mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 10,487
- 14,559
Kwa nini hao wajapan wasijipangie miak 300?Unafikiri na umeaminishwa tu hivyo.
Hakuna maana yoyote ya huyo mungu kama yupo kumtesa mwanamke kwa kuumba mimba halafu ifie tumboni.
Suala la watu wote kutaka kuishi miaka 1,000 ni assumptions zako tu pia. Kuna watu wanataka kufa mapema , hawaoni maana yoyote ya kuendelea kuwepo duniani.
Suala la urefu wa umri wa kuishi ni la kimaendeleo zaidi na mipango ya binadamu ndio maana Ulaya, Japan, Korea na Singapore wastani wa umri wa kuishi ni miaka 85 wakati Africa ni miaka 64.
Binadamu anaboresha maisha yake kila siku, Sayansi sio kama mazingaombwe ya dini watu wanayoaminishwa bali ni mchakato mrefu wa utafiti wenye kupatia na kukosea lakini kila hatua ikiwa ni kusonga mbele, ndio maana leo tunaongelea wastani wa kuishi wa miaka 80 tofauti na miaka 6000 iliyopita ambapo wastani wa kuishi ulikuwa ni miaka 35 tu.Kwa nini hao wajapan wasijipangie miak 300?
Huwezi kutumia kifo kuthibitisha uwepo wa mungu, badala yake zaidi inaweza kuwa inathibitisha kinyume chake.Kwa nini hao wajapan wasijipangie miak 300?
Nani ni mpangaji wa kifo?Huwezi kutumia kifo kuthibitisha uwepo wa mungu, badala yake zaidi inaweza kuwa inathibitisha kinyume chake.
Kwanini mkuu umeuliza aliyemuumba mungu?Aliyemuumba mungu ni nani ?
Ndio maana mie huwa naona hata wenye kuona kwamba hakuna Mungu ni moja tu ya mitazamo au chaguzi zilizopo, wengi wasioamini Mungu na kusema hayupo walikuwa waumini wa dini na hata huyo Mungu wanayesema hayupo ni wa hizi dini mbili, lakini sio wote waliyoacha kuamini Mungu wa hizo dini basi alikana kabisa uwepo wa Mungu bali wapo waliyochagua kuamini Mungu tofauti na dini.Wait, umebase upande mmoja wa kuonesha hakuna Mungu Well... utafika wakati utaona matukio ya kuonesha kuwa Mungu yupo. Ni masuala ya nyakati tu na upo sahihi
Kwa ufupi wanaosema Mungu yupo na wanaosema Mungu hayupo wote wapo sahihi kutegemea kila mtu amepitishwa kwenye njia gani
Na kwa wewe unavyoona watu wanapinga dhana nzima ya uwepo wa Mungu au ubishani upo kwenye hayo mambo uliyoyataja kama sifa zake,malengo yake, makazi yake?Nikuhakikishie Mungu yupo, ila historia yake, sifa zake, makazi yake, lengo ama malengo yake kuhusu ulimwengu ndo vinaleta utata mwingi.
Mimi nilishaamua kuacha blank iyo sehemu maana ata yeye hajataka iwe na majibu ndo maana karuhusu macho yangu yaone Maji ila yasione Upepo kwaiyo na deal na na maisha yangu kulingana na vile alivoniumba na kuruhusu niwe kulingana na uwezo wangu fullstop.
Pole sana kwa kumpoteza rafiki yako, umenipa majonzi sana kwasababu umenikumbusha nilivyompoteza rafiki yangu mwaka 2010 sababu ya pumu, siwezi sahau hadi siku nitakayoingia kaburini.NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Kwa sababu anasema binadamu tupo kwa hiyo tumeumbwa na aliyetuumba ni mungu, kama hiyo ni hoja basi mungu kuwepo naye atahitaji muumbaji wake ili kutimiza Sheria ya kila kitu kilichopo kuwa na muumbaji wake(infinite regress)Kwanini mkuu umeuliza aliyemuumba mungu?
Mimi nilivyoelewa kwenye hilo suala la uumbaji ni kwamba vipo vilivyoumbwa na vipo vilivyotokana na hivyo vilivyoumbwa, na pia uumbaji ni katika miongoni mwa sifa za kipekee za huyo Mungu.Kwa sababu anasema binadamu tupo kwa hiyo tumeumbwa na aliyetuumba ni mungu, kama hiyo ni hoja basi mungu kuwepo naye atahitaji muumbaji wake ili kutimiza Sheria ya kila kitu kilichopo kuwa na muumbaji wake(infinite regress)
Mtihani hupima uelewa wa wanafunzi ambao mwalimu yeye haujui. Ila Mungu anapima nini ambacho yeye hakijui? Anampaje mtihani mbakaji ambae anajua kabisa huyu atabaka tu. Pale anampima nini? Kwamba mbakaji anaweza kubadiri maamuzi asibake au.. Usifananishe mfano wa mitihani ya waalimu hawa ambao wanapima kitu ambacho hawakijui ila Mungu anapima kitu ambacho matokeo anayajua kabisa sababu yeye anajua kila kitu. Hapo ndo watu wanapouliza kama yeye anajua kila kitu kwann akupe mtihani ambao anajua matokeo yake?!Hayo maswali yako hayapaswi kuulizwa hata na mtoto mdogo mwenye akili timamu.
