusaidie kupima ujue ni kg ngapi. Alaf pia ulizia kwa wenyeji, kwenye debe 1 zinaingia hizo ndonya ngapi? Utapata majibu. Hili sio jambo la kuingia darasani ni uelewa tu wa kawaida.
 
hivyo vipimo mbeya vipo sana. Kama alivyosema Copy hapo juu, nunua hiyo ndonya moja then tafuta sehem yenye mzani muombe akupimie, simple and clear.
 
Katika mazingira ya kawaida, vipimo hiv mara nyingi huwa ni nusu kilo au kilomoja!
 
Ndonya zipo nyingi ipo ndogo ya kati na kubwa ndogo inaitwa sikukuita hiyo ni robo kilo na kidogo ya kati ni nusu kilo kasoro na kubwa ni zaidi ya nusu kilo debe ni kilo 21.5 ni vipimo vinavyoiba tu kutegemea ujazo na sio uzito wa bidhaa husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…