Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 14,578
- 31,662
Sio kwamba umeshindwa totally kwamba haiwezekani.Kwa kutumia hiyo mantiki yako mbovu, kama mimi nikichagua kwenda benki kuu kuiba mabilioni ya pesa, lakini nikashindwa kwa sababu kuna walinzi na mfumo mzima wa kuingia ndani ni mgumu, utasema sikuwa na free will ya kuchagua kwenda kuiba?
Freewill ili ikamilike lazima uweze kupanga, kuchagua na kutake ACTION.🤣🤣 Boom! Soma hayo maneno niliyo yabold , Umekiri mwenyewe kwa maandishi yako kuwa freewill ya kuiba ninayo, mjadala umeisha!
Kumbe ulikuwa unabisha nini sasa wakati sasa hivi umekubali kuwa binadamu ana free will ya kupanga na kuchagua matendo yake? Asante kwa kukiri.
Kuna uthibitisho wa binadamu kuumba??Kabla hatujaendelea mbele wewe umeumbwa na nani?
Au hoja yangu ni ya kumkosoa Mungu?
Hakuna sababu zozote za WaIsrael kukatazwa kula ngamia, kitimoto, sungura, Pweza, crabs, ngisi na Kambale.Unajua watu wengi hawajui kabisa kwa nini wana Israel walikatazwa kula baadhi ya vyakula
Hata sisi tuliobahatika kujua baadhi ya vitu ukimweleza mtu anakuona kubwa jinga ....most people are set to perish
No one take a moment to think why this
Wewe kuwepo duniani kama kiumbe logically uliumbwaKuna uthibitisho wa binadamu kuumba??
Uthibitisho wa kuumbwa ni upi?Wewe kuwepo duniani kama kiumbe logically uliumbwa
Anayebakwa, anayeibiwa na anayeuwawa utashi wake unamsaidia nini? Yeye lawama ampe nani?Umepewa akili na utashi wa kuamua mambo.
Maovu mfsnye nyie lawama mumpe mungu?
Mungu anayezungumziwa na binaadamu hayupo, je yupo Mungu anayezungumziwa na kiumbe gani?Mungo huyu watu wanaomzungumzia makanisani,,sijui huko kwenye mavyombo ya Habari kiufupi mungu anayezungumziwa na binadamu hayupo hizi Habari za mungu ni za kufikirika hata wale waliokuwa wanasema na mungu walikuwa ni watu ambao walipitia matukio ya nature inavyotaka ndo wakaamua kubambikiza kama hayo ni matukio ya kimungu ila sio kama watu wanavyosema kwamba Kuna mungu wao mpenda Sadaka
Hili la kuruhusu matatizo kuwepo ni kawaida ya nature ili kubalance,,,fikiria watu wangekuwa wanazaliwa tu Hawafi?
Umewahi kujiuliza kwann kuna kuzaaa?
Usingeumbwa usingekuwepo.Uthibitisho wa kuumbwa ni upi?
Nani aliniumba?
Aliyemuumba mungu ni nani ?Usingeumbwa usingekuwepo.
Aliyemba ni Mungu.
Kwani wewe unahisi uliumbwa na nani?
Sijaumbwa, nimezaliwa.Usingeumbwa usingekuwepo.
Aliyemba ni Mungu.
Kwani wewe unahisi uliumbwa na nani?
Mungu sio kiumbe hadi aumbweAliyemuumba mungu ni nani ?
Ni nani aliyeamua uzaliwe?Sijaumbwa, nimezaliwa.
Mbona wengi tu wamefia tumboni?!Ni nani aliyeamua uzaliwe?
Na vipi kama ungefia tumboni kabla ya kuzaliwa unadhani ni nani angekuwa ameamua au kupanga hilo?
Kama Mungu sio kiumbe ni kitu gani?Mungu sio kiumbe hadi aumbwe
Halafu mbona maswali yangu unakwepa kuyajibu?
Mungu ni Mungu muumba ardhi na mbingu pamoja na vyote vilivyopo ulimwenguniKama Mungu sio kiumbe ni kitu gani?
Tthibitisha haya madai yakoMungu ni Mungu muumba ardhi na mbingu pamoja na vyote vilivyopo ulimwenguni
Kufia tumboni maana yake hicho kiumbe umri wake uliopangwa na Mungu ndio umeishia hapo.Mbona wengi tu wamefia tumboni?!
Kwa nini unafikiri yuko anayepanga mimba kufia tumboni? Kama yuko anayeamua mimba ifie tumboni kwa nini alisibabisha mimba itungwe? Point ni nini kusababisha mimba itungwe halafu ifie tumboni??
Unafikiri na umeaminishwa tu hivyo.Kufia tumboni maana yake hicho kiumbe umri wake uliopangwa na Mungu ndio umeishia hapo.
Ingekuwa kwenye ishu ya umri tunajipangia wenyewe kila mtu angejikadiria kuishi miaka 1000 na kuendelea ila ndio haiwezekani yuko muamuzi juu ya hilo.