Njaa isingekuwepo wewe ungeijulia wapi?
Hiyo ni mitihani tuliyopewa kwa hiyo unapaswa kutumia akili yako uliyozawadiwa kuikwepa.
Yaani swali lako halinq utofauti na kumuuliza mwalimu"Mwalimu kama wewe una nia nzuri na ufaulu wa wanafunzi wako kwa nini unatupatia mtihani,ni kwa nini usiandike kwenye ripoti kwamba darasa lote tumefaulu"
Kwanza pole sana kuhusiana na rafiki yako.Sio kwamba natafuta sifa au nataka kubishana na mtu kuhusu imani. Lakini nikitazama yanayoendelea duniani vita, mauaji, watoto wanaoteseka, njaa, magonjwa na watu wasio na hatia kupoteza maisha naanza kujiuliza kwa dhati kama Mungu yupo na ana uwezo wote, kwa nini anaruhusu mateso haya yaendelee?
Huenda kuna majibu ambayo mimi siyajui. Lakini kwa sasa, swali hili limenifanya nianze kujiuliza kwa kina kuhusu uwepo wa Mungu.
Ningependa kusikia mawazo yenu Je, wewe unaamini Mungu yupo? Na kama ndiyo, unaelezaje uwepo wa mateso makubwa duniani?
NB: Bado nipo kwenye majonzi ya kumpoteza rafiki yangu, aliyeteseka kwa ugonjwa wa sickle cell. Na aliyeishi maisha ya maumivu mpaka kuondoka kwake. Kijana mdogo miaka 23.
Kilichokuondoa kwenye hiyo shida ni kanuni za asili tu na sio huyo Mungu.Kuhoji sio kutokujua bali kujiuliza kwanini unahisi nafsini mwako yupo..
I was once a non believer ila nilipo fikia the verge of breaking na akaingilia kati kuni okoa.. Hapo si kutaka hata kuuliza kwanini yupo
Sasa kama huyo Mungu ana zone ya ubaya, ubaya wa shetani ni nini ?Nashauri kasome the stori of job..
Au kaangalie video YouTube.. Inakusaidia kumwona Mungu katika zone zote za ubaya na uzuri... Akiwa na lengo la kukujenga kiimani
Mungu anaejua kesho yako kabla hujazaliwa aliamua kukufunza Ili ubadirike.Actually, nilikosea kusema I believe...
I don't believe I know intuitively..
That surpasses any explanation because nitadogosha kile nafsi yangu inakijua
Nilikuwa kama wewe mpaka pale Mungu alipoamuwa kunifunza, na nina mshukuru kuniokoa maana ningekuwa mfano mbaya sana
Kama jina la Yesu linaondoa Pepo basi jina la Yesu liondoe ukosefu wa ajira, magonjwa muhimbili, ajalai, vita n.kKwanini ukitaja jina la Yesu pepo linakimbia ? Kama huyu mtu hayupo lisingeogopa kwanini ukitaka jina la Yunes halitoki?
Mtihani hupima uelewa wa wanafunzi ambao mwalimu yeye haujui. Ila Mungu anapima nini ambacho yeye hakijui? Anampaje mtihani mbakaji ambae anajua kabisa huyu atabaka tu. Pale anampima nini? Kwamba mbakaji anaweza kubadiri maamuzi asibake au.. Usifananishe mfano wa mitihani ya waalimu hawa ambao wanapima kitu ambacho hawakijui ila Mungu anapima kitu ambacho matokeo anayajua kabisa sababu yeye anajua kila kitu. Hapo ndo watu wanapouliza kama yeye anajua kila kitu kwann akupe mtihani ambao anajua matokeo yake?!
Sio wajibu wa Sayansi kukanusha uwepo wa mungu ila ni wajibu wa waamini mungu kuthibitisha uwepo wake.Uwepo wa Mungu ni suala la imani, falsafa na namna mtu anavyotafsiri ushahidi na uzoefu wa maisha, si jambo ambalo sayansi imeweza kulithibitisha au kulikanusha.