Je, Kuna Taasisi ya ovyo Kabisa Nchini Kuizidi TANESCO?

kua mstahimilivu na mwenye subra hivi karibuni tu marekebisho yanayofanyiwa kazi yakikamilika changamoto hii itakua imeisha...
Kwa historia ya utendaji wa hovyo wa TANESCO na ahadi zao nyingi za uongo, siamini kama kuna anayeweza kuyaamini maelezo yoyote ya TANESCO na Wizara ya kutatua tatizo la umeme, mpaka tutakapoona. Ahadi na maelezo ya uwongo tumeambiwa mara nyingi sana.
 
Huyo unayemsihi amwajibishe MTU wa TANESCO ndiye alipaswa kuwa wa kwanza kuwajibishwa na wananchi.
Nitajie taasisi 2 tu za serikali ambazo zinafanya vizuri kwa angalau 80%?
 
Si tanesco tu taasisi zote zinazosimamiwa na serikali ni kisanga
 
ndio maana tuanasisitiza subra na ustahimilovu

kipindi kama hicho huko nyuma ilikuepo tatizo la maji na madawa mahospitalini, ghadhabu na kebehi kama hizi zilikua nyingi sana tena kulikoni hizi. Matatizo yale yametatuliwa wanaharakati kimyaaaa hamna ghadhabu tena mnainjoy tu huduma hamna maneno mbofumbofu tena 😀

hii shida ya umeme inakwenda kutatuliwa na mtatulia bila maneno ya shukrani mnainjoy matunda ya serikali ya awamu ya 6 chini ya kiongozi msikivu sana Dr.Samia Suluhu Hassan
 
CC: chama cha Walimu Tanzania.
 
Kumlaumu mfanyakazi, meneja au waziri ni makosa makubwa sana hao hawana mamlaka wala uwezo wa kubadili order yoyote kutoka juu zaidi ya kutekeleza tu

Katika majukwaa ya Makonda huko anakozunguka alifika Arusha akakutana na meneja wa TANESCO Arusha na wananchi wenye kero ya umeme

Alichosema meneja ni maelezo ya Mheshimiwa rais
Makonda akauliza maelekezo umepewa wewe au wizara meneja anasema ni wizara
Makonda aliona mambo yameingiliana akamwambia usijichanganye

Tatizo ni rais na wala siyo yeyote zaidi
 
Si tanesco tu taasisi zote zinazosimamiwa na serikali ni kisanga
Nakubaliana nawe. Kwa aina ya watu waliopo Serikalini na taasisi zake, hata wangepewa genge la mama nitilie waliendeshe, watashindwa. Hawa watu sijui ni kitu gani wanaweza kujivunia kuwa wanafanya vizuri.
 
Yes. Taasisi ya Raisi na ikulu
 
Upuuzi mtupu!

Niambie ni wapi kwenye uhakika wa maji? Maeneo mengi wananchi wanategemea maji ya mvuana mito, au unataka kusema mvua zinazonyesha ni matunda ya serikali ya awamu ya 6?

Subiri mvua ziishe halafu uje utoe taarifa jinsi Serikali ya awamu ya 6 ilivyomaliza tatizo la maji.
 
CCM, baba kazaliwa kakua kasoma kamaliza katafuta mchumba kaoa wamezaa mtoto anatembea, bado mama, baba na mtoto wao wanakwenda mbugani kuchota maji kwenye gema ambalo tembo alichimba kwa ajili ya matumizi yake na mwae, eti mama ameupiga mwingi.
 
Mchawi mkuu ni ccm ambaye anazalisha serikal na serikali inazalisha taasisi. Baba mkuu ni mavi matupu vp watoto wake na wajukuu wawe wa maana?
Aliyetengeneza na kuasisi mfumo bovu wa nchi hii ni nyerere. Hawa wa sasa wanapita humohumo. Na mfumo unawanufaisha hawako tayar ubadilike
 
Si tanesco tu taasisi zote zinazosimamiwa na serikali ni kisanga
Upo sahihi.

Kuna mambo ya hovyo sana nchi hii.

Hivi karibuni nilienda mkoani Njombe, Wilaya ya Ludewa. Nikakutana na diwani (CCM), analalamika kuwa katani kwake waliambiwa wamepewa pesa ya mradi wa maji wa kata takribani bilioni 1.5 lakini mpaka sasa kazi iliyofanyika haiwezi kuzidi hata milioni 300, lakini wanalazimishwa waseme kuwa matanki ya maji yamejengwa 3 wakati limejengwa 1, wanalazimishwa waseme kuwa maji tayati yanatoka wakati mpaka sasa maji wanayopata ya mgao ni ya mradi wa zamani uliokuwa umefadhiliwa na Kanisa Katoliki. Anasema amehangaika sana kufuatilia na kulalamika mpaka kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Ludewa dhidi ya uwongo wa pesa iliyotumika, lakini anaambiwa kuwa atulie kwa sababu hiyo pesa, kiasi kikubwa imerudi kwa wakubwa huko wizarani.

Yaani hawa watu wa Serikali, ni hovyo kila mahali.
 
Naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